MAMA TERESA

Author
Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amemtangaza rasmi Mama Teresa kuwa Mtakatifu. Papa Francis alitangaza mapema mwaka huu kuwa Septemba 4 itakuwa siku ambapo sherehe ya kutakatizwa kwa Mama Teresa itafanywa, ambayo itakuwa ni siku moja kabla kuadhimisha miaka 19 tangu kufariki kwake.

Mama Teresa alipewa tuzo ya Nobel kutokana na kazi zake zilizolenga masikini, wagonjwa, wazee na wapweke katika mitaa ya mabanda ya Kolkata, ambako zamani kulitambulika kama Calcutta. Pia amekuwa na mchango mkubwa kwa Kanisa haswa baada ya kufanya idadi kubwa ya wakazi wa India kwenda kuhij katika kanisa la Mtakatifu Peter huko Roma.

Jina halisi la Mama Teresa lilikuwa Agnes Gonxha Bojaxhiu, mwenye asili ya Albania aliyezaliwa 1910 katika eneo ambapo sasa linatambuliwa kama Skopje, Macedonia.

Alifika India mnamo 1929 baada ya kuishi na kundi la wamishenari kwa muda nchini Ireland.
Alianzisha kundi la Wamishenari wa Misaada mnamo 1950 na akapewa uraia wa India mwaka uliofuata.

Mnamo 2015, alisifiwa na wataalamu wa Vatican kwa kusababisha uponyaji wa mwanamume wa Brazil katika mwaka wa 2008 ambaye alikuwa na uvimbe kwenye ubongo wake.
Hiyo ilimfanya Teresa kufikisha kiwango kinachohitajika kwa mtu kutangazwa kuwa mtakatifu.
Papa John Paul wa Pili alimtangaza kuwa mbarikiwa mnamo 2003.
Francis aliwahi kukutana na Teresa 1994.

0 comments:

Post a Comment