NIFANYE NA MIMI KAKA DICK -07

Author


 CHOMBEZO:NIFANYE NA MIMI KAKA DICK-07

Mtunzi:Juma Hiza

0712988278


Alianza kwa kunipigia simu, sikuwa na haraka ya kutaka kuzungumza naye kwa wakati ule, nilichoamua kukifanya ni kukata simu. Si kana kwamba nilikuwa nikiogopa kuzungumza naye lah! Ila nilikuwa najaribu kumtengezea hofu katika moyo wake. Niliamini kwa kitendo kile nilichokuwa nakifanya ni lazima angeweza kuwa katika wakati wa maswali yaliyokosa majibu.

Muda wote huo nilikuwa nikitabasamu tu! kichwani mwangu nilikuwa nikijaribu kutafakari ni kwa namna gani ningeweza kummaliza.

Haikuchukua muda mara ukaingia ujumbe mfupi kwenye simu yangu, sikuutetereka sana, niliamini kwa asilimia zote kuwa ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa mume wa Precious hivyo sikuwa na hofu hata kidogo. Nilipoichukua simu yangu na kuitazama kweli nilikutana na ujumbe wake. Alianza kwa kuniuliza swali ambalo naweza kuliita lilikuwa ni swali la kizushi na ni hapa ambapo tukaanza kuchat kama ilivyokuwa kawaida yangu. Nilikuwa hodari wa kucheza na maneno ambayo kiukweli kama ungetaka ligi na mimi hakika kila siku ungekuwa ni mtu wa kuambulia patupu, nilikuwa hodari nisiye na kifani.

“Unaitwa nani?” aliniuliza katika ujumbe mfupi aliyokuwa amenitumia kupitia simu ya mke wake ambaye mimi nilikuwa namfahamu kwa jina la Precious.

“Mbona unanirudisha nyuma tena?”

“ Kivipi na mbona hunitajii jina lako?”

“Nirudie kukutajia mara ngapi?”

“Nimekuambia naitwa mwizi.”

“Mwizi gani embu nitajie jina lako.”

“Sina jina.”

“Huna jina?”

“Ndiyo.” Nilimjibu kisha ukimya ukatawala kwa muda wa dakika kadhaa. Nilifahamu fika ukimya ule haukuwa wa bure, kwa akili yangu ya harakaharaka nilifahamu kuwa alikuwa akijaribu kulitafuta jina langu kupitia huduma za kifedha. Hilo niliweza kulibaini na ni kama nilivyokuwa nikifikiria mara akanitumia ujumbe ambao alikuwa ameandika jina alilokuwa amekutana nalo, lilikuwa ni jina la marehemu babu yangu ambaye alikuwa akiitwa Akili Maganga.

“Akili Maganga.” Alinitumia kisha sikutaka kumjibu lolote, niliamua kufanya hivyo kwa makusudi kabisa ili aweze kunipigia simu.

Naam! Haikuchukua dakika mara akanipigia simu.

“Hallo mbona unanisumbua sana hivi hujui kwamba nipo kazini?” nilimuuliza mara baada ya kupokea simu.

“Samahani sana ila nilikuwa na ombi.”

“Ombi gani?”

“Ni kuhusu hiyo pochi ya mke wangu.”

“Imefanyaje?”

“Nilikuwa naomba uni….uni..unisaidie kunirudishia.”

“Ulinipa?”

“Hapana.”

“Sasa nitakupaje wewe wakati hujanipa.”

“Samahani lakini.”

“Hakuna cha samahani hapa.”

“Basi niambie nikupe nini au nikupe pesa kiasi gani ili uturudishie.”

“Mwambie mkeo aifuate na zikipita siku tatu kama hajanitafuta basi hamtakuwa na chenu hapa.” Nilimjibu kisha nikakata simu.

Ndugu yangu katika maisha yangu nimewahi kukutana na wanaume wengi sana, wengi wenye misimamo yao thabiti na wengine waliyozubaa. Ama kwa hakika mume wa Precious alikuwa amezubaa kwelikweli.

Nilizidi kupata ujasiri wa kumteka akili yake pale alipokubali kuwa mimi nilikuwa ni mwizi. Kupitia imani yake hiyo niliweza kumingia vizuri kiasi kwamba kila kitu ambacho nilikuwa nikimwambia alikuwa akikifanya.

Kwa muda wote huo Precious alikuwa bado hajanifahamu kama mimi ndiye ambaye nilikuwa nikimtetemesha mume wake. Alikuja kunifahamu pale ambapo aliamua kunipigia simu, usiku uleule majira ambayo mume wake alikuwa amelala, muda huo ndiyo kwanza nilikuwa nikiendelea kuliandika chombezo langu.

“Hallo,” alisema hapa ni baada ya kupokea simu yake.

“Yes.” ( Ndiyo.)

“Dick.”

“Naam!”

“Ni wewe?”

“Ndiyo hujakosea.”

“Siamini.”

“Huamini nini?”

“Umeiokoa ndoa yangu.”

“Nimeiokoa kwani ilitekwa?”

“Hapana ila umetumia akili sana kunisaidia unastahili pongezi.”

“Usijali mrembo.”

“Nikuulize kitu.”

“Niulize.”

“Ulijuaje kuwa nimemwambia nimeibiwa pochi yangu.”

“Nilijua tu.”

“Ulijuaje?”

“Mimi ni mwandishi naweza kufahamu nini kitatokea kabla hata tukio halijafanyika.”

“Hongera.”

“Hongera ya nini?”

“Kwa kipaji.”

“Hahahaha haya.”

“Ok ila we genious.”

“Kesho njoo uipitie pochi yako uliisahau kwa haraka zako.”

“Hahaha! Haya bhana ila nilikuwa nimechelewa ndiyo maana hata hivyo sikuogopa kwani ilikuwa sehemu salama.”

Precious alizidi kuniamini sana, kila nilichokuwa nakizungumza alikuwa akiniamini. Hakutaka kuamini kama niliwahi kukosea katika maisha yangu, kila wakati nilipokuwa nazungumza naye alikuwa akitabasamu jambo ambalo aliweza kukiri kuwa mume wake hakuwa mtu wa kumfanya awe hivyo. Nilianza kumchombeza kwa maneno yangu.

“Halafu nimesahau kukwambia.”

“Kuniambia nini?”

“Kuhusu uzuri wako.”

“Umefanyaje?”

“Wewe ni mzuri sana, yani huna mfano.”

“Mmh! Kwa kukuza sasa.”

“Kweli ujue wewe ni msichana mrembo sana,” nilimwambia kwa maneno ya kumsifia yaliyomfanya atokwe na sauti ya kicheko.

“Halafu siamini?”

“Huamini nini?”

“Kama nimeweza kulala na wewe?”

“Sasa huamini nini?”

“Yani nimejikuta nakuwa mrahisi kulala na wewe sijui umenipa nini.”

“Kwani sistahili kulala na mwanamke?”

“Hapana simaanishi hivyo.”

“Ila.”

“Mimi ni mke wa mtu.”

“Kwahiyo ukiwa mke wa mtu.”

“Hivi mume wangu akijua unafikiri itakuwaje?”

“Itakuwa fresh tu.”

“Halafu unafanya utani.”

“Mumeo hawezi kujua labda umwambie wewe.”

“Sasa nitaanzaje kumwambia?”

“Ndiyo ujue sasa kuwa hawezi kujua kwanza wewe ni mtu mzima sio kila kitu ukikifanya kiwe matangazo hivi huwezi kuwa kama Wazungu?”

“Wazungu?”

“Ndiyo Wazungu wao siri wanaifanya kuwa kama roho hawawezi kuitoa bila sababu ya msingi.”

“Kwahiyo unasemaje?”

“Hawezi kujua.”

“Sawa,” alinijibu Precious kwa kisauti ambacho haraka niliwahi kukifananisha na sauti ya mtoto mdogo. Sikutaka kukaa kimya nilizidi kumchombeza.

“Sauti yako.”

“Imefanyaje?”

“Nzuri kama ya mtoto mdogo.”

“Hahaha umeshaanza mambo yako.”

“Sauti yako nzuri.”

“Ahsante.”

“Kesho utakuja?”

“Ndiyo nikitoka kazini nitapitia hapo.”

“Ndiyo uje uchukue mzigo wako.”

“Hahahaha! Sawa ila sitakaa sana.”

“Usijali mrembo.”

“Haya usiku mwema mkaka.”

“Usiku mwema pia mdada,” nilimjibu na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu kwenye simu.

Sikumbuki ni nini niliwahi kumpa kikubwa katika maisha yake lakini alionekana kunijali sana, kila ilipokuwa inaitwa leo hakuacha kunijulia hali, alikuwa akinionyesha mapenzi ya dhati ambayo yalinifanya muda mwingine niringe kwani alioneka kunipenda sana.

Siku iliyofuata alipanga kuja kwangu kwa lengo la kuchukua pochi yake. Sikutaka kuwa nyuma katika kupanga mipango yangu, nilipanga siku hiyo kumchezesha sebene ambalo hakuwahi kuchezeshwa hata siku moja katika maisha yake na ni katika sebene hilo nililopanga kumchezesha alitokea kumchukia mume wake kwani hakuwa akimridhisha hata kidogo.


Je, nini kitaendelea?

Tukutane Kesho mahali hapa hapa.


#Share kwa wingi.

0 comments:

Post a Comment