Labda ni swali ambalo umekuwa ukijiuliza mara nyingi na hukupata jibu la kuweza kukutoa gizani kuhusu matumizi ya majina ya pili (surname) kwa sehemu kubwa ya wanandinga wanaokipiga kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza badala ya majina binafsi ya wachezaji.
Lakini pia inawezekana wakati mwingine umewahi ulijiuliza kwamba mbona
wengine hutumia majina yao ya utani (nicknames) badala ya majina yao
binafsi ama majina ya yao ya pili?
Hebu tuangane kwenye makala haya kwa maelezo na mifano mbalimbali kwaajili ya kupata majibu ya maswali hayo lakini pia kuweza kutoka gizani na kufahamu vyema matumizi ya majina mbalimbali kwa wanandinga kwenye ligi ya “Primia”.
Kwanza kabisa hebu tuangalie sheria inasemaje, kwenye moja ya sheria na taratibu za chama cha soka nchini Uingereza (FA) kuhusu majina kwenye jezi inasema “kila mchezaji atatakiwa kuvaa jezi ambayo kwa nyuma namba ya jezi na juu yake jina lake la pili (surname) vitaonyeshwa ama jina lingine ambalo limepitishwa na bodi kwa maandishi”.
Sheria imekuwa wazi kabisa kuonyesha kwamba katika jezi za wachezaji baada ya namba jina lake la pili (surname) ndilo linatakiwa kuonekana kwenye jezi hiyo hivyo tusishangae kuona majina kama Costa badala ya Diego, Gerrard badala ya Steven ama Milner badala ya James.
Lakini pia sheria imekuwa wazi kuhusu matumizi ya majina mengine ambayo ni ya utani (nicknames) kama vile Chicharito (Javier Hernandez), Kun Aguero (Sergio Aguero), Nani (Luis Carlos) majina ambayo shirikisho la soka itayaruhusu kutumika baada ya klabu husika kutuma maombi kwenye bodi ya shirikisho hilo na kutoa sababu za msingi.
Ili mchezaji wa timu fulani kuweza kuruhusiwa kutumia jina la utani na FA wakati mwingine timu hulazimika kupeleka vithibitisho vya picha kwamba mchezaji huyo amewahi kutumia jina hilo kwenye klabu nyingine.
Pamoja na kwamba sheria inasema mchezaji anatakiwa kutumia jina lake la pili ama jina lingine kwenye jezi lakini kuna wachezaji ambao walikuwa wakitumia majina yao ya kwanza kwasababu mbalimbali za kimsingi.
Mfano mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Manchester United Jordi Cruyff aliamua kutumia “Jordi” badala ya “Cruyff” ili kujitofautisha na baba yake ambaye pia alikuwa mchezaji siku za nyuma ingawa FA hawakutaka kutokana na sheria inavyosema.
Kipa wa zamani wa Bolton Wanderers Stelios Giannakopoulos aliamua kutumia jina lake la kwanza Stelios sababu ikiwa jina lake la pili ni gumu kutamka hasa kwa mashabiki wa klabu yake, jiulize nani anaweza kutamka “Giannakopoulos” kirahisi na kwa haraka?
Nafikiri kwa namna moja ama nyingine kutokana na makala haya basi tutakuwa tumefahamu kwanini wanadinga hutumia majina yao ya kwanza, pili ama majina yao ya utani
NAWASILISHA.
@Chikoti Cico

0 comments:
Post a Comment