MAAFANDE wa JKT Mgambo kutoka
Kabuku, Handeni, Mkoani Tanga wamezidi kufifisha matumaini ya Azam fc
kutetea ubingwa wao baada ya kuwalazimisha suluhu (0-0) katika mechi ya
ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa CCM
Mkwakwani Tanga.
Mechi hiyo ilikuwa na ushindani kwa timu zote na dakika za majeruhi ilibaki kidogo Mgambo kufunga goli.
Kipindi cha pili Mgambo walitengeneza nafasi nyingi kuliko cha kwanza na dhahiri safu ya ulinzi haikuwa imara.
Hii ni sare ya tatu mfululizo Azam wanavuna katika mechi mbili za ugenini na moja ya nyumbani.
Walianza kutoka sare ya 1-1 na
Mbeya City, kisha 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mwishoni mwa juma lililopita
na leo wanatoka suluhu Tanga.
Matokeo hayo yanafanya Azam waendelee kukaa nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 39 baada ya kucheza mechi 21.
Yanga wanazidi kukaa salama kileleni kwa pointi zao 46 kufuatia kushuka dimbani mara 21.
Mgambo wao 28 katika nafasi ya tano baada ya kucheza mechi 21.
Msimu uliopita, mechi ya kwanza
Azam walishinda 2-0 uwanja wa Chamazi, mechi ya marudiano huko Tanga
Azam wakashinda 2-0 tena uwanja wa Mkwakwani.
0 comments:
Post a Comment