KABLA YA NDOA MWANAUME JIFUNZE HAYA

Author
KWA WANANDOA NA WALE WANAOTARAJIA KUINGIA KTK NDOA.

Mbebe mke wako pale anaposinzia akiwa sebuleni na mpeleke kulala, muda mwingine mfanye ajisikie kama mtoto mdogo.

Ukweli ni kwamba kila mwanamke anapenda kudekezwa kama mtoto wa miaka miwili. Ndio maana muda mwingine wanawake hufanya mambo ya kitoto.

Inawezekana ukawa na mabishano na mkeo na ukaona anafungusha mabegi yake na anataka kuondoka.

Hiyo haimaanishi anataka kukuacha, ni utoto tu, anachotaka ni wewe umshike mkono, umvutie kwako, umtizame usoni kwake na umwambie 'Samahani kwa mabishano na kukukashifu, haitajirudia tena"

Huyo ndiye mwanamke wako, ubavu wako, Eva wako. Kila Brother anahitaji kusoma chuo cha wanawake kabla hajaoa, soma vitabu kuhusu wao, soma vitabu vya dini vinasemaje juu ya kuishi nao na kamwe hautakuwa na tatizo la kuishi nae.

Ingawa kunaweza kuwa na changamoto za hapa na pale, hiyo ni kwa sababu wote mmetoka katika familia tofauti, zenye malezi ya tofauti na historia tofauti.

Hivyo basi soma vitabu kuhusu ndoa, pitia mafundisho mbalimbali ya walimu wa mahusiano kama Dr. Chris Mauki, Dr.Gulam Mhedu tizama mafunzo ya Dr. Myles Munroe katika Youtube, Ongeza maarifa kuhusu malezi ya watoto na umuhimu wa Ndoa na mengineyo.

Usikimbilie tu ndoa kisa Washikaji zako wote wameshaoa au umechoka kula msosi wa hotelini, na huku kichwani bado kweupe kuhusiana na ndoa, utajiletea matatizo.

Ni wanaume wangapi wanaeza vumilia wake zao wanaoongea sana na kushout kwa kila jambo? Kama vile ilivyo shida kwa mwenye miguu ya mzee kupanda mlima uliojaa
mchanga, ndivyo ilivyo kwa mume mpole kuishi na mke mwenye makelele.

Unaambiwa uwe mkimya pale mmoja wenu anapokuwa na hasira na kuongea sana, Mmoja wenu anapokuwa moto basi mwingine awe maji. Hapo mambo yataenda sawia.

Kaka zangu, ukiwa kama mwanaume jifunze kupotezea baadhi ya vitu, sio kila jambo unakua mkali kama pilipili mpaka watoto wanaenda kujificha chini ya uvungu wa vitanda.

Cheza michezo ya kitoto na mkeo, imba nae siku za weekend huku ukimsaidia kufua au kutengeneza bustani, kuwa serious sana kunamuogopesha mkeo na hawezi kuwa rafiki yako wa karibu.

Msaidie kazi za nyumbani, yeye si mfanyakazi wako wa ndani bali ni msaidizi, ulikuwa bachelor na kazi zote ulifanya mwenyewe sasa amekuja mke kukusaidia na sio kubadili kuwa kazi zake, menya viazi, teka maji, Oga nae, muamshe kwa ajili ya sala, mfindishe kupika chakula ambacho hajawahi kupika.

Mpigie simu ukiwa kazini mwambie umemkumbuka na unampenda sana. Andika neno "I Love you" na uweke chini ya mto wake au pochi yake kabla hujaenda kazin.

Mbusu siku zote, mkumbatie, mmbembeleze. Siku zote mueleze kwamba yeye ni mzuri na una bahati ya kuwa mume wake.

Yote haya ni sehemu ya kuwa romantic, pale mke anaposema kwamba hauko romantic, anamaanisha humfanyii haya mambo, hamaanishi romance mkiwa chumbani.

Ni vitu fulani vidogo sana na vya kipuuzi ila kwa mwanamke vina maana kubwa sana, niamini mimi.

Tamati nawashauri kaka zangu, gawanya usiku wako katika sehemu tatu. Moja ni kwa ajili yako (kuwaza mipango yako ya maendeleo na kulala) mbili ni kwa ajili ya mke wako (ongea nae, kama uwezekano upo make love with her) na tatu ni kwa ajili ya Mungu wako (Mshukuru kwa kukulinda siku nzima na kukufanikishia mipango yako)

Nakuahidi huo utakuwa usiku bora kabisa ambao hujawahi kuupata!

Mambo mawili ya kuzingatia na mtakua mmemaliza, wanawake watiini wanaume zenu, na wanaume wapendeni wake zenu. utii ni bora kuliko sadaka!

Busara yangu, "A happy man, marry the woman he loves, but the happiest man keep loving the woman he marry!"

Asante dk. Gullam

0 comments:

Post a Comment