MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF),
Prof. Ibrahim Lipumba, ametangaza
kung’atuka wazifa wake, kwa kile alichoeleza,
“kuwa kikwazo” katika harakati za kukindoa
madarakani Chama Cha Mapinduzi. Anaandika
Saed Kubenea … (endelea).
Amesema, ndani ya CUF
haaminiki tena katika
mapambano ya sasa ya kutaka
kukiondoa chama tawala
mamlakani, hivyo “nimeamua
kujiweka pembeni” ili kazi
hiyo iweze kufanyika kwa
ufasaha.
Amesema, “Katika hali halisi iliyopo ndani ya
uongozi wa chama chetu, mimi naonekana
kikwazo. Naonekana nakwamisha mapambano
ya ukombozi. Kwamba siwezi kuwa na
mchango wa maana kama mwenyekiti katika
mapambano ya kudai haki sawa kwa wote
katika kipindi hiki.”
Aidha, Prof. Lipumba amesema, ameamua
kujiuzulu kwa kuwa baadhi ya viongozi
wenzake ndani ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA), wamewakaribisha
wanachama na viongozi wa CCM waliokuwa
mstari wa mbele kupinga Rasimu ya Pili ya
Katiba.
Hata hivyo, Prof. Lipumba alikuwa mmoja wa
wenyeviti wanne wanaounda UKAWA,
waliokutana na waandishi wa habari makao
makuu ya CUF, Buguruni, jijini Dar es Salaam
na kutangaza kumkaribisha Edward Lowassa
ndani ya vyama vyao.
Wenyeviti wengine walikuwa James Mbatia,
NCCR- Mageuzi; Emmanuel Makaidi, National
League Democrat (NLD); na Freeman Mbowe,
Chadema.
Prof. Lipumba ndiye aliyetoa tamko la
kumkaribisha Lowassa kujiunga na UKAWA ili
kutimiza adhima yao ya kukiondoa CCM
madarakani.
Tayari Lowassa amejiunga na Chadema na
kutangazwa kuwa mgombea urais wa chama
hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka
huu.
Naye Juma Duni Haji, aliyekuwa makamu
mwenyekiti wa CUF, ametangazwa kuwa
mgombea mwenza, baada ya kutimiza takwa
la kikatiba la kujiuzulu nyazifa zake na
kujiunga na Chadema.
Kabla na baada ya Lowassa kujiunga na
upinzani kumekuwa na vishawishi vingi
vinavyowataka viongozi wakuu wa UKAWA
kumzuia Lowassa kujiunga na umoja huo.
Taarifa zinasema, Lowassa mwenyewe alikuwa
akishawishiwa kupitia watu mbalimbali
waliotumwa na viongozi wa CCM, serikali,
madhehebu ya dini na marafiki zake,
kutokihama chama chake alimojiunga moja
kwa moja alipotoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na kukulia humo.
Hata hivyo, Lowassa alilazimika kusema,
kimoyomoyo, na baadaye wazi na kwa sauti,
akikariri kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere alipoona chama chake kinakwenda
kuzimu, kuwa “CCM siyo baba wala mama!”
Taarifa zimesema kumekuwa na shinikizo
kadhaa kutoka serikalini, CCM na ndani ya
familia yake; zikitaka mwanasiasa huyo
kutohama chama chake
Miongoni mwa waliokuwa wanahaha kumzuia
Lowassa kuondoka CCM, ni pamoja na
swahiba wake wa karibu, Rostam Aziz;
mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni ya
kuchapisha magazeti ya New Habari
Corporation.
Wengine waliotajwa kumpelekea ujumbe
katika sura mbalimbali – ombi, ushawishi,
shinikizo – ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana;
Rais mstaafu Benjamin Mkapa, mgombea
urais wa chama hicho, John Magufuli na
baadhi ya viongozi wa madhehebu ya kidini
na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).
Huku kukiwa na ushawishi Lowassa asitoke
CCM, upande mwingine kulikuwa na ushawishi
kwa Chadema – ukitafuta viongozi wa chama
hicho kukataa kumpokea Lowassa.
Miongoni mwa wanaodaiwa kutumiwa na
baadhi ya viongozi ndani ya CCM na TISS,
kumzuia Lowassa kujiunga na Chadema, ni
pamoja na Josephine Mushumbuzi, mke wa
Dk. Willibrod Slaa.
“Hilo la Josephine linaeleweka,” ameeleza
kiongozi mmoja wa CCM aliyejiapiza kuhamia
Chadema na kuongeza, “Anaona nafasi yake
ya ‘Festiledi’ (mke wa rais) – inahamia
kwingine.”
Lowassa, ambaye alijiunga na Chadema wiki
mbili zilizopita, alikuwa miongoni mwa
wagombea 38 wa urais waliojitosa katika
kinyang’anyiro cha urais kupitia CCM. Jina
lake liliondolewa katika hatua za awali; na
yeye amekuwa akilalamika kuwa ilikuwa
kinyume cha kanuni, taratibu na katiba ya
chama hicho.
Alitajwa kuwa mmoja wa wanasiasa wenye
ufuasi mkubwa ndani ya CCM kutokana na
kubeba kundi kubwa la wafuasi analodaiwa
kuunda kwa juhudi binafsi na kukuza kwa
ushabiki wa viongozi na wanachama.
Kupatikana kwa taarifa kuwa safari ya
Lowassa ya kujivua “kijani” na kujiunga na
chama cha magwanda – Chadema, ilikuwa
ngumu – mithili ya kuvuka mito, kupanda
milima na kushuka mabonde – kumekuja siku
moja baada ya mwanasiasa huyo kutangaza
kuhama chama chake.
“Haikuwa kazi rahisi Lowassa kuhama CCM
na kujiunga na Chadema. Tulilazimika kufanya
kazi kubwa na ya ziada kuzuia shinikizo za
kutaka asiondoke,” ameeleza mmoja wa walio
karibu na Lowassa na Chadema.
Habari zinasema, Rostam alifanya kazi usiku
na mchana kujaribu kumzuia Lowassa
kuondoka CCM; lakini juhudi zake
hazikufanikiwa kwa kuwa, baada ya Lowassa
kuweka msimamo wa kuondoka, aliamua
kuwaficha taarifa muhimu baadhi ya marafiki
zake.

0 comments:
Post a Comment