Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo imetupilia
mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama Cha
Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama wake
ndani ya chama hicho.
Mahakama hiyo imekubaliana na hoja pingamizi toka
chadema dhidi ya kesi hiyo kwamba ilifunguliwa bila kufuata utaratibu wa
kisheria.
Katika Hukumu Mahakama hiyo imemuamuru Zitto Kabwe
kulipa gharama zote za kesi hiyo baada ya kujiridhisha kuwa hakufuata
kanuni za kufuangua kesi dhidi ya chama chake.
Aidha Mahakama imeamua katika hukumu yake kuwa
Chama kinaweza kuendelea na taratibu zake kama jinsi zilivyokuwa
zikiendelea kabla ya kuwekwa zuio.
Siku za hivi karibuni Mahakama kuu kanda ya Dar es
Salaam ilitoa zuio la muda kwa kamati kuu ya Chadema kutojadili
uanachama wa aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe
katika vikao vyake.
Januari mwaka jana Mahakama hiyo ilisikiliza hoja
za mawakili wa pande zote kuhusu maombi hayo chini ya Jaji John Utamwa ,
Mahakama hiyo ilitoa zuio la kutojadiliwa kwa uanachama wa Zitto Kabwe
hadi hapo kesi yake ya Msingi itakaposikilizwa.
Baada ya Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo
kutupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama
Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama
wake ndani ya chama hicho…
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu
ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe.
Akitangaza hatua hiyo ya kumvua uanachama,Lissu
amesema kanuni na sharia za chama hicho ziko wazi na zinaelekeza kuwa
endapo mwanachama yeyote atakishtaki chama hicho mahakamani na iwapo
atashindwa atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye chama






0 comments:
Post a Comment