fikra potofu!!!

Author

ULAJI wa supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume, kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita, kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanamume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Dk Cuthbert Maendaenda wakati akitoa mada yake katika semina ya wahariri, iliyofanyika mkoani Morogoro iliyojadili nafasi ya wanaume katika kuleta mabadiliko katika jamii juu ya afya ya uzazi na ujinsia.

Dk Maendaenda ambaye alikuwa akijibu maswali pia kuhusu dhana hiyo iliyozoeleka kuhusu nguvu ya supu ya pweza, alisema ipo haja ya wanaume kuangalia sababu za kudorora kwa uwezo wao na kufanya marekebisho, badala ya kudhani kwamba kuna dawa kutoka katika vyakula hivyo.

Katika miji mingi nchini kwa sasa, nyakati za jioni supu ya pweza na karanga mbichi huuzwa, ambapo wauzaji wamekuwa wakinadi kama msaada wa kurejesha heshima katika ndoa.

Alisema ufanyaji mapenzi unaathirika na vitu vingi na jamii lazima kuangalia ukweli huo ili kuwa na watu wanaojiamini katika mapenzi na wale ambao wana matatizo kupata ushauri wa daktari.

Mwezeshaji huyo kutoka Taasisi ya Sweden inayohusu haki za afya ya uzazi na ujinsia (RFSU) Tawi la Tanzania, ambayo inaendesha mradi wa TMEP wenye lengo la kuwaamsha wanaume kuwa chachu ya mabadiliko na hivyo kuwa na uelewa mpana kuhusu haki za ujinsia, alisema mwanamume mwenye afya, hutoa kiasi cha manii cha CC 3-5 kinachotarajiwa kuwa na mbegu milioni 300-500 katika mshindo mmoja.

0 comments:

Post a Comment