WENGINE wanasema ni kukua kwa demokrasia ndani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), wapo pia wanaojisifia kwamba hizo ni dalili za kukomaa kwa chama,
lakini kwa wenzangu na mie, hizo ni dalili za uholela, ni ishara ya
kukosa kujitambua.
Wahenga wanasema mtu asiyejua anachokifanya kila kitu kwake ni sawa, mtu asiyekuwa na jibu la kwa nini yupo au anaishi, yeye kila kitu kwake hewala ni sawa tu na mtu asiyejua aendako kwake njia zote ni sawa, atajuaje njia inayompeleka kusikotakiwa wakati huko kunakotakiwa hakujui, hata kama anapotea hawezi kutambua kama anapotea kwa sababu kinyume cha kupotea ni kutambua unakwenda wapi.
Hili ni sawa pia kwa taifa kama taifa, ukiwa na taifa lisilokuwa na dira wala mwelekeo, lisiloweza kujieleza lenyewe ni nini, linatoka wapi na linakwenda wapi, na nini maono ya hatima yake, hili ni taifa la kiholela, linaweza kufanya kila kitu na kufuata nia yoyote ile hata kama inaelekea shimoni. Ndiyo, litawezaje kuepuka njia ya kwenda shimoni wakati njia sahihi haliijui?
Taifa la aina hii hata aina ya viongozi linaowahitaji haliwajui, maadam halijui linataka nini, linaelekea wapi na kwa namna gani, hili linaweza kumfanya yeyote kuwa kiongozi wao. Tofauti ya taifa la aina hii na taifa linalojitambua ni kwamba, hili la pili linakuwa na uhakika kwamba, likitoka hapo lilipo linataka kesho liwe wapi, kwalo inakuwa rahisi kujua ni aina gani ya kiongozi linalotaka aongoze ili wafike wanapotaka wawe kesho.
Wachina kwa mfano, hawafanyi uchaguzi wa kuchagua rais moja kwa moja, kiongozi wa taifa hilo anatambuliwa mapema na kuanza kuandaliwa kushika nyadhifa mbalimbali kwenye chama. Anapokuwa tayari Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti hukaa na kuteua mtua atakayekuja kuwa kiongozi wao.
Inafanyika hivi kwa kuwa Wachina wanaamini kwamba, ili taifa lao lisonge mbele zaidi, aina ya kiongozi anayetakiwa kuisongesha mbele zaidi lazima ajipambanue, watu wamtambue na adhihirishe uwezo huo kuanzia chini. Kazi hii hufanywa na Kamati Kuu ya chama kuandaa viongozi na kuwapitisha katika vikao mbalimbali na hatimaye mtu anakuwa kiongozi.
Hii ndiyo aina ya demokrasia waliyoichagua, ukitaka uwalazimishe waingie kwenye sanduku la kura ya kila raia hawatakuelewa kwa kuwa wanajua hatari zake. Taifa lenye idadi ya watu bilioni 1.3 ukitaka wachague mtu mmoja kuwa rais wao wanaweza kujikuta wanaliangamiza taifa lao kwa kuwa kila mwananchi anaweza kutumia vigezo vya ajabu kabisa, visivyoweza kukidhi mahitaji ya nchi kwa wakati huo.
Hii ndiyo kusema kwamba, kama ulivyo msingi wa taaluma ya habari, kila kitu kinaandikwa na kutangazwa kwa sababu moja tu, kwa ajili ya maslahi ya taifa. Wakati mwingine jamii inadhani au inakiona kitu kama cha maslahi yao kumbe ni kinyume kabisa cha maslahi ya taifa (what interests the pubic, might not necessary be of public interest.)
Kama ambavyo tunashuhudia katika Tanzania, watu wanajua wazi kwamba, kurekebisha hali ilivyo sasa nchini kunahitaji mtu mwenye uadilifu usiotiliwa shaka, ambaye si tu yeye ni mwadilifu lakini anao uwezo wa kuwakemea wenzake katika serikali kwamba, hataki mzaha na mali ya wananchi.
Lakini utashangaa, wananchi hao hao ambao maslahi yao ndiyo yanatakiwa yalindwe na kutetewa kwa nguvu zote na mtu mwadilifu na mwenye uwezo wa kusimamia maadili na hata kuweko miiko ya viongozi kwa watakaomsaidia kuendesha serikali, mtu wa aina hiyo ndiye mwenye mvuto mdogo miongoni mwa wanaotangaza nia kuwania uongozi wa juu wa taifa hili.
Badala yake, wale wenye sifa zilizo kinyume cha maslahi ya taifa ndiyo ambao utasikia wanasifiwa na watu, mishipa ikiwasimama wakiwatetea, ukiwauliza kwa nini hawawezi kukuambia jibu lolote la maana zaidi ya ushabiki tu kama vile wa Yanga na Simba, wakati mwingine huwezi kumshangaa mtu anayetabiri kuwa tunaelekea kuwa taifa la ajabu au la kizuzu hivi, kwa sababu kwa hakika hatujielewi.
Ndiyo maana hata urais wa Tanzania sasa umekuwa rahisi, hata mtu ambaye hawezi kuendesha biashara ya kuuza vocha za simu, leo anataka kuwa Rais wa Tanzania, hata kama hawezi kuwa, kile tu kitendo cha kila mtu kudhani kwamba anaweza kuwa Rais wa Tanzania ni kiashiria kwamba, hii ya kwetu si demokrasia ni demoghasia.
Hata kama ni haki ya kila mtu kugombea nafasi hiyo Kikatiba lakini ni ukweli halisi wa maisha kwamba, si kila Mtanzania anaweza kuwa Rais wa Tanzania, tukijitoa akili na kuupuuza ukweli huu hatutakuwa na tofauti na simulizi ya mama jongoo na mwanawe.
Wakati fulani Mwalimu Julius Nyerere, alipokuwa akisisitiza mafunzo kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema: “Mama jongoo alizaa mtoto, alipojikuta ana miguu mingi akamuuliza mamaye Je, mama, katika miguu yote hii nikitaka kutembea nitangulize mguu gani? Mama jongoo akamjibu; wewe tembea tu miguu itajua yenyewe itakavyojipanga.”
Hapa alimaanisha kuwa, viongozi lazima wawe na tofauti kati ya majibu ya mama jongoo na majibu ya viongozi waliopikwa wakaiva na wenye uwezo wa kuongoza. Ukiwasikiliza baadhi ya wasaka urais ndani ya CCM, ukaangalia nafasi zao, halafu ukazichambua kwa makini hotuba au ahadi zao binafsi wanazoahidi Watanzania, hutapata shida kukosa tofauti kati yao na mama jongoo.

0 comments:
Post a Comment