Msanii Jose Chameleone wa Uganda akilia baada ya kumpoteza mdogo wake AK47.
Emmanuel Mayanja alimaarufu kama "AK47",mdogo wa mwanamuziki Jose Chameleone alikutwa ameanguka chooni na baada ya marafiki kugundua hilo ndipo walipomchukua na kukimbiza Hospital lakini bahati mbaya alifariki dunia njiani wakati akipelekwa Hospital ya Nsambya na walipofika hospital ndipo ikathibitika kuwa mwanamuziki huyo amefariki dunia.
"AY Pole sana kaka yangu Jose Chameleone kwa kumpoteza mdogo wako Gerald Mayanja @akfourtysevenmusic Mungu amlaze mahali Pema Peponi..Kuwa strong bro ndio maisha wote tunapita..Very Sad News ulinipigia ukijua ni mimi kumbe ni damu yako..Pole sana na tuko pamoja kwenye wakati huu mgumu."
AK47 ni baba wa watoto wawili ambao ni mapacha lakini pia ni mdogo kabisa wa msanii Jose Chameleone,Weasel na Pallaso.