WANAWAKE WAMFANYIA UNYAMA MWENZIO KISA WIVU

Author
Unyama ulioje! Wanawake wanne wanaojiita Kundi la ‘Boko Aramu, hivi karibuni wamemteka msichana
mmoja mrembo aitwaye Marry kisha kumfanyia kitu mbaya ikiwa ni pamoja na kumdhuru sehemu zake za
siri.
Akizungumza kwa tabu akiwa katika
Hospitali ya Mount Meru, Marry ambaye
anamiliki saluni ya kike alisema, chanzo
cha kufanyiwa hivyo ni wivu wa mapenzi
huku akimtaja rafiki yake wa karibu
aitwaye Maurin kuhusika.
Alisema, siku ya tukio akiwa ndani ya
saluni yake alifika Maurin na kumtaka
aende kwenye chumba chake kuna jambo
akamsaidie lakini alipofika huko
akashangaa anataitiwa.
“Ilikuwa saa mbili usiku, alikuja Maurin na
kuniomba niende katika chumba chake,
nilipofika tu mlangoni kwake
akanisukumia kitandani, mara nikaona
kundi la wanawake likinivamia na kuanza
kunishambulia.
“Walinipiga sana, baadaye walinivua nguo
zote na kunilaza kitandani kisha mmoja
akanifanyika kitendo cha kikatili ambacho
siwezi hata kukisimulia Niliumia sana, nikapiga kelele sana lakini
hawakuniachia,” alisema Marry na
kuongeza:
“Walizidi kunikandamiza, nahisi lengo lao
ilikuwa ni kuniua. Mara mwanamke
mmoja akaniuliza kwa nini natembea na
bwana wa Maurin. Nikashangaa kusikia
maneno hayo. Nikawaambia Maurin ni
rafiki yangu na wala huyo bwana wake
simjui. Basi wakazidi kunipiga.
“Mmoja akachukua kisu na kuniwekea
shingoni, mwingine akachukua kichupa
ambacho nahisi kilikuwa na tindikali,
ikabidi nijilazimishe kuamka na kuwapigia
magoti wasiniue.“Wakakubali kunisamahe
lakini wakadai niwalipe gharama zao
kwani wametoka Dar kuja kuniua.
Nikawaambia sikuwa na fedha, wakaitana
pembeni kisha wakaondoka na kuniacha
pale nikiwa na maumivu. “Walipoondoka tu nikaanza kupiga kelele na ndipo watu walipokuja kunipa msaada kisha tukaenda kutoa
taarifa katika kituo kikuu cha polisi na kufungua jalada la kesi lenye namba AR /RB /3717/2015,” alisema
Marry.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Arusha, Edward Balele alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa
mpaka sasa jeshi hilo linawashikilia
wanawake wawili kati ya wanne
waliohusika kumtendea unyama dada
huyo.

0 comments:

Post a Comment