China imeongeza msaada wake katika
shughuli za kupambana na Ebola Afrika Magharibi kwa kutuma wafanyakazi
wa utabibu 160 huko Liberia.
Wafanyakazi wa utabibu ambao wengi
wao ni wanajeshi, watawekwa katika kituo cha ukaguzi na matibabu
kilichojengwa na China yenyewe katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.Ubalozi wa China ulieleza kuwa wafanyakazi hao waliowasili hivi karibuni walipata uzoefu wa kutibu homa ya SARS ilipozuka Asia zaidi ya miaka 10 iliyopita.
China imekuwa ikilaumiwa kuhusu janga la Ebola - kwamba haikutoa msaada wa kutosha na msaada wenyewe unachelewa.






0 comments:
Post a Comment