MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu
Lissu amesema chama hicho hakikurupuka
kumpendekeza Waziri Mkuu Mstaafu Edward
Lowassa kuchukua fomu ili kuwania urais wa
Tanzania kwa tiketi ya chama hicho.
“Tukio la leo ni la kihistoria. Ni ukamilishaji
wa utaratibu wa ukamilishaji wa utafiti
uliofanyika na chama chetu kwa zaidi ya miezi
mitatu. Tumefanya utafiti tunaendaje katika
uchaguzi mkuu. Tunajipangaje. Tunahitaji
wagombea wa aina gani na wenye nguvu kiasi
gani kwa sababu tunataka 25 oktoba mwaka
huu ndio uwe mwisho wa utawala wa CCM na
mfumo tawala,” amesema Lissu.
Lissu amesema wamefanya utafiti wa kina
hata kupata jina la Lowassa. Kazi kubwa
imefanyika ila hawakutangaza kwa sababu
maalum.
“Katika utafiti wa Kamati Kuu, ulihusisha
viongozi wote wakuu wa chama hiki pamoja
na wajumbe wa Kamati Kuu ya chama na
wajumbe wa sekretariet.
“Naposema viongozi wakuu nina maana
utaratibu uliotumika kumpata Lowassa
ulishirikisha katika hatu zote; mwenyekiti wa
chama taifa, katibu mkuu, mkamo wenyeviti
wote wawili wa chama, manaibu katibu wakuu
wote wawili na wajumbe wote wa kamati kuu
ya chama,” ameongeza Lissu.
Aidha, amesema baada ya kazi hiyo Kamati
Kuu ilikaa siku ya Jumapili iliyopita katika
kikao kilichomalizika saa 6 za usiku. kikao
hicho kilifanya uamuzi kwamba, “Mtu
anayefaa kupeperusha bendela ya Chadema
na kwa maana hiyo bendela ya Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika uchaguzi
mkuu ni Lowassa. Uamuzi huo ulifanywa kwa
kina na ukafikiwa baada ya mjadala mrefu na
mpana.”
Ameongeza kuwa kwa mila na desturi za
Chadema, uamuzi unapofanywa na vyombo
halali vya chama kwa kufuata njia zilizowekwa
na katiba na taratibu za chama, Kila kiongozi
na kila mwanachama anapaswa kuuheshimu
na kuutekeleza.

0 comments:
Post a Comment