Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeombwa kutumia busara wakati uteuzi wa
jina la mgombea urais kwa kupitia chama hicho kuangalia mtu anayependwa
na wananchi bila kukiathiri kwa kuteua mtu asiyekubalika.
Wamempendekeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (pichani), kuwa ndiye wanayemuona anaefaa kutokana na kukubalika.
Wito huo ulitolewa na taasisi ya Ilawa Improvement ya mkoani Njombe
kupitia Mwenyekiti wake, Nathaniel Mgani, ambaye alisema vikao vya CCM
vitakapompendekeza mtu atakayemrithi Rais Jakaya Kikwete iangalie mtu
anayekubalika kwa watu ili kutopoteza mvuto wa chama kwa wananchi
katika uchuguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
“Kwa niaba ya taasisi yetu tunapendekeza wanapoangalia mtu wa
kumuweka kugombea urais wahakikishe wanaweka mtu anayekubalika kwa watu
ili kuepuka anguko kubwa, sisi kama Ilawa tunampendekeza Edward Lowassa
kuwa mgombe wa urais,” alisema Mgani.
Aidha, alisema wakati Lowassa akiwa waziri mkuu hapakutokea mauaji ya ovyo ya raia wala vurugu katika maeneo nchini.
Mgani alisema Lowassa alipokuwa waziri mkuu hata Rais Jakaya
Kikwete hakupata shida kwa kuwa alikuwa na kiongozi aliyekuwa
anaisimamia serikali yake na kuwa ilikuwa imetulia.
Aliongeza kuwa wanamuona Lowassa ni kiongozi bora kutokana na
alivyosimamia maendeleo katika jimbo lake la Monduli ambalo lina
barabara nzuri, huduma za afya na huduma zingine za kijamii zenye
uhakika tofauti na maeneo mengine ya nchi.
Aliiomba Kamati Kuu ya CCM kumpitisha Lowassa kuwa mgombea urais wa
CCM kushindana na vyama vya upinzani kutokana na jina lake kuwa
masikioni mwa watu wengi na kwa kufanya hivyo chama hicho kitapata
ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment