Kufuatia
taarifa kuzagaa mtaani kwamba, Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano
wa Yanga, Jerry Muro amefutiwa kibarua chake kwenye klabu hiyo ya
Jangwani, uongozi wa timu hiyo umeamua kulitolea ufafanuzi jambo hilo
ili kuondoa utata na maswali mengi yanayoulizwa na mashabiki wa mabingwa
hao wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu uliopita.
Katibu
mkuu wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, hakuna ukweli
wowote juu ya jambo hilo na kuongeza kuwa Jerry Muro bado ni Afisa
habari wa Yanga na ni mfanyakazi halali wa klabu hiyo na hakuna kikao
kilichoitishwa kuchukua uamuzi huo.
“Hakuna
ukweli juu ya jambo hilo, Jerry bado ni afisa wa habari na mahusiano na
ni mfanyakazi wa Yanga, na hicho kikao sidhani kama kilifanyika maana
mimi ndiye ninayeitisha vikao na sijaitasha kikao cha hivyo”, amesema.
“Nimeshangaa
hata mimi kwasababu nimeona kwenye ‘groups za WhatsApp’ jana.
Nimeshawahi kuongea wakati mwingine unakuta taarifa zimeandikwa kwenye
blogs, sasa sijui huyu mtu aliyeandika yeye taarifa anazitoa wapi”,
alifafanua.
“Mashabiki
wa Yanga waelewe kwamba, Jerry Muro bado ni mtumishi wa Yanga na bado
ataendelea kuwahabarisha habari za Yanga. Tunajaribu kuangalia na
kuchunguza chanzo cha hiyo habari ni nini”, Tiboroha alimaliza.
Awali,
kulikuwepo na taarifa zilizo zagaa kwenye mitandao ya kijamii (social
networks) kwamba afisa habari wa Yanga Jerry Muro ametimuliwa kunako
klabu hiyo lakini habari hizo hazikwenda ndani zaidi kueleza sababu
zilizopelekea Yanga kumtimua Muro.
0 comments:
Post a Comment