Hofu ya kukataliwa kwa Katiba Mpya
kumeifanya Serikali ivunje
makubaliano ya Kituo cha Demokrasia
Tanzania (TCD), kwamba Kura ya
Maoni isitishwe hadi baada ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Hadi sasa hatujui nani atakuwa
madarakani kati ya upinzani au
chama tawala. Hata hivyo, CCM
inaipigia debe Katiba Mpya kwa
mtindo uleule wa kulazimisha.
Kuna madai kwamba kunafanyika hila
ili Daftari la Wapigakura lisiboreshwe
kwa lengo la kufanikisha mpango huo.
Mbona Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), ilisema wafadhili walishatoa
fedha za kuboresha daftari hilo? Pia,
ilisema hakuna uchaguzi
utakaoendeshwa bila kuboresha
daftari hilo.
Nini kimetokea hapo katikati? Hofu ni
Katiba Inayopendekezwa kuja
kukataliwa na umma, hivi Serikali
imeona heri iendelee kuisukuma
angalau ikubalike na umma wa
Tanzamia kwa kutumia nguvu?
Hata hivyo, ukweli ni kwamba katiba
hii imekataliwa na wananchi wengi na
ina maana imekataliwa pia na Mungu,
kwa sababu ‘sauti ya wengi ni sauti ya
Mungu.’ Ukiisoma Katiba
Inayopendekezwa utagundua kuwa ni
ya “kulinda masilahi” ya watu
wachache.
Huku ni kuvuruga uchaguzi kwa
kutumia katiba mbaya na kanuni
mbaya ambazo mwishowe huleta
machafuko, vita na mauaji kama yale
yaliyotokea Kenya katika uchaguzi wa
mwaka 2007.
Rais Mwai Kibaki alilazimisha ushindi
na akaapishwa usiku usiku mbele ya
watu wachache. Ukisoma alama za
nyakati unagundua kwamba hayo
ndiyo yanayokuja mbele yetu. Je,
tukae kimya?
Uchaguzi wa haki na huru ndiyo
ukomavu wa demokrasia unaoweza
kuepusha machafuko, vurugu,
malalamiko na mauaji hapa nchini.
Mambo sita
Ili kuepusha Katiba Inayopendekezwa
isilete maafa kuna mambo sita ya
kufanya kwa wananchi, vyama vya
upinzani, madhehebu ya dini,
wanaharakati, wasomi na wananchi
wenye mapenzi mema.
Mosi, wadau wa demokrasia, utawala
bora na amani ambao ni wanasiasa,
viongozi wa dini, wanaharakati na
wananchi, wadai kuboreshwa kwa
Daftari la Wapigakura ili kuwapa
watu wengi fursa ya kutumia haki ya
kikatiba kupiga kura hasa vijana.
Kama kweli Serikali ya CCM inaamini
juu ya demokrasia na inasema
inakubalika, basi wasiwe na hofu
kukataa kuboresha daftari hilo.
Pili, wapinzani na wadau wa siasa
lazima wailazimishe Serikali kuunda
tume huru ya uchaguzi ili kuhakikisha
uchaguzi unakuwa huru na wa haki
kwa kila chama.
Jambo la tatu ni kwamba sheria za
uchaguzi ziboreshwe ili kujenga
mazingira ya usawa katika ushindani
kwa vyama vyote. Kila chama kifuate
sheria na kanuni bila kujali kipi ni
chama tawala.
Mgombea binafsi aruhusiwe kama
ilivyoamriwa na Mahakama ya Rufaa.
Hii ni katika kupanua wigo wa
demokrasia ya kweli, kama kweli CCM
inajigamba kudumisha demokrasia na
utawala nchini .
Jambo la nne, vyombo vya dola
visiingilie mchakato wa uchaguzi.
Hata pale vinaponusa kwamba CCM
inashindwa, waiache kwani hii ndiyo
demokrasia ya kweli.
Zisitumike nguvu bila sababu ya
maana na hilo litaepusha vurugu,
kwani mara nyingi wanaoanzisha fujo
na vurugu katika vituo vya uchaguzi
ni vyombo vya dola kwa kisingizio cha
kulinda amani.
Tano, kila chama kisaini makubaliano
kwamba kutokana na mazingira hayo
ya uwazi, basi atakayeshindwa
akubaliane na matokeo. Hii ndiyo
demokrasia ya kweli inayoambatana
na utawala bora.
Sita, wananchi wote wenye mapenzi
mema na nchi yao wahamasishwe
kujiandikisha katika daftari na siku ya
uchaguzi wakafurike vituoni kwenda
kupiga kura kwa kuchagua viongozi
bora na siyo ‘bora viongozi.’
Kuhusu kura ya maoni ya Katiba
Mpya, kuna ushauri mwingi
unaendelea kutolewa na wasomi,
viongozi wa dini, wanaharakati, watu
binafsi kwamba ni vyema kura hiyo
ikaahirishwa kwa masilahi mapana ya
Taifa lote.
Kuna wanaotoa hoja kwamba, kuna
haraka gani ya kupata katiba mpya,
kwani hata ikipitishwa haitaweza
kutumika katika uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
Kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete
alianzisha mchakato wake, hatuna
budi kumpongeza ila sehemu iliyobaki
tumwachie Rais ajaye ama awe
kutoka CCM au upinzani.
Wananchi wengi wanafikiri ikiwa
mchakato mzima wa upatikanaji wa
Katiba Inayopendekezwa, umekiuka
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
maana yake ni kwamba Katiba hiyo ni
feki. Haina uhalali kwa sababu
imekosa maridhiano na hivyo
haikubaliki kwa wananchi. Mungu
wajaalie Watanzania ujasiri wa
kukataa kuburuzwa. Siasa zitapita
lakini Tanzania haitapita kamwe.
Tukumbuke kuwa uchaguzi wa
mwaka huu ni kipimo cha ukomavu
wa demokrasia na utawala bora
katika nchi yetu. Je, mtihani huu
tutafaulu au tutafeli?
kumeifanya Serikali ivunje
makubaliano ya Kituo cha Demokrasia
Tanzania (TCD), kwamba Kura ya
Maoni isitishwe hadi baada ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Hadi sasa hatujui nani atakuwa
madarakani kati ya upinzani au
chama tawala. Hata hivyo, CCM
inaipigia debe Katiba Mpya kwa
mtindo uleule wa kulazimisha.
Kuna madai kwamba kunafanyika hila
ili Daftari la Wapigakura lisiboreshwe
kwa lengo la kufanikisha mpango huo.
Mbona Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), ilisema wafadhili walishatoa
fedha za kuboresha daftari hilo? Pia,
ilisema hakuna uchaguzi
utakaoendeshwa bila kuboresha
daftari hilo.
Nini kimetokea hapo katikati? Hofu ni
Katiba Inayopendekezwa kuja
kukataliwa na umma, hivi Serikali
imeona heri iendelee kuisukuma
angalau ikubalike na umma wa
Tanzamia kwa kutumia nguvu?
Hata hivyo, ukweli ni kwamba katiba
hii imekataliwa na wananchi wengi na
ina maana imekataliwa pia na Mungu,
kwa sababu ‘sauti ya wengi ni sauti ya
Mungu.’ Ukiisoma Katiba
Inayopendekezwa utagundua kuwa ni
ya “kulinda masilahi” ya watu
wachache.
Huku ni kuvuruga uchaguzi kwa
kutumia katiba mbaya na kanuni
mbaya ambazo mwishowe huleta
machafuko, vita na mauaji kama yale
yaliyotokea Kenya katika uchaguzi wa
mwaka 2007.
Rais Mwai Kibaki alilazimisha ushindi
na akaapishwa usiku usiku mbele ya
watu wachache. Ukisoma alama za
nyakati unagundua kwamba hayo
ndiyo yanayokuja mbele yetu. Je,
tukae kimya?
Uchaguzi wa haki na huru ndiyo
ukomavu wa demokrasia unaoweza
kuepusha machafuko, vurugu,
malalamiko na mauaji hapa nchini.
Mambo sita
Ili kuepusha Katiba Inayopendekezwa
isilete maafa kuna mambo sita ya
kufanya kwa wananchi, vyama vya
upinzani, madhehebu ya dini,
wanaharakati, wasomi na wananchi
wenye mapenzi mema.
Mosi, wadau wa demokrasia, utawala
bora na amani ambao ni wanasiasa,
viongozi wa dini, wanaharakati na
wananchi, wadai kuboreshwa kwa
Daftari la Wapigakura ili kuwapa
watu wengi fursa ya kutumia haki ya
kikatiba kupiga kura hasa vijana.
Kama kweli Serikali ya CCM inaamini
juu ya demokrasia na inasema
inakubalika, basi wasiwe na hofu
kukataa kuboresha daftari hilo.
Pili, wapinzani na wadau wa siasa
lazima wailazimishe Serikali kuunda
tume huru ya uchaguzi ili kuhakikisha
uchaguzi unakuwa huru na wa haki
kwa kila chama.
Jambo la tatu ni kwamba sheria za
uchaguzi ziboreshwe ili kujenga
mazingira ya usawa katika ushindani
kwa vyama vyote. Kila chama kifuate
sheria na kanuni bila kujali kipi ni
chama tawala.
Mgombea binafsi aruhusiwe kama
ilivyoamriwa na Mahakama ya Rufaa.
Hii ni katika kupanua wigo wa
demokrasia ya kweli, kama kweli CCM
inajigamba kudumisha demokrasia na
utawala nchini .
Jambo la nne, vyombo vya dola
visiingilie mchakato wa uchaguzi.
Hata pale vinaponusa kwamba CCM
inashindwa, waiache kwani hii ndiyo
demokrasia ya kweli.
Zisitumike nguvu bila sababu ya
maana na hilo litaepusha vurugu,
kwani mara nyingi wanaoanzisha fujo
na vurugu katika vituo vya uchaguzi
ni vyombo vya dola kwa kisingizio cha
kulinda amani.
Tano, kila chama kisaini makubaliano
kwamba kutokana na mazingira hayo
ya uwazi, basi atakayeshindwa
akubaliane na matokeo. Hii ndiyo
demokrasia ya kweli inayoambatana
na utawala bora.
Sita, wananchi wote wenye mapenzi
mema na nchi yao wahamasishwe
kujiandikisha katika daftari na siku ya
uchaguzi wakafurike vituoni kwenda
kupiga kura kwa kuchagua viongozi
bora na siyo ‘bora viongozi.’
Kuhusu kura ya maoni ya Katiba
Mpya, kuna ushauri mwingi
unaendelea kutolewa na wasomi,
viongozi wa dini, wanaharakati, watu
binafsi kwamba ni vyema kura hiyo
ikaahirishwa kwa masilahi mapana ya
Taifa lote.
Kuna wanaotoa hoja kwamba, kuna
haraka gani ya kupata katiba mpya,
kwani hata ikipitishwa haitaweza
kutumika katika uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
Kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete
alianzisha mchakato wake, hatuna
budi kumpongeza ila sehemu iliyobaki
tumwachie Rais ajaye ama awe
kutoka CCM au upinzani.
Wananchi wengi wanafikiri ikiwa
mchakato mzima wa upatikanaji wa
Katiba Inayopendekezwa, umekiuka
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
maana yake ni kwamba Katiba hiyo ni
feki. Haina uhalali kwa sababu
imekosa maridhiano na hivyo
haikubaliki kwa wananchi. Mungu
wajaalie Watanzania ujasiri wa
kukataa kuburuzwa. Siasa zitapita
lakini Tanzania haitapita kamwe.
Tukumbuke kuwa uchaguzi wa
mwaka huu ni kipimo cha ukomavu
wa demokrasia na utawala bora
katika nchi yetu. Je, mtihani huu
tutafaulu au tutafeli?
0 comments:
Post a Comment