
MRISHO NGASSA AWA MMFUNGAJI BORA AFRIKA LAKINI MKONO MTUPU
Mshambuli
aji wa Dar Young Africans,Mrisho
khalfan Ngassa amepata zali Afrika,Baada ya kumaliza kinara wa mabao
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,Licha ya klabu yake kuaga
mashindano Alfajiri kabisa,Ngasa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao
6 na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya
Demokrasia ya Congo,Haythem Jouini wa Esperance de Tunisi ya Tunisia na
El Hedi Belameiri wa Es Setif ya Algeria.Ni baada ligi ya Mabingwa
Afrika kufika tamati wikiendi iliyopita na Es Setif kutangazwa mabingwa
wapya wakibebwa na bao lao ugenini kutokana na matokeo ya sare ya 1-1
mchezo wa Algeria na sare ya 2-2 mchezo uliochezwa kinshasa.Ngassa
aliyafunga mabao hayo katika raundi ya kwanza walipocheza na Komorozine
ya Comoro mchezo wa kwanza walishinda 7-0 na marudiano walitoka kifua
mbele kwa ushindi wa mabao 5-2.Yanga ilitolewa na Al Hahly ya Misri kwa
penalt 4-3,Lakini Ngassa hawezi kupewa zawadi kwa vile wamefungana
kiutaratibu hata mchezaji akishinda tuzo hiyo CAF huitoa kwa klabu yake .

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment