VILABU NA USAJILI WA WAGENI 10.
Ndani ya wiki hii vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya VODACOM nchini Tanzania vimewasilisha pendekezo kwa shirikish la soka nchini TFF la kutaka ongezeko la idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka watano hadi kufikia 10 kuelekea msimu mpya wa ligi 2015/2016.
Pendekezo ambalo ndilo kiini cha makala haya na kupitia maelezo ya Katibu wa Yanga Jonas Tiboroa wakati akiongelea swala hilo, kuna maswali machache ya kujiuliza kabla ya TFF kufikia kupitisha pendekezo hilo.
Swali la kwanza la kujiuliza ni kwamba, vilabu vingapi vina fedha za kusajili wachezaji wa kigeni? Kila kitu kilichobora na kizuri huja na gharama zake, tukiangalia vilabu ambavyo unaweza kusema vina uwezo wa kusajili wachezaji wa kigeni ni Yanga, Simba na Azam (simaanishi vilabu vingine haviwezi) ila kwa kuangalia kwa muda mrefu hivi ndivyo vilabu ambavyo vimekuwa vikisajili wachezaji wa kigeni kwa pesa nyingi.
Swali la pili la kujiuliza ni kwamba vilabu viko tayari kukabiliana na gharama za usajili wa wachezaji wa kigeni? Hapa ndipo panaponipa mgagaziko, kila mara tumekuwa tukisikia ubabaishaji wa vilabu vya Simba na Yanga ktk kuwalipa wachezaji wa kigeni stahili zao na wakati mwingine mpaka kesi hizo kufika FIFA, tukumbuke hapo idadi ni wachezaji wa tano je wakifika 10 itakuaje?
Swali la tatu ni kwamba ligi yetu inaziingizia vilabu mapato kiasi gani kuweza kuwasajili wachezaji 10 wa kigeni? Sehemu kubwa ya vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya VODACOM vinategemea zaidi mapato ya mlangoni kujiendesha hapo unaongelea mishahara, usafiri, malazi, chakula na madawa, vipi tukiongeza na gharama za usajili wa wachezaji wa kigeni?
Swali la nne ni je tunataka vilabu vya Yanga, Simba na Azam kuwa na “advantage” zaidi ya vilabu vingine kwenye usajili na uboreshaji wa vilabu vyao? Hivi ndivyo vilabu vyenye wadhamini na wafadhili wenye uwezo wa kusajili wachezaji wa kigeni kwa gharama zozote zile, na kama tukiziingalia tu klabu hizi inamaana tunataka kuuua ushindani uliopo kwasasa VPL?
Swali la tano ni kwamba sasa kama tunaweza kusajili wachezaji 10 wa kigeni hivi zile timu B ama za vijana (kama zipo) kwa vilabu vyetu ni za nini? Kwa mawazo ya kawaida tu hebu fikiria kama vilabu vitasajili wachezaji 10 wa kigeni hii inaamanisha wachezaji wanaochipukia watakuwa na nafasi finyu ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza na mwishowe vipaji tulivyonavyo vitabaki kucheza “ndondo” tu.
Makala haya imejaribu tu kujiuliza maswali matano ingawa naamini kuna maswali mengi zaidi ya kujiuliza kabla ya kupitisha pendekezo hili la vilabu. Mwisho hebu tuwaze kuhusu Taifa Stars yetu ambayo mpaka sasa ni tia maji tia maji tu.
NAWASILISHA.
@Chikoti Cico.

0 comments:
Post a Comment