Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini -52
SOON NAACHIA NEW STORY LIKE PAGE ToWENDE SAWAAA
ILIPOISHIA:
Taarifa ile haikuwa ngeni kwa Mustafa alijua mtoto kishachukuliwa na owe yake. Alirudi nyumbani haraka ili kumtuliza mkewe ambaye muda ule alikuwa amepagawa. Alipofika
alimkuta amechanganyikiwa akilia ovyo mikono kichwani. Husna alipomuona mumewe alimkimbilia na kumkumbatia na kuendeleza kilio.
“Mume wangu mwanangu ameibiwa!”
SASA ENDELEA...
Alijitahidi kumbembeleza na kumueleza watamtafuta, walipeleka taarifa polisi na kwenye vyombo vya habari lakini ajabu walipotafuta picha za mtoto hawakuziona. Taarifa ilitawanyika kila kona ambayo siri yake alikuwa akiijua Mustafa. Familia ya mume nayo iliungana na Husna katika tukio lile.
Japokuwa mtoto alikuwa amepotea lakini hali ya amani ilikuwepo kwenye ndoa na wazazi kuamini mkwe wao siyo mgumba. Walimpa moyo kuwa awe makini na watu wasiojulikana kutokana na tabia za watu kuiba watoto wachanga. Mustafa alitengeneza uongo kwa kumueleza kuwa Shehna amesema asilie kwa vile mtoto wao atarudi na kumfanya aishi kwa matumaini.
Kupotea kwa mtoto kulifanya wazazi wa Mustafa waendelee kumpa moyo Husna kwa kuhofia kumuumiza kwa kumkumbusha maumivu ya kuibiwa mtoto wake. Baada ya miezi saba kukatika, usiku mmoja Mustafa aliota akizungumza na Shehna akimueleza kuwa ni muda muafaka mkewe kushika ujauzito wa kweli.
Shehna aliendelea kumueleza mtoto yule atakuwa chini ya ulinzi wa majini mpaka atakapokuwa ndipo atarudishwa chini ya wazazi wake. Lakini wakati huo ndugu zake watakuwa wamekua, wataendelea kumlinda siku zote za uhai wake.
Baada ya wiki moja akiwa kazini mkewe alimpigia simu kumweleza mumewe hali aliyohisi, Mustafa alijua dalili zile zilikuwa majibu ya ndoto aliyoota, walipokwenda hospitali vipimo vilionesha ujauzito wa mwezi mmoja. Ujauzito ule ulikuja kawaida wa miezi tisa tofauti na mimba ya ajabu iliyotangulia ya miezi miwili tu mtoto kuzaliwa.
Ujauzito ulikwenda vizuri ulipotimiza miezi tisa alijifungua salama mtoto wa kiume, Husna baada ya kujifungua alimlinda sana mwanaye ili asirudie kosa la awali. Mtoto alikuwa katika malezi mazuri, Mustafa na Sara waliendelea na kazi zao huku Sara akiwa na somo kubwa maishani mwake kuwa mwanadamu anaweza kuwa mbaya kuliko jini pia kutofuatilia lisilokuhusu. Hakuamini kama majini wana roho nzuri siku zote aliamini ni viumbe wabaya kumbe wapo wazuri na wabaya kama wanadamu.
Mustafa alisubiri miaka mitatu ili aende kwa Shehna kwa njia ya ndoto kuwaona watoto wake japo wa kiume alimuona.
Mtoto wao naye alikuwa vizuri bila kujua akiwa mkubwa atakuwa na tabia gani?
#Mwisho.
#ASANTEN SANA WATU WANGU WA NGUVU KWA KAMPANI NA SAPORT MLIONIPA MWANZO MPAKA MWISHO WA HADITHI HII ILA KUNA HADITHI NYINGNE ZINAKUJA ZENYE MVUTO.
0 comments:
Post a Comment