MTIBWA YAPATA USHINDI DHIDI YA PRISONS

Author
AME ALLY1BAADA ya kufungwa mechi mbili kanda ya ziwa, mabao 2-1 na Kagera Sugar, 1-0 dhidi ya Stand United na sare ya 1-1 ya mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Azam fc , hatimaye wakata miwa wa Manungu, Turiani, Mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mechi ya kiporo ya ligi kuu iliyomalizika jioni hii uwanja wa Manungu Complex.
Kabla ya mechi hii Mtibwa Sugar walikuwa nafasi ya 11 katika msimamo wakijikusanyia pointi 24 baada ya mechi 21.
Leo ilikuwa mechi ya 22 na kuvuna pointi tatu kumewasogeza mpaka nafasi ya 6 katika msimamo, pointi moja nyuma ya Mgambo wanaoshika nafasi ya tano kwa pointi 28 baada ya kutoka suluhu dhidi ya Azam fc jioni CCM Mkwakwani Tanga.
Hali imezidi kuwa dhoofu kwa Prisons ambao baada ya kipigo cha leo wanaendelea kuwa nafasi ya 13 kwa pointi zao 21 baada ya kucheza mechi 22.

0 comments:

Post a Comment