Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amekabidhiwa hundi ya
zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya kufidia ujenzi wa upande wa nyumba yake
uliodondoka.
Wakati akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Kampuni ya Bima ya UAP kwa
ushirikiano na Benki ya CRDB, Diamond alisema ukuta wa nyumba yake
ulianguka wakati akiwa anamuuguza mama yake aliyekuwa katika hali mbaya.
“Ilikuwa ghafla ukuta wa nyumba yangu ya Tegeta ukaanguka wakati huo
nilikuwa natakiwa kulipia fedha kwa ajili ya kurekodi wimbo wangu mpya.
“Hivyo nisingekuwa nimejiunga na bima sijui sasa ningekuwa kwenye hali
gani? Ni kipindi kigumu sana kwangu,’’ alieleza Diamond huku akiwataka
Watanzania wajiwekee bima kwa kuwa ina msaada mkubwa unapopatwa na
majanga mbalimbali ya vitu ulivyokatia bima hiyo.
Naye, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa UAP, Raymond Komanga,
aliwasisitizia Watanzania waondoe fikra za kwamba bima inayokatwa ni ya
gari pekee bali wakate bima za aina mbalimbali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment