SIKU mbili baada ya kukihama chama
alichokulia, Chama Cha Mapinduzi (CCM),
mwanasiasa machachari nchini, Edward
Lowassa, hatimaye amechukua fomu ya
kuomba kuteuliwa kugombea urais kupitia
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).
Katika eneo la Ufipa, maelfu ya wananchi
walijipanga kandokando ya barabara kumlaki
kiongozi huyo. Alikabidhiwa fomu ya
kugombea nafasi hiyo na Freeman Mbowe,
mwenyekiti wa taifa wa Chadema.
Mara baada ya kukabidhiwa fomu ya
kugombea urais, Lowassa alisema, “…mmenipa
heshima kubwa. Sina cha kuliwapa zaidi ya
kuwahidi, kwamba nitafanya kazi mliyonituma
kwa uadilifu.”
Alisema, “…jibu la shukrani zangu, ni namna
gani nitawatendea haki. Nakishukuru chama
kwa mapokezi mazuri na wale wote
waliojitolea pesa kwa ajili ya kununua fomu
na kunikabidhi. Naamini kuwa nguvu zenu na
matumaini yenu kwangu kuhusu taifa lenu
yatakamilika.”
Amesema njia pekee ya kuhakikisha taifa hili
linafikia malengo yake katika utawala mpya,
ni kuhakikisha walio na sifa wakajiandikishe ili
kupata uhalali wa kupiga kura kwenye
uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Hata hivyo, Lowassa aliomba viongozi wa
Chadema, wanachama na wananchi wengine,
kushirikiana kwa pamoja ili kupatikane nguvu
ya kuiong’oa CCM madarakani.
Kuhusu kashfa mitandaoni Lowassa amesema,
wanaotumia muda mwingi kumkebehi
kutokana na uamuzi wake wa kuhama CCM,
Lowassa alisema, “…sina muda wa
kuwasikiliza na wala hawataniyumbisha.”
Alisema, “Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alisema, “Wananchi
wanataka mabadiliko. Wakiyakosa ndani ya
CCM, watayatafuta nje ya CCM.
Nimejiridhisha kuwa ndani ya CCM hakuwezi
kupatikana mabadiliko. Miaka 52 ya uhuru,
tumebaki palepale. Ni vema wakaachiwa watu
wengine kuendesha nchi ili kuondoa umasiki
wa Watanzania.”
Lowassa ambaye aliyejiuzulu uwaziri mkuu
mwaka 2008 alikuwa miongoni mwa
wagombea 38 waliorejesha fomu za kugombea
nafasi hiyo CCM, jina lake lilikatwa katika
hatua za awali kutokana na kile kilichoolezwa
“kutotakiwa na mwenyekiti wa CCM.”
Hatua ya Kamati Kuu (CC), kukata jina la
Lowassa kuliibua mjadala mzito ndani na nje
ya CCM huku baadhi ya wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC),
wakitoka tahadhari na kueleza kutoridhwa na
uamuzi huo.
Kabla ya Lowassa kukabidhiwa fomu ya
kugombea nafasi hiyo, Mwanasheria Mkuu wa
Chadema, Tundu Lissu alisema, “tukio la leo
ni la kihistoria;” na matunda ya kazi ya kitafiti
ya zaidi ya miezi mitatu iliyofanywa na chama
hicho.
Alisema, “Tumefanya kazi kubwa na utafiti wa
kina hadi kumpata Lowasa na tulikuwa
hatutaki kumtangaza mapema kwa sababu
tulikuwa hatutaki kukurupuka leo tumemaliza
na ndio maana tumemtangaza kwenu.”
Amesema, utafiti wa kumpendekeza Lowasa
ulishirikisha viongozi wote wakuu, akiwamo
katibu mkuu, mwenyekiti na naibu katibu
mkuu.
“Hatukukurupuka. Tumefanya maamuzi sahihi
na yalifanyika kwa kufuata katiba ya Chadema
ya mwaka 2006 Ibara ya 39,1 (c).
Akiongea kwa kunukuu ibara hiyo, Lissu
alisema, Lowassa ametimiza masharti yote ya
lazima ya kupendekezwa kuwa mgombea urais
wa Chadema na jumuiko la vyama vine
vinavounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA).
“Kwa kuzingatia vigezo hivyo, kamati kuu
imejiridhisha kwa kufanya uchunguzi na
kutembelea mahakama zote nchi na kubaini
kuwa, Lowasa hajawahi kushitakiwa wala
kuwa na kosa lolote mahakamani.Hivyo
wanachama wote wanatakiwa kuheshimu
maaumuzi ya kamati kuu,” ameeleza Lissu.
Akizungumzia umuhimu wa kushinda
uchaguzi, Lowassa alisema, mara baada ya
kuvuka kiuzi cha kuingia katika urais Octoba
25, atakuwa na jukumu la kuteua mawaziri.
Amesema, Tumeya uchaguzi (NEC), imeongeza
majimbo mapya 26 hivyo kuwa na majimbo
265. Hivyo, tunahitajika kushinda viti vya
wabunge 133. Kazi kubwa ni kushinda urais
pamoja na kupata wabunge wengi zaidi
bungeni.
Awali Lissu alikana madai kuwa amejiuzulu
nafasi yake na kusema, “…tuhuma hizo sio za
kweli.”

0 comments:
Post a Comment