HATUKUPENDA TUWE HIVI-30

Author

Mirim alipekua katika pochi yakeakatoa kitambulisho cha Genes chenye picha yake ndogo (passport) na kuibusu,"haaakilekitambulisho unacho tu" Anitha aliuliza kwa mshangao kwani aliamini kitakua kishapotea,"sasa nitapotezaje,,," Miriam alijibu kwa tabasamu zito.Waliongea mengi hadi usingizi ukawachukua.Asubuhi waliamka na kujiandaa tayari kwenda kazini.***Penzi la Angel na Genes lilizidi kukua,"hivi mpenzi una mpango gani na mimi" Angel alimuuliza Genes,"mpango gani kivipi mamii?" Genes alijibu huku akijidai hajaelewa swali kwani wanaume wengi huwa hawapendi kuulizwa juu ya mpango wa baadae,"liniutajenga kwako unioe"Angel alimuuliza Genes ambaye kwa wakati huo aliinamisha kichwa kwenye dawati,"usijali mke wangu nitajenga tu na nitakuoa cha muhimu tusome kwa bidii ili tuje kushirikiana kujenga" Genes alijibu huku kichwani akiwaza jinsi akili ya wasichana ilivyo ndogo kwani maranyingi mwanamke huwaza kumsubiri mwanaume ajenge ili aolewe naye wakati huo huo mwanaume anamsubiri aoe mwanamke ili wajenge wote.Angel alifurahi kusikia hivyo.Siku zilizidi kusonga huku Angel akijikuta akizidisha upendo kwa Genes kwani waliokua wanamshurutisha kuua wao walishakufa,"huyu atakua mume wangu"Angel alijisema kimoyomoyo.***Miriam alishaanza kufuga na tayari ashaanza kukuza mtaji aliopewa na wafanyakazi wenzake na sifa zake zilizidi kuenea mtaani,watu wote walimpenda," jamani kwa niniasiwe dada yangu"watoto waliomjua walimpigania kwani alipenda sana watoto pia alikua na rohoya utoaji sana."sasa Miriam natakaufungue biashara yako uiendeshe mwenyewe" muajiri wake alimshauriMiriam licha ya Miriam kusikia ushauri ule badoaliaahidi kuendelea na kazi pale lakinikwenye biashara zake ataajiri watu,"lakini yakupasa uende shule kwanza ujifunzekusoma.Miriam baada ya kuulizia mahali ambapo angeweza kupata elimu ya watu wazima ili aweze kujua kusoma na kuandika ambayo ilijulikana kama kufukuza ujinga,"hapoArusha Secondaryinaanza kesho kutwa jumatatu nenda hapo tena ni bure kabisa" alipewa taarifa na mfanyakazi mmoja.Bila kupoteza mda Miriam alianza masomo,japo ilikua vigumualijitahidi na kwakua aliendakwa moyo,"hapa nisipompata Genes basi sitompata tena"Miriam alijisemea baada ya kumuona Genes amesimama mwenyewe katika lango la shule,"mambo" Miriam alianzisha maongezi,"powavipi" Genes alijibu huku akiwa kainamisha kichwa chini akijifanya kama hamjui,"mbona uko hapa mwenyewe na wenzio washaishianyumbani?" Miriam aliuliza,"ninamatatizo kidogo nilikua natafuta pesa yangu nimepoteza yaani sijui hata nifanyeje hapa" Genes alijibu huku machozi yakimtoka,
"shilingi ngapi"Miriam alimuuliza kwa huruma,"elfu hamsini (50,000)" Genes alijibu,"basichukua hii" Miriam aliongea huku akiingiza mkono katika sidiria yake na kutoa notikadhaa za elfu kumi na kumpa Genes bila hata kuhesabu.Genes alipokea na kuzificha mfukoni."vipi naomba namba yako ya simubasileo nataka niongee nawewe kidogo"Miriam aliongea kwa sauti y chini.Genes alimpa Miriam namba ya simukisha wakaachana."Huyu msichana itakua ananipenda ila sasa nishampenda Angel"Genes aliwaza jinsi Miriam anavyojitoa kwa ajili yake na bila kutarajia akajikuta akisahau mambo yaliyowahi kutokea kipindi cha nyuma,"akinitafuta kwenye simu namkubalia sasa, na nitamuacha Angel" Genes aliwaza.Tayari Genes alishaanza kumuwaza Miriam, ashasahau kila kitukibaya ambacho kilitokea kwa kasababishwana Miriam.***

0 comments:

Post a Comment