Jeshi La Chukua Nchi

Author
Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso jeneral Honore Traore sasa amejitangaza kuwa rais baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kutangaza kujiuzulu. Jenerali Traore ameitikia mwito wa waandamanji ambao walikuwa wanamtaka kuchukua usukani baada ya kuondoka kwa bw Compaore. Bwana Compaore amesema kuwa amekubali kujiondoa mamlakani ilikutii matakwa ya waandamanji ambao hawamtaki kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kutawala kwa miaka 27. Bwana Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90. Awali msemaji wa jeshi alikuwa amewaambia waandamanji kuwa bwanaCompaore hayuko tena uongozini huko Ouagadougou. Hata hivyo hakubaini ikiwa afisa huyo wa kijeshi alikuwa akizungumza kwa niaba ya jeshi lote. Jeshi lilisema kuwa litafanya mkutano na waandishi habari. Siku ya alhamisi waandamanaji waliokuwa wamekasirishwa na jitihada za rais za kuongeza muda wa uongozi wake wa miaka 27 walitetekeza bunge na kuvamia kituo cha runinga ya taifa. Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa angebaki madarakani kwa mwaka moja zaidi .

0 comments:

Post a Comment