MARAFIKI CLUB-34

Author
Marafiki Club-34
by Sparner Boy 0765148781
ilipoishia..
endapo wakishtua moyo wa mchungaji mara kadhaa bila mafanikio,maana yake ni kwamba mchungaji atakuwa ameaga dunia..
Endelea..
Wakati daktari anajiandaa kushtua moyo wa mchungaji alishtushwa na kauli ya Nesi
"dokta mgonjwa ameshafariki,apa mashine ya oksijeni imesimama na hakuna hewa inayoingia wala kutoka"
"oh my God, ni kweli ameshafariki tayari,mfunikeni akahifadhiwe wakati tunasubiri ndugu zake,kifo kibaya sana"
alijibu daktari yule kwa huzuni baada ya kugundua kuwa mchungaji hayupo tena duniani.
Taarifa zile zilikuwa mbaya sana kwa waumini,maaskofu na ndugu zake mchungaji.Mama mchungaji hakuamini kuwa mumewe amefariki.Alilia sana akimwomba Mungu amsamehe kwa kile alichofanya kwani mpaka wakati ule hakujua ni kitu gani hasa kilitokea mpaka akatoka nje ya ndoa.
Baada ya msiba na kila kitu kumalizika Roy hakuthubutu tena kwenda kanisani kutokana na yaliyotokea.Aliendelea kuishi na Ester kwenye nyumba ile huku habari za Mariam zikianza kupotea kwenye kichwa chake.Upande wa Ester hakuwa anampenda Roy ata kidogo kutokana na aliyoyafanya lakini alilazimika kuishi nae kwa sababu moja tu,hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda kuishi pia hakuwa na mtu yeyote atakaeweza kumsaidia.Roy alitamani kumwambia Ester ukweli lakini kila akijaribu kueleza hadithi nzima ya maisha yake mpaka kukutana na Husna alishindwa na alihisi ulimi wake unakuwa mzito hivyo hakuwa na namna yoyote zaidi ya kukaa kimya maisha yaendelee.
* * *
Naomy aliumia sana kwa matendo Roy aliyomfanyia.Baada ya kuwaza sana aliamua akatoe ile mimba kama ni kufa afe kukwepa aibu ile.
"lazima nitoe hii takataka kwenye tumbo langu kisha Roy atanikoma labda nife"
Aliwaza hayo Roy na alipoangalia saa yake ilionesha ni saa tano asubuh na akawaza huo mda utamtosha kabisa kufanya alichodhamiria.Kwa upande wa pesa haikuwa tatizo kwake kwani pesa zote za baba yake yeye ndie mmiliki, kadi za benk zote alikuwa nazo na namba za siri zote anazijua pia kama baba yake anahitaji pesa huwa anamtuma Naomy.Tokea mama yake afariki baba yake alimkabidhi kila kitu na kwao alikuwa peke yake.
Baada ya kujiandaa alielekea benk i lakini kilichokuwa kinamsumbua kichwa ni kwamba hakujua aende hosptali ipi nzuri,hakujali gharama alichokuwa anahitaji ni kuona mimba ile aliyoiita 'takataka' inatoka kwenye tumbo lake.
Wakati anaondoka pale bank baada ya kutoa kiasi cha pesa alizoona zitamtosha,alisikia kuna mtu anamwita jina lake na alipogeuka alikutana na sura ambayo anaifahamu
"Naomy ata siamini jamani ni wewe"
"ndio ni mimi, wewe kama nakufahamu"
"acha masihara mimi ni Sheila tulisoma wote nikaacha shule tukiwa form two umenisahau?"
Naomy alimkumbuka wakakumbatiana.Walit­oka eneo lile la bank wakaenda mahali wakapiga story za maisha ambapo Sheila alimuadithia kuwa alipoacha shule aliteseka sana mtaani kiasi kwamba alikosa ujanja na kujiingiza kwenye kazi ya umalaya ambapo aliifanya kwa malengo akapata mtaji na sasa anamiliki maduka mawili ya vipodozi moja lipo pale pale kilimanjaro lingine lipo dar es salaam.
Naomy alimpa rafiki yake pole na hongera kwa pamoja kutokana na aliyoyapitia mpaka kufanikiwa kimaisha.Na yeye alimweleza historia yake mpaka kukutana na Roy.kumpa mimba na kumtelekeza.Alipomaliza Sheila alimwambia
"sasa umeamuaje"
"nataka nitoe hii mimba alafu nimshughulikie Roy"
"haha,lisikupe presha mimba itatoka ni kitu kidogo sana.Na huyo mwanaume umepanga kumfanyaje"
"nitamtafutia majambazi wampige wamvunje vunje lakini wasimuuwe nataka kumwona akiteseka"
"ya niini?,.wanaume uume ndio wanaringiaga cha kufanya fanya uume wake ushindwe kufanya kazi"
Naomy alishangaa na kuuliza inawezekanaje ambapo Sheila alimwambia kuna mtaalamu anamjua atafanya hiyo kazi na hapo atakuwa amemkomoa Roy kwa sababu hataweza kuishi na mwanamke maisha yake yote.Naomy alipenda sana wazo lile waligonga wakaendelea kupiga stori na walipanga kesho yake waende kwa mganga wamkomeshe Roy kwanza ndio suala la kutoa mimba lifuate.
Kama walivyopanga kesho yake Naomy na Sheila walikutana,Naomy alikuwa wa kwanza na baada ya muda mfupi Sheila aliwasili,sasa kikosi kikawa kimekamilika na safari ya kwenda kwa mganga ikaanza...

Itaendelea

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment