Waziri wa maswala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaiserry amethibitisha
kuwa watu 15 wameuawa huku wengine 53 wakijeruhiwa kufuatia shambulizi
la alfajiri katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya.miongoni mwa
waliokfariki ni walinzi wawili wa mlango wa chuo hicho.Akizungumza
kutoka Garissa Nkaiserry amesema kuwa oparesheni ya kuwasaka wahalifu
hao itaendelea hadi mateka wote waokolewe
.Serikali
ya Kenya imemtaja Mohammed Kuno kama mshukiwa mkuu aliyepanga njama za
shambulizi la chuo kikuu mjini Garissa.Katika taarifa kwa vyombo vya
habari waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Nkaiserry alitoa zawadi ya
dola 53,000 kwa mtu yeyote atakayemkamata mshukiwa huyo ama kutoa habari
zake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment