Marafiki Club 37
by Sparner Boy 0765148781
Ilipoishia..
Roy aliposikia sauti ile alishtuka kidogo kisha akamwangalia Ester na haraka akainuka kwenda kufungua mlango ule..
Endelea..
Alipofungua mlango alishtuka kumuona Mariam,alitamani akimbie kwani alifahamu yule ni Husna lakini alisita baada kuona hali yake sio nzuri,alionekana kuchoka sana pia alikuwa na alama za kipigo usoni.Roy alimkaribisha ndani akijaribu kuficha uwoga aliyokuwa nayo.Ester alipomwona Mariam,alifurah sana akainuka na kumbatia akimkaribisha nyumbani.
"karibu wifi yangu nilikuwa na wasi wasi sana kuna siku ulipiga simu nikasikia unalia sana na hizi alama ni za nini wifi"
"siku hiyo mlipokuwa gest nilipiga Roy akakata simu nilikuwa kwenye matatizo sana"
"umejuaje tulikuwa gest wifi?"
"kila kitu anachokifanya Roy mimi nakijua"
"nisamehe wifi nilianzisha uhusiano na Roy bila kukuambia"
Roy alikuwa kimya akiwasikiliza na alitamani Ester atambue yule sio Mariam.Alipiga mahesabu ya haraka haraka akawaza akifanya mchezo Ester atauwawa pale pale.
Haraka alimshika Ester mkono akamvuta na kumwambia
"huyu ni Husna wala siyo Mariam"
"Husna ndio nani jaman Roy unanivuta ghafla na ungeniumiza?"
Roy alimnasa Ester kibao cha uso baada ya kuona haelewi.Ester alimwangalia Roy na hakuamini kama ipo siku Roy atampiga.
Roy unanipiga mimi kisa naongea na wifi yan.."
"ishia hapo hapo huyu ni Husna pumbavu wewe,Mariam alikufa ivi ivi"
"Mariam alikufa? Lini mbona unanichanganya au umeanza kuwa kichaa"
Roy kabla hajajibu swali la Ester,pale kwenye kiti alipokuwa amekaa Mariam Sura yake ilibadilika ikawa sura ya Husna kisha akasema
"ni kweli mimi sio Mariam na sura yangu hii apa"
Alizungumza maneno hayo Husna wakati huo akiwa kwenye ile sura yake halisi.Ester alishtuka sana akajificha nyuma ya Roy akisema
"Mungu wangu kumbe ni jini?"
Husna alitabasamu kidogo akasema,,
"unaweza kuniita jina lolote unalopenda kwa sababu hujui chochote Ester na mimi ndio nilimfunga Roy asikuambie kila alipojaribu kukuambia alikuwa anashindwa"
Husna alianza kueleza kila kitu kuwa yeye alitumwa apa duniani kutafuta roho za watoto pamoja na vizazi vya wanawake,hakutaka kumpa kazi ile Roy lakini siku alipomfumania na Mariam alimpa kazi ile kama adhabu yake.Alieleza kuwa siku alipowafumania ni yeye aliyechoma nyumba moto ambapo nyumba ilipoanza kuungua Roy alikimbia nje na hapo akamuuwa Mariam na kuvaa sura yake hivyo Roy akajua Husna ndio amekufa baada ya kuona mwili wa Mariam ikiwa imeungua vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.Aliendelea kueleza kuwa siku alipolala kuwa mchungaji,vile vitu juu ya bati ni yeye alikuwa anafanya ili kumtisha mama mchungaji akalale kwenye chumba cha Roy kwa kutokana na woga.Pia ile ndoto Roy aliota ni husna ndio alimuotesha makusudi kumtega mama mchungaji.
Husna alipoadithia mpaka hapo alimwangalia Roy na kumwambia..
"Nilikupa kazi ile nikakupa na nguvu kiasi kwamba sio rahis msichana yoyote kukukataa,mwanzoni ulifanya kazi vizuri lakini uliharibu ile siku ulipokunywa pombe ukalewa sana mpaka ukaletwa nyumbani na meneja wa bar.Majini huwa hatupatani na pombe kumbuka nilipowapeleka club siku ile wewe na Mariam,ile inaitwa Marafiki Club na ipo chini ya bahari ndio maana niliwafumba macho msione njia tunayopitia.Kumbuka Roy uliagiza pombe kila mtu akakushangaa na ikatokea ugomvi mkubwa yani sisi na pombe ni maadui wakubwa.
Sasa pombe ilipoigia kwenye damu yako,kila kitu kiliharibika ata mimba za mabinti wote zikakataa kutoka.Ni kosa kubwa ulifanya lakini haikuwa kosa lako bali kosa langu kwa sababu sikukuambia na baba alijua nimefanya kusudi,pia ukumbuke hakupenda mimi kuanzisha uhusiano na wewe binadamu wakati nilikuja duniani kufanya kazi.Kutokana na makosa hayo niliyoyafanya baba alikasirika sana akawa ananiita nyumbani na kunipiga,amenitesa sana siku ile Roy uliponikuta na alama za fimbo mgongoni ni baba na ndugu zangu ndio wamenipiga"
Roy alimwonea huruma akamuuliza kwa nini alijitambulisha kanisani kuwa wao ni ndugu.Husna alicheka kidogo kisha akasema alifanya vile ili iwe rahis yeye kuwa pata mabinti wa pale kanisani.
Ester alilegea aliposikia maneno yale na sasa alielewa kila kitu,wakati anajiuliza afanye nini Husna alisema
"sidhani kama nitaweza kuishi duniani lakini kabla sijaondoka nataka lile kanisa tulifanye club ile marafiki Club ya kuzimu ihamie pale"
"hapana haiwezekani"
alijibu Ester.
Husna alimwangalia Ester na Roy kisha akawaambia
"kanisa gani lile lilikuwa kanisa zamani kama hamuamini angalieni pale ukutani kwa makini.
Roy na Ester waliangalia ukutani walipoelekezwa na Husna na ndani ya sekunde chache ilitokea tv pale ukutani na walianza kuona maajabu yanayoendelea mle kanisani nyakati zile za usiku...
Itaendelea

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment