Lowassa na Mkewe |
mstaafu Edward Lowassa na wengineo. Kwa leo mwenyeji kwa siku ya leo ni Mheshimiwa Mbowe. Makaidi anasubiriwa
ambae ataingia muda wowote na Lowassa anakaribishwa.
Lowassa: Hizi microphone za hapa ni sawa na hirizi, ni nyingi sana. Watu wanaoniunga mkono wamekuwa wakinisubiri
muda mrefu, wamesema nifanye maamuzi magumu. Anamshukuru kipekee mkewe Regina na watoto wake, anawashukuru
wanachama wa CCM waliomuunga mkono kumpa udhamini. Anawashukuru viongozi wa dini katika maombi ya kumuunga
mkono, uchaguzi wa CCM ulifanywa kwa upendeleo na chuki iliokithiri dhidi yangu. Viongozi walikuwa tayari kupanda
mbegu ya chuki na mifarakano, yaliyotokua Dodoma yameitia dosara nchi yetu. Nimenyimwa haki ya unapotuhumiwa
unajitetea, natural justice.
CCM niliyoiona Dodoma sio chama kile nilichokuliwa na kilichojengwa katika misingi, nasema sasa basi, Nyerere alisema
CCM sio baba yangu na wala si mama yangu na alisema mkikosa mabadiliko nje ya CCM hivyo basi baada ya kutafakari
kwa kina nimeamua naondoka CCM na kuitikia wito wa UKAWA na kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo
CHADEMA. Na anawashukuru viongozi wa vyama vya upinzani kuona kuwa anaweza kutoa mchango wake.
Natoa wito kwa watanzania wenye nia njema, kujiunga nasi kuleta maendeleo ya taifa, Safari ya matumaini inaendelea
kuwepo kwa kupitia UKAWA, lakini safari hii haiwezi kukamilika bila kujiandikisha hivyo twende kujiandikisha. Nimesikia
tetesi wanakaribia kufunga, naomba tume ya uchaguzi waongeze muda kama walivyoongeza Njombe ili wakazi wote wa
Dar waweze kujiandikisha.
Balie: Lowassa unahama kwenda kulipiza visasi endapo utashindi lakini pia wapo wanasema una ukaribu na matajiri
wengi katika nchi hii, He, Ukishinda hutaamisha rasimali kwa matajiri
Nachukia sana umasikini, natamani watanzania wawe matajiri, wawe kama kina Mengi na mzee wa Azam. Marekani kuna
matajiri wengi, unawataka wawatupe chooni
Umefanya nini mpaka uogope kulipiwa kisasi, waulizeni wamefanya nini mpaka waogope mimi kulipa kisasi. Lakini mimi
ni mkristo, samehe saba mara sabini hivyo kama wana madhambi yao wakamuombe tu Mungu wao.
====
Kadi inaanza kukabidhiwa kwa mama Lowassa, mama Regina Lowassa. Na sasa anakabidhiwa mbunge wa Monduli na
mwenyekiti wa CHADEMA
Times FM: Wakati wa Richmond ulikua na matatizo na hivi vyama, Je usipotimiza walivyotarajia?
Mwambungu (Habari cooperation): Je, Ikiwa watanzania watawapeni ridhaa, tumeshuhudia bunge letu limepisha sheria
mbovu na mikataba, mtabadilisha hilo?
Lowassa: Naona hili panoge tushirikiane sote, namp
Tutumie rasilimali kwa wananchi wote, mikata na mikataba iliopitishwa itatazmwa upya ili wananchi wote tunufaike na
rasilimali hizi
Makaidi: Tutaangalia sababu walizopitishia na tuone ni kwa nia njema au mbaya na ikiwa mbaya tutafumua sheria zote.
Mbowe: Kama tuna hasara moja kubwa tunaipata kama taifa, ni kuwa na bunge linalotoka kutoka chama kimoja, absolute
majority. Kwa namna CCM kimekuwa na wabunge wengi, kimekuwa kinaangalia maslahi ya chama chao kuliko ilivyo kwa
taifa. Bunge la kumi na moja litakuwa na uwiano wa kuridhisha hivyo watu watashindwa kufanya maamuzi kwa maslahi
ya vyama vyao
Mbatia: Rasimu ya pili ya katiba yetu ambayo ndio imetufanya kuwepo UKAWA. Tunawahahakishia watanzania, tutaweka
mfumo wa kikatiba kwamba serikali yoyote itayokuwa madarakani ifate maagizo ya Bunge. Nashukuru sana Lowassa
kujiunga
Lowassa: Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika Richmond aende mahakamani, kama
huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.
Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu
mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani
MANENO KUTOKA VYAMA VINAYOUNDA UKAWA
Makaidi: Salamu zangu fupi tu, kwanza kwa bwana Mbowe nimpongeze kwa kuweza kutuletea kifaa, bwana Lowassa na
nampongeza Lowassa baada ya kuona kiza mbele akaamua kuja kwetu, simfahamu sana mzee Lowassa lakini
namfahamu kupitia kwa mwanangu amefanya kazi na Lowassa. Viongozi wa UKAWA tutakuwa pamoja nae kuhahakisha
CCM mnaondoka, kwa pamoja tutaweza kuiondoa CCM tarehe 25 Oktoba. Nashukuru sana Lowassa kuamua, ukiona njia
ina matatizo, unabadilisha. Kama amekuja kutukwamua, watu wote tutamsikiliza.
Juma Duni(CUF): Kazima niseme nimepigwa na butwaa, Lowassa karibu katika ukawa na tumepata fahari, na kwa lugha
ya kisasa tumepata jembe na Oktoba patachimbika, CCM wamesahau kabisa hata malengo ya kugombea uhuru. Tuna
wajibu pamoja wewe kurudi kaotika misingi ya kupigania uhuru nchi hii, na leo nimefurahi kusikia na wewe umasikini
huupendi. Sote tuliokaa hapa ni watoto wa masikini, Lowassa tunapata fahari kubwa kuwa nawe, CUF tutashirikiana.
Mkapa alisema Zanzibar hakuna mtu mwenye hatimiliki ya nchi hii, hamna kikundi chochote kina hatimiliki wa nchi hii.
Mbatia: Haki zako kama waziri mkuu ukihamia UKAWA haziondoki, UKAWA tutazilinda. Mpaka leo UKAWA tupo pamoja,
watanzania wameshinda, tutahakikisha Tanzania bila CCM itawezekana. KANU iliondoka Kenya 2002 na Kenya bado ipo
na tunaamini mwafaka wa kitaifa ambapo taifa letu hili lina ombwe la uongozi. Tunatoa rai kwa wale wote ambao
wanaona ovu la CCM, wajiunge na UKAWA. Mzee Lowassa historia itakukumbuka kwa ujasiri wako. Wana usalama
wanalipa kwa kodi za watanzania wote na sio za CCM, nawaomba wafatilie mchakato huu kwa uadilifu. Tutatumia
hekima, umoja wa watanzania na tuwahahakikishia amani, hatutamwaga damu lakini wasituchokoze. Naamini hatua hii
tuliofikia, mama Tanzania kwanza, vayama vya siasa baadae.
Mshehereshaji: Sasa ni wakati wa kumsikiliza mwenyeji wetu hapa, mheshimiwa Mbowe.
Mbowe: Leo kwa niaba yangu, viongozi na wanachama wote wa CHADEMA, tumependa kwa dhati kukukaribisha Lowassa
na familia yako. Ujio wako umezua hofu kwani hili ni taifa la hofu. Nimesema hofu kwani imeanzia katika chama chako,
wamekuwa wakinipigia simu kwa muda mrefu kuwa mnampokea huyo, atawaharibia chama na mimi nikawahahakishia
kwa nguvu zote kuwa Lowassa hawezi kuhamia CHADEMA tena nikasema kwa kizungu 'over my dead body'. Nikajiuliza
tangu lini wanaitakia mema CHADEMA, nikajua ni urafiki wa mashaka.
Hofu hii haijaishia kwa CCM bali imeingia hadi CHADEMA, chama hiki ni chetu sote. Chama hiki sio mahakama, simsemi
Lowassa ni mtakatifu, nani mmoja wetu humu ndani ni mtakatifu achukue mawe amrushie mwenzake. Taifa hili haliwezi
zaidi ya miaka 20, kulipa visasi, kumleta Lowassa katika meza hii haikuwa shughuli nyepesi, tumefanya mashauriano
mengi. Eti kwa kuwa tuliwahi kumuita Lowassa mtu mchafu hatuwezi kumkarisha hasa bila ushahidi wa wazi.
Ndo mara ya kwanza mtu aliefikia waziri wa waziri mkuu kuhama CCM, nchi yetu inahitaji mkakati mpya, inahitaji fikra
mpya. Watanzania wanataka umoja wetu na hawataki utengano wetu. Eti tutaacha kumpokea Lowassa kiongozi ambae
anaungwa mkono na wananchi wengi wa nchi hii, anayeungwa mkono na robo tatu ya wabunge wa ccm. Kama kuna
mwanachadema ambae hajatuelewa namuombea kwa Mungu aendelee kumjaza busara. Chama csha siasa ni watu, sasa
nimeletewa watu milioni nitawakataa. Siwezi, mtanifukuza uenyekiti na kwa utaratibu huo sitakubali kuondoka.
Kuna wasiwasi kwa watumishi wa umma, Vyombo vya usalama vilivyopo ndio hivyo hivyo vitaendelea, watumishi wa
umma ndio haohao wataendelea. Wapo wengine wengi, tutawakaribisha muda ukifika.
Tumebadilisha gia angani ili dynamics ziweze kutekelezeka, CHADEMA kinaongozwa na katiba na hii simwambii Lowassa
kwa sababu tayari anayo, nawaambia watanzania wanaotaka kujiunga nasi. Tukiikiua hii tutabamizana. Kwenye chama
hiki hatuji kugawana vyeo, niwashukuru sana.
Mwapokee wageni, naombeni msiwaogope wageni kwa kuogopa kuchukuliwa nafasi zenu. Kuna watu tuliwatukana sana,
nawaomba na nyie mkija huku muwarushie wa upande wa pili. Tuna imani sana nguvu mpya inayokuja itakua nguvu ya
neema. Niwashukuru watanzania wote, tunachopambana nacho sio mtu, tunapambana na mfumo dola. Leo hata
ukamchukua malaika ukamshusha CCM na kumuacha kwa mwezi mmoja, ukimchukua tayari atakuwa Ibilisi. Huu ni
mpango wa Mungu. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipotoa shukrani za dhani kwa mtu mmoja wa kipekee sana.
Namshukuru sana sana mheshimiwa Kikwete, chama chetu kina idara ya uenezi, hakijafanya kazi nzuri kama aliyofanya
Kikwete. Kwa hio mheshimiwa wakati unakatwa Dodoma, wewe unalalamika sisi tunasema yes, mambo haya.
Sio kila linalotokea nia baya, mengine ni mpango wa Mungu. Mungu aliona ili muishi kwa amani na familia yako lazima
mtoke CCM ila lazima ujiandae na mazoezi kidogo maana huku kuna mabomu. Waandishi wa habari tunawashukuruni
sana, tunaamini ule ushirikiano mliokuwa mnampa team Lowassa mtaweza kutupa.
Kufikia hapa tumefikia hitimisho, kutakuwa na wimbo wa taifa kuhitimisha. Na mheshimiwa Mbatia anaongoza wimbo wa
taifa wa mama Tanzania.
0 comments:
Post a Comment