Tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu
haki za binadamu linasema “Watu
wote ni sawa”. Hii inatufahamisha
kuwa sote kama binadamu tuna
thamani sawa. Licha ya dhana hii iliyo
maarufu ulimwenguni, kuna ukweli
usioweza kukatalika, kuwa pia kila
mmoja wetu ni mtu binafsi mwenye
haiba ya aina yake ya kipekee.
Tujiulize haiba ni nini? Haiba ni
mwenendo wa binafsi wa jinsi mtu
anavyojiweka au kujiwasilisha kwa
jamii na namna anavyojirekebisha ili
kuendana na mazingira. Kwa hakika
hakuna watu wawili wanaofanana au
kulingana kwa kila hali. Hata watoto
mapacha ambao mimba yao
hutungwa kutokana na yai moja kisha
wakakuzwa na kulelewa katika
mazingira ya aina moja na
yanayofanana kwa kila hali bado
hutofautiana wanapokua.
Haiba ya mtu hujengeka kutokana na
nini?
Ili tuweze kuelewa vyema suala la
haiba ni vyema tuelewe haiba ya mtu
hujengeka kutokana na mwingiliano
wa vitu viwili ambavyo ni urithi wa
sifa kutoka kwa wazazi na taathira
kutokana na mazingira.
Elimu ya uzazi iitwayo “genetics”
hutoa ufafanuzi wa kibaolojia kuhusu
jinsi mtoto anavyoweza kurithi vitu
fulani kutoka kwa baba au mama. Hii
ndiyo maana mara nyingi tunaona
mtoto akifanana na baba au mama.
Kinachorithiwa kutoka na mchakato
wa kijenetiki ni kama vile ukubwa au
rangi ya macho, rangi na aina ya
nywele rangi ya ngozi, sura na
pengine hata umbo. Kwa upande wa
umbo mtoto huweza kuwa mrefu ama
mfupi kama mama yake au baba yake
ama anaweza kuwa mwembamba au
mnene kutokana na jinsi alivyo mmoja
wa wazazi wake.
Je mtoto anaweza kurithi, akili kutoka
kwa mzazi?
Labda kwanza tujiulize maana ya
akili. Tunaposema mtu ana akili
tunatumia neno akili kama uwezo wa
kufikiri na kuchambua masuala
mbalimbali na kubainisha kile
kinachofikiriwa kwa kufanya kitendo
au kutumia mawazo hayo kukabiliana
na changamoto za maisha. Hii ni aina
moja ya tafsiri ya akili miongoni mwa
aina kadhaa.
Kuna tafiti nyingi ambazo zimewahi
kufanyika ili kubaini kama akili
huweza kurithiwa na mtoto kutoka
kwa mzazi au hapana. Tafiti hizo
zimeonyesha dalili zinazoashiria kuwa
kwa kiwango fulani akili huweza
kurithiwa kidogo sana na kwamba
akili ya mtoto, kwa kiwango kikubwa
hujengeka kutokana na mazingira.
Imethibitika kuwa mazingira yana
umuhimu mkubwa katika makuzi ya
mtoto na wala siyo tu katika kujenga
tabia bali kwa kiwango kikubwa,
katika kujenga uwezo wa kiakili. Kwa
mfano iwapo mtoto atachangamshwa
nyumbani, akapata fursa ya kujifunza
kutoka kwa dada zake na kaka zake
na kama atapatiwa msaada wa
kuzitambua na kukabiliana na
changamoto za maisha malezi yake
yatakuwa na ufanisi mkubwa. Aidha,
tunajifunza kuwa hisia ya utamaduni,
maadili na uwezo wa kiakili ni
muhimu sana katika kumjenga mtoto.
Tukirudi kwenye uwezo wa kiakili
kama moja ya vitu vinavyoweza
kumfanya mtu atofautiane na
wengine ninakumbuka suala jingine
lenye mdahalo mkubwa. Wakati
fulani nilikutana na watu waliokuwa
na fikra kuwa watoto wa Kizungu
wana akili zaidi kuliko wa Kiafrika.
Sijui wewe msomaji una mawazo gani
kuhusu dhana hii. Je ni kweli rangi au
utaifa wa mtu unaweza kuwa kigezo
cha uwezo wa kiakili? Hata kabla
sijaendelea labda nieleze kuhusu
utafiti uliowahi kufanyika kuhusiana
na dhana hii.
Kuna wakati ulifanyika utafiti kwa
kuwachukua watoto wadogo wa
Kizungu na Kiafrika na kuwaweka
pamoja katika mazingira ya kijiji cha
Kiafrika. Wakalelewa pamoja katika
kijiji hicho kwa miaka kadhaa.Kwanza
iligundulika kuwa wale watoto wote
walianza kujenga tabia zilizofanana
kabisa katika michezo, namna ya
kusema na hata sauti zao zilifanana.
Jambo la ajabu zaidi wote waliweza
kuongea lugha moja. Walipoongea
wakiwa ndani mtu aliye nje hakuweza
kutofautisha kati ya sauti ya mtoto wa
Kizungu na mtoto wa Kiafrika.
Walipowapeleka shule ya chekechea
haikuonekana kama watoto wa
Kizungu walikuwa na akili zaidi kuliko
wa Kiafrika. Wote walikuwa na uwezo
ambao kwa wastani uliokuwa
karibuni sawa. Kuna baadhi ya watoto
wa Kiafrika walikuwa na maendeleo
zaidi kidogo kuliko wale wa Kizungu
katika mitihani kuna wakati aliongoza
mtoto wa Kiafrika na wakati
mwingine aliongoza mtoto wa
Kizungu. Utafiti huu ulithibitisha
kuwa hakuna tofauti ya akili baina ya
mataifa bali ni mazingira ndiyo
yanayojenga tabia na kuunda akili ya
binadamu.
Je tunatofautiana vipi?
Tunabaini kuwa kila binadamu ana
tabia yenye chembe ya kipekee
inayoweza kuwa imetokana na kurithi
kwa wazazi wake au kutokana na
mazingira. Lakini tunapolinganisha
kwa ujumla sifa za kimaumbile na
uwezo wa kiakili tunagundua kuwa
karibuni sisi sote tunafanana.
Kuna nchi moja iliweka kiwango cha
urefu anachostahili mtu awe nacho ili
kuajiriwa jeshini. Kiwango hicho
kilikuwa sentimeta 174.5. Walipo
wapima vijana waliofika kwenye usaili
waligundua kuwa asilimia 68
walikuwa na sentimeta 168 – 182,
asilimia 28 walikuwa na sentimeta 158
– 190. Ni asilimia 2 tu waliokuwa na
urefu wa chini ya sentimeta 157 na
asilimia 2 nyingine waliokuwa na
urefu wa zaidi ya sentimeta 191.
Takwimu hizi za urefu wa vijana
waliojitokeza katika nchi kutaka
kungia jeshini ni mfano wa jinsi
uwiano wa tofauti za vimo vya watu
katika taifa unavyoweza kuwa. Aina
hii ya mtawanyiko hufuata kanuni ya
kizingo cha kawaida ambayo kwa
kiingereza huitwa “Normal curve”
Hiki ni kizingo halisi cha hali fulani ya
idadi ya watu katika nchi inayoweza
kuwa. Ni dhahiri kuwa katika taifa
haiwezekani watu wengi wakawa
warefu au wafupi.
Kanuni hii ya taaluma ya kitakwimu
hawa haitumiki tu katika kuanisha
tofauti za kimaumbile bali huweza pia
kutumika katika kugawa mtandao wa
viwango vya akili, uadilifu, umakini na
uaminifu.
0 comments:
Post a Comment