WATAZANIA KAMA NYUMBU

Author
Ukienda katika mbunga nyingi za wanyama hapa Tanzania utawakuta wanyama aiana ya Nyumbu, wanyama hawa wakati mwingine huitwa zero brain, yaani wanyama wasio na akili. Sababu inayowafanya waitwe hivyo ni uwezo wao wa kutunza kumbukumbu na waoga wao japo ni wapole sana. Wanyama hawa utawakuta kwa makundi mengi nafikiri ndiyo wanyama wengi katika mbuga zetu. Pamoja na wingi wao hauwasaidii kujilinda na maadui.

Katika mbuga ya Serengeti utawaona wakivuka mto Mara kuelekea upande wa pili wa mto, akipita nyumbu moja kati kati ya mto akakamatwa na kuliwa na mamba nyumbu waliobaki husahau na kuendelea kupita hapo hapo na kuliwa wenye bahati huvuka, lakini pia Nyumbu wakiona simba anawanyemelea huwa hawana uwezo wa kujihami, hata simba akiondoka nyumbu husahau mara moja kama Simba alitafuna mwenzao.

Watanzania tuna sifa kama za mnyama nyumbu. Kwa nini ninasema ni sawa na nyumbu; sifa alizonazo nyumbu ndiyo hizo tulizonazo Watanzania. Watanzania ni waoga sana katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi ambako nyumbu hupatikana kwa wingi kama walivyo Watanzania katika eneo hili.

Watanzania ni wepesi wa kusahau adui, hupenda kupita njia ile apitayo mnyama nyumbu hata kama kuna hatari. Utawaona Watanzania kwa makundi wakivuka mto mara hata kama baadhi wameliwa na mamba au simba. Simba na mamba huwawinda watanzania na kuwala, hulalamika sana kipindi hicho kuwa simba na mamba wamewashambulia na kuwaua lakini baada ya muda husahau kabisa kama simba na mamba aliwahi kuwadhuru na anaweza kurudia mchezo wa kuwatafuna.

Kwa usahaurifu huu wa Watanzania kwa nini tusiitwe zero brain kama wanyama wetu nyumbu ambao hawaoni hatari iliyo mbele yao? Wakati tukielekea katika uchaguzi wa mwaka huu hatuoni hatari zilizo mbele yetu, tumeshahau tulivyojeruhiwa na baadhi ya wagombea.

Nchi yetu ni masikini japo haistahili kuwa masikini, watu wameweka mapesa nje ya nchi, wamepiga dili kubwa mbalimbali wakituacha hoi bin taabani tukibeba zege la misamaha ya kodi za matajiri.

Kwa kipindi cha miaka 10 kashfa nyingi zilikuwa katika wizara nyeti ya nishati na madini, wizara hii ndiyo imekuwa mto Mara, watanzania tumeliwa ndani ya mto huu ukiacha Simba BoT.

Watanzania sasa utawambia nini kuhusu simba hawa wanaotaka kuwa viongozi wetu, kama waliweza kututafuna wakiwa watoto je sasa wakiwa wakubwa itakuwaje, mfano kuna watoto walibeba pesa kwenye viroba kutoka pale benki ya STANBIC lakini mpaka sasa mifumo ya usalama ya nchi imepata kiharusi kuwakamata au kuwatambua.

Kuna walio nunua mitambo mibovu kwa pesa nyingi , sasa wanatundanganya eti tuvuke mto mamba hawali nyama ya nyumbu tena, wanakula majani tu. Kwa kuwa watanzania ni zero brain tunaelekea kuamini kuwa mamba wameacha kula nyama sasa wanakula majani.

0 comments:

Post a Comment