1. Argentina haina bahati lakini Messi hana bahati kabisa, baada ya kombe la Dunia kumponyoka, Copa America nayo imemuondoka tena, bado maneno yatabaki kuwa Messi na Mcatalunya zaidi kuliko Mwajentina kwasababu tu ya hilo.
2. Messi ni mchezaji bora lakini Mascherano ni mchezaji muhimu. Maneno ya Maradona nayarejea tena “Argentina ni Mascherano na wachezaji wengine 10. Mshikaji ni mpiganaji nje na ndani ya uwanja. Mescharnon ni Captain kivuli ingawa havai “armband”
3. Dah! Di Maria akiumia basi Argentina wanaumia zaidi, unakumbuka kombe la Dunia kabla hajaumia shughuli yake ilivyozaa matunda lakini kukosekana fainali ikawagharimu, ndicho kilichotokea jana usiku, Di Maria huipa Argentina kitu cha tofauti baada ya Messi.
4. Tata Martino unataka kunambia Higuain ni mahiri kuliko Tevez? Hapana mpira hauchezwi chumbani kujua hilo? hata takwimu za magoli SERIE A zinakushangaa.
5. Nawaza tu kama Argentina wamekosa kunyakua Copa America kipindi hiki ambacho wapinzani wao Brazili wakiwa dhofu bin hali na pia Messi akiwa kwenye ubora wake hasa, lini tena wataweza?
6. Wale Chile waliandaa Copa America ili kuchukua na sio vinginevyo, toka makundi walionyesha nia na uthubuti kwamba wanalitaka kombe, na waamuzi pia hapa na pale walituonyesha kwamba hawa ni wenyeji.
7. Messi alicheza lakini Sanchez alishinda, ile panenka ilikamilisha kachumbari kwenye pilau ama wanja kunakshi uso mzuri wa binti kigoli mshikaji alicheza na akawachezesha Argentina. Asante Wenger kwa zile pauni za kutuletea huyu el maravilla.
8. Jorge Valdivia, jezi namba 10, umri miaka 31. Huyu mshikaji alifanya mpira uonekane kitu kirahisi sana kama vile kuota jua, kinachoshangaza mshikaji timu yake kubwa aliyowahi kuchezea ni Palmeiras. Jamaa alifanya sehemu ya kati kati ya uwanja ionekane kama alilipia kodi kama makazi yake ya kudumu. Kwasasa anachuma hela za mafuta pale Al Wahda Abu Dhabi.
9. Kama unataka kuchukua kombe unawahitaji kina Vidal wa tano na Sanchez sita. ila yule Fernandez yule aliyeingia badala ya Valdivia yule, yule aliyepiga penati ya kwanza mshikaji anaujua sana yule.
10. Walichokuwa nacho Argentina ndicho walichokosa Chile, nawaza tu vipi kama Chile wangekuwa na Tevez ama Aguero ingekuaje? Ivan Zamorano na Marcelo Salas waliondoka na magoli yao kitambo ila Chile hii ina moyo zaidi kuliko ufundi.
11. Hongera Chile ila hongera zaidi mashabiki wa Chile, washkaji walishangilia haswaaa hakika kulikuwa na wachezaji 12 pale estadio nacional de Chile.
@Chikoti Cico

0 comments:
Post a Comment