NICK MINAJ ‘AMWAGANA’ NA MPENZI WAKE

Author
Mwanamuziki asiyekwisha vituko wa nchini Marekani,Nick Minaj inadaiwa ameachana na mpenzi wake safaree samuel baada ya kutokea ugomvi mkumbwa kati yao hadi kupekelekea gari ya mchumba wake huyo aina ya mercedez benz kuvunjika kioo.
Habari zinasema kuwa kwenye ugomvi huo Minaj alichukua fimbo na kuvunja kioo cha gari ya mpenzi wake ambayo aliinunua yeye mwenyewe nicki minaj wakati wa mapenzi motomoto.
Kana kwamba haitoshi Nick alichukua nguo za mpenzi wake na kuzitupa kwenye takataka,tukio hilo lilikuwa kama filamu.
Inasemekana kwamba polisi wakafika eneo la tukio lakini hakukuwa na mtu aliyekamatwa na sababu kuu ni kwamba msanii huyo ndiye mmiliki wa ndinga hiyo, alimuachia tu atumie wakati walipokuwa pamoja.
Mpenzi wake huyo alisindikizwa na polisi nje na kuondoka zake,na kwa sasa anaonekana kwamba amebadilisha zile tattoo kubwa za nicki minaj alizojichora.

0 comments:

Post a Comment