LUKU KUKOSEKANA KWA SIKU MBILI NCHI NZIMA

Author
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba amesema kesho na keshokutwa hakutakuwa na huduma ya ununuzi wa umeme kupitia Luku nchi nzima.
Hatua hiyo inatokana na kubadilisha mfumo wa uuzaji na usambazaji wa umeme kwa wateja kutoka Luku kwenda mfumo mpya wa 3E.
Alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuhusu taarifa zilizosambaa kuwa huduma hiyo haitakuwapo kwa siku saba na kufafanua kuwa huduma hiyo itakosekana kwa saa 24 tu.
“Mfumo huu wa Luku haukidhi vizuri mahitaji ya wateja kutokana na kushindwa kuhudumia wateja wengi kwa wakati mmoja, lakini mfumo 3E unaweza kuhudumia wateja wengi zaidi,” alisema Mramba.
Amewaomba wateja kuwa wavumilivu katika kipindi hicho cha kufanya marekebisho hayo ya mfumo. Mramba alisema mfumo wa 3E utaongeza ufanisi, ikiwa ni pamoja na wateja wote kupata huduma kwa urahisi na haraka kuliko hapo awali.

0 comments:

Post a Comment