PRISCA
SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA
SONGA NAYO
Nilitamani kukimbia baada ya kusikia sauti ile ikisema maneno ya kunitisha lakini nikaamua kujikaza kisabuni na kuendelea kuingia japo woga ulishanitawala kichwani mwangu, niliingia ndani na kukuta kidume cha nguvu kikiwa kimeshikilia mtutu wa bunduki kisawasawa huku kikiwa kimenikazia macho kwa hasira sana
“Geukia ukutani pumbavu wewe” alisema kwa ukali
Mwanaume niligeuka huku nikiwa nimenyoosha mikono juu kwa kusalimu amri, kichani nilikuwa nawaza ni kitu gani nifanye ili nimdhibiti yule jamaa aliyeniweka chini ya ulinzi, akili ilikuwa inanituma akinisogelea nifyatue teke kali sana ili nimdondoshe chini na kummaliza moja kwa moja
“weka mikono yako kichwani” alisema huku akinisogelea pale nilipokuwa ili anisachi kama nimebeba silaha yoyote
Yule jamaa alikuwa hajui kitu gani nilichokipanga kichwani kwangu kwani alikuwa anakuja kwa kujiamini sana, nilivuta pumzi kwa nguvu ili nifyatue teke kali sana ambalo lingemkuta yule jamaa bila shaka angekufa hata bila kuomba maji, lakini kabla sijapiga teke nilishangaa mshindo wa nguvu ukitokea sehemu ile, sikujua nini kimetokea lakini nilipogeuka nikakuta yule jamaa amelala chini huku damu zikiwa zinamtoka mdomoni na nilipoangalia pembeni niliona wale wanawake wa nguvu wakiwa wamesimama kama wanaume wa shoka
“asanteni sana” niliongea huku nikiwakumbatia wakina Prisca
“usijali mpenzi wangu mapambano bado yanaendelea” Prisca alisema huku akinikumbatia kwa furaha
Tuliendelea kuingia kwenye ile nyumba huku tukiwa na tahadhali kubwa sana kwani ile nyumba ilikuwa na walinzi wengi sana, tuliamua kugawana ili kila mtu aende na upande wake kurahisisha kazi ya kupambana na wale jamaa, mimi niliingia kwenye chumba kimoja kilichokuwa wazi, nilianza kuzunguka kwenye kile chumba lakini nilikuwa sioni sehemu ya kutokea
Niliendelea kuzunguka kwenye kile chumba kutafuta mlango lakini sikubahatika kuona mlango, wakati naendelea kutembea nilikanyaga sehemu ambayo ilikuwa na mfuniko,nilipofunua ule mfuniko niliona kuna handaki kubwa sana huku kukiwa na ngazi za kushukia, kabla ya kuingia nilianza kuchungulia ili niangalie kama kuna watu wapo karibu na lile eneo
Baada ya kuona kwamba hakuna mtu yoyote aliyekuwa karibu na eneo lile nilianza kuingia huku nikipepesa macho kuangalia nini kinaendelea pale ndani, nilipomaliza zile ngazi nikaanza kutembea kwenye mlango uliokuwa mbele yangu ili nikaangalie kuna nini kinafanyika, nilipochungulia mule ndani niliona watu wakiwa busy wakiendelea na shughuli za upakiaji unga kwenye vifuko huku wakiwa wamevaa nguo kama za madaktari
“dah kumbe hawa jamaa wanapack madawa ya kulevya humuhumu ndani ya nchi hii?” nilijiuliza mwenyewe huku nikiendelea kuchungulia
Nilitoka pale na kukunja kwenye kolido moja ndefu iliyokuwa upande wa kulia nako niangalie nini kinaendelea kule, nilikuta kuna milango miwili mmoja ukiwa mkono wa kulia mwingine ulikuwa mkono wa kushoto, niliamua kuanza kuchungulia kwenye mlango wa kushoto ili nijue nini kinaendelea, nilipochungulia niliona watu wakiwa wamefungiwa huku wakiwa wamechoka sana kwani walionekana dhaifu sana na sura zao zikiwa zinaonyesha huzuni sana
Kichwani nilikwa najiuliza kwanini wale jamaa wamefungwa pale na mbona wanaonekana kuchoka sana huku sura zao zikionekana kama wazee wakati bado walikuwa ni vijana tena wangesaidia kujenga taifa la Tanzania, kingine kilichokuwa kinanihudhunisha ni kuona hadi wanawake nao walikuwepo mule ndani, akili ilikuwa haifayi kazi kwani sikujua wamewekwa pale kwa dhumuni gani
Nilipopeleka macho yangu kwenye mlango wa kulia nikaona maandishi yameandikwa “OPERATION ROOM” ikiwa na maana chumba cha upasuaji, nikaone bora nichungulie ili nijue nini kinafanyika kwani nilishaanza kupatwa na mashaka na kile chumba, nilipochungulia ili nijue nini kinafanyika mule ndani nusura nizimie kwani nilikuta mtu akiwa anapasuliwa na watu waliokuwa wamevaa makoti ya kidaktari
Wale jamaaa walikuwa wanachukua madawa na kuyatumbukiza kwenye tumbo la yule mtu waliyempasua kisha wakaanza kumshona, wakati naendeea kuchungulia nikaona mtu anakuja kwenye ule mlango kwa taratibu, nilitoka mbio mpaka kwenye ule mlango wa kushoto na kuingia sababu ulikuwa wazi
Kwakuwa kulikuwa na giza kidogo nilipata sehemu ya kujificha ili yule jamaa kama atauja mule ndani asije akaniona,mlango ulifunguliwa na kuingia watu wawili wakiwa na makoti meupe,walikuja na kuanza kuwakagua wale jamaa waliofungwa pale chini, alimchukua jamaa mmoja na kuanza kutoka nae nje ili kumpeleka kwenye kile chumba cha upasuaji
Wale jamaa walipotoka nikawafuata wale jamaa waliobaki ili kwenda kuwahoji maswali mawili matatu nijue nini kimewasibu, nilimfuata wa kwanza yeye alikuwa hata hajielewi kwani alikuwa amechoka sana mpaka alikuwa hawezi kuzungumza kabisa, nikamfuata na mwingine ili nijue nini kimemsibu mpaka kuwa katika eneo lile ambalo lilikuwa ni la hatari sana, yeye alikuwa ni mwanamke na kidogo alikuwa na nguvu za kuongea kidogo japo alikuwa anaongea kwa taratibu sana
“Dada nini kimekufanya mpaka uwe katika eneo hili?” niliuliza
“kwanza wewe ni nani?” nae aliniuliza
“mimi nimekuja kuwaokoa nimetumwa na serikali” nilisema japo nilidanganya kwani nilikuwa nataka nijue ukweli
“kaka mimi nilichukuliwa kama mfanya kazi wa ndani kutoka kijijini kwetu Iringa, boss alituma kijana mmoja kijijini kwetu Iringa kutafuta mfanya kazi wa ndani na kwakuwa mimi nilikuwa na hamu sana ya kuja Dar es Salaam nikamwambia kwamba nipo tayari kuja kufanya kazi mjini, nilipofia huku nikafanya kazi siku tatu nyumbani kwa boss na siku moja akaniomba twende tukaembee wakati tupo kwenye gari nilishangaa nikiwekewa kitambaa puani na kuanza kupoteza fahamu, nilipokuja kushtuka nikjikuta nipo humu ndani nikitumikishwa kama mbebaji wa madawa ya kulevya nikifanywa kama maiti,kwa sasa nina miezi mitatu humu ndani huku nikiwa nimewakuta wenzangu wakiwa wameshamaliza mwaka na zaidi” yule binti alisema
Hapo ndipo nilipoanza kuvuta kumbukumbu za kuwa kuna wadada wa kazi wengi walikuwa wakipotea kwenye mazingira ya kutatanisha bila taarifa zao kujulikana wapi walipokwenda, hawa jamaa walikuwa wanawaraghai wanawake kwa wanaume ili waingie kwenye mitego yao na kuwachukua kwa kutumia madawa ambayo yanawapoteza fahamu na kuja kujikuta wapo kwenye hiyo nyumba.
“msijali nimekuja humu ndani kwaajili yenu” nilisema huku nikijiweka sawa
“asante kaka tunaomba utusaidie tutoke humu ndani kwani tunateseka sana” alisema yule dada
“msijali nitarudi muda siyo mrefu” nilisema huku nikitoka nje
Nilichungulia pale kwenye kolido na kuona watu wakipita kwa kunyata pale kwenye kolido, nilipoangalia vizuri kuangalia ni wakina nani, macho yangu yakakutana na Prisca na Rose, nilitoka na kuwapungia mkono ishara ya kuwaita, walikuja pale na kuwaambia yote niliyokutana nayo mule ndani
“sasa tunafanyaje?” Rose aliuliza
“hapa ni kupambana ili kuwamaliza wote” nilisema
“huko nje tumesafisha kila kitu hakuna ha mlinzi mmoja aliyekuwa hai” Rose alisema
“ina maana mmewaua wote” niliuliza
"ndio tumewamaliza wote na ndio maana tumekuja humu ndani" Rose alinijibu
“basi vimebaki vyumba viwili tu navyo ni chumba cha upasuaji na chumba cha kufungia yale madawa ya kulevya” nilisema
“basi inatakiwa tugawane ili tuwasambaratishe wote kwa pamoja” Prisca alisema
Tuligawana vyumba mimi na Rose tuliingia kwenye chumba cha kupakia madawa ya kulevya sababu kulikuwa na watu wengi kidogo, Prisca aliingia kwenye chumba cha upasuaji sababu hakikuwa na watu wengi sana
“mojaaaa mbiliiii tatuuuuuuuuuuu” nilihesabu na kuingia mpaka ndani
Wala hatukupoteza muda tulianza kugawa kichapo mule ndani japo mimi sikuwa na ufundi mwingi kwenye kupigana nilikuwa natumia silaha yoyote iliyopo mbele yangu, Rose alikuwa anajua sana kuwachangamkia wale jamaa na baada ya dakiaka tano wote walikuwa chini kwani hatukuwapa pumzi ya kutafuta silaha zao kwani lilikuwa shambulio la kushtukiza
Tuliwamaliza wale jamaa wote na kuanza kutoka nje kuangalia kama Prisca ameshamaliza ile misheni yake, tulimkuta amewamaliza wale jamaa na tayari alikuwa ameshatoka nje ya kile chumba, nilipomuangalia vizuri niliona hayupo sawa nilipomsogelea nijue kuna nini, nilikuta anavuja damu kwenye mkono wake wa kushoto karibu na bega, damu zilikuwa zinatoka kwa kasi ya ajabu na kujikuta akidondoka chini kama mzigo
Nilimuokota ili kumpa huduma ya kwanza lakini alikuwa amefumba macho akiwa hajitambui, mwanaume nilichanganyikiwa kwani kumpoteza Prisca ni sawa na kupoteza maisha yangu, nilimwambia Rose aingie kwenye kile chumba walichofungwa watu ili tutoke nao nje na kuondoka, nilimuokota Prisca na kumuweka begani huku nikianza kupandisha kwenye zile ngazi za kutokea nje
Nilifaikiwa kutoka nje na kuanza kuangalia gari la kuweza kuondoka nalo, Rose nae alikuwa ameshatoka na wale watu waliochukuliwa kama mateka, wakati naendelea kuwasha gari nilishangaa kuona magari mengi yakija kwenye eneo lile tulilokuwepo
“Mungu wangu vita nyingine tena?” nilijiuliza
Kabla hata sijafanya chochote magari yalikuwa yameshafika pale tulipokuwa, nilipoyachunguza vizuri yalikuwa magari ya Police
“mpo chini ya ulinzi magaidi wakubwa nyie” askari mmoja alisema huku akitunyooshea bastola
ITAENDELEA……………
Je, nini kitaendelea hapo?
Je, Prisca amekufa?

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment