MATOKEO ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika kote nchini juzi, yameanza kutangazwa huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiongoza katika maeneo mengi na kufuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi navyo vimefanya vizuri katika baadhi ya maeneo, ambako wagombea wake walisimamishwa na kuungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Kwa mujibu wa matokeo yaliyokusanywa kutoka sehemu mbalimbali nchini, ushindani mkubwa baina ya CCM na Chadema umeonekana zaidi katika miji ya Arusha, Bukoba, Moshi na Iringa.
Katika maeneo mengi, CCM imepata ushindi wa kishindo kwa asilimia kati ya 80 na 100. Mchuano mkali Arusha Vyama vya CCM na Chadema vimekabana koo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani Arusha, kutokana na CCM kuzoa viti 78 huku Chadema ikichukua viti 75.
Aidha, uchaguzi katika vituo vya Old Police na Mtaa wa AICC, unarudiwa leo kwa nafasi za wajumbe huku Mtaa wa Oysterbay uchaguzi ukirudiwa kutokana idadi ya kura kuzidi, tofauti na watu waliokuwa wamejiandikisha.
Akitoa matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mkurugenzi wa Manispaa Arusha, Juma Idd alisema CCM kati ya viti 78 viti sita imepita bila kupingwa huku Chama cha ACT, NCCR na TLP vikiwa havina watu waliochaguliwa.
Kuhusu kurudia uchaguzi huo, alisema kituo cha Old Police na Mtaa wa AICC Kata ya Sekei uchaguzi huo utarudiwa kwa Viti Maalum huku kituo cha Old Police kikirudia kutokana na kura za wajumbe wanne, kufungana kwa kila mmoja kupata kura 64, huku wajumbe wawili wakipita kwa kutofautiana kura.
Alisema mitaa iliyopiga kura ilikuwa ni 154, lakini kutokana na wingi wa watu baadhi ya vituo viliongezwa na kufikia 202. Wakati wa kuhesabu kura, vituo hivyo vilirudi na kufikia 154 huku baadhi ya vituo vya Longdom Kata ya Sokon 1 kura zilihesabiwa hadi saa 4:10 usiku.
“Uchaguzi umekwenda salama bila vurugu za aina yoyote, lakini kituo cha Oysterbay uchaguzi utarudiwa tena leo kutokana na idadi ya watu kuzidi na kuleta tafrani wakati wa kuhesabu matokeo pamoja na kituo cha Sekei na Old Police ingawa nakiri kuna kasoro zilijitokeza, lakini tuliweza kuzitatua,’’ alisema.
Alisema baada ya uchaguzi huo wa kesho kurudiwa kwa baadhi ya maeneo, wataandika ripoti ili kuboresha zaidi uchaguzi huo. Katika uchaguzi huo, vyama vya CCM, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, ACT na TLP vilichuana kuwania uongozi katika Kata 25 na mitaa 155.
ACT ilisimamisha wagombea 11, CCM 154, Chadema 152 na CUF 5. TLP na NCCR kila kimoja kilijaribu kwa kuwa na mgombea mmoja tu. Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Mwenyekiti wa Mtaa (1) kwa kila mitaa na Wajumbe (5) wa Kamati ya mtaa, kati yao nafasi tatu zitagombewa kwa pamoja baina ya wanaume na wanawake na nafasi mbili ni maalum kwa wanawake tu.
CCM yapeta Moshi Mjini Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambayo inatajwa kuwa ni ngome kuu ya Chadema, CCM imeendelea kuongoza. Msimamizi wa uchaguzi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Shaaban Ntarambe alisema uchaguzi huo ulifanyika kwa kufuata sheria na taratibu.
Alisema katika matokeo hayo, CCM imeshinda katika mitaa 28 na Chadema mitaa 26 huku mitaa sita iliahirisha uchaguzi wake. Halmashauri ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro ilitangaza matokeo ya Kata sita kati ya 31, huku Chadema ikionekana kuongoza ikifuatiwa na CCM.
Katika matokeo ya awali, Chadema ina vitongoji 64 na vijiji 10, CCM ina vijiji saba na vitongoji 45, NCCR Mageuzi ina vijiji viwili na vitongoji 12 na TLP ina kitongoji kimoja. Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Fulgence Mponji alisema wilaya hiyo ina jumla ya vijiji 157 na vitongoji 701, ambapo vijiji 19 na vitongoji 115 matokeo yake yamekamilika.
Akifafanua matokeo hayo, alisema katika kata za Makuyuni na Njiapanda zenye jumla ya vitongoji 18, CCM imeshinda vitongoji 11, NCCRMageuzi vitongoji vinne na Chadema vitongoji vitatu.
Alisema katika Kata ya Old Moshi Mashariki yenye vitongoji 19 na vijiji vinne, CCM imeshinda katika vitongoji 14 na vijiji vitatu, Chadema vitongoji 5 kijiji kimoja, Kata ya Uru Mashariki yenye vijiji saba na vitongoji 40 CCM imeshinda vijiji viwili vitongoji 10, Chadema vijiji vitano na vitongoji 30.
Mponji alisema katika kata ya Mbokomu yenye vijiji vinne na vitongoji 21, Chadema imeshinda vijiji vitatu na vitongoji 14 na CCM imeshinda kijiji kimoja na vitongoji saba. Katika Kata ya Kilema Kusini yenye vijiji vinne na vitongoji 17, CCM imeshinda kijiji kimoja na vitongoji vitatu, Chadema kijiji kimoja na vitongoji vitano na NCCR-Mageuzi vijiji viwili, vitongoji vinane na TLP kitongoji kimoja.
CCM yapata viti 35, Ukawa 31 Bukoba Wakati hali ikiwa hivyo Arusha na Moshi, katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, CCM imenyakua mitaa 35 huku Ukawa wakipata mitaa 31 kati ya mitaa 66 ndani ya Manispaa hiyo. Katibu wa CCM Manispaa ya Bukoba, Abdul Kambuga, alithibitisha kwa kusema chama chake kimepata viti 35.
Kabla ya uchaguzi wa mwaka huu, CCM ilikuwa na mitaa 55 wakati vyama vya upinzani kwa ujumla wao vilikuwa na viti 11. Alisema uchaguzi huo umegubikwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo baadhi ya watu kujiandikisha kwenye mitaa wasiyoishi.
Alidai sheria za uchaguzi hazikufuatwa na msimamizi wa uchaguzi wa manispaa alikiuka ibara ya 19 kifungu cha 6, kinachomtaka mpiga kura kuonesha kitambulisho na hawakufanya hivyo.
Katika wilaya ya Muleba, Katibu wa CCM wilayani humo, Anatory Nshange alisema wilaya hiyo ina jumla ya Vijiji 166, lakini hadi sasa yametangazwa matokeo ya Vijiji 84, ambapo CCM imeshinda 52 na Chadema 32.
CCM ilipata ushindi wa bila kupingwa katika vijiji 13. Aidha, imeelezwa katika wilaya za Kyerwa na Ngara, baadhi mitaa hawakuweza kufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo dosari katika vifaa vya kupigia.
Dodoma yote ni CCM Matokeo yanaonesha kuwa CCM imeshinda katika takribani wilaya zote za mkoa wa Dodoma. Katika wilaya ya Dodoma Mjini, CCM imebomoa kambi ya upinzani katika kata za Dodoma Makulu, Iyumbu na Ipala na kupata ushindi mkubwa Katika kata ya Dodoma Makulu yenye mitaa saba, CCM imeshinda mitaa sita ambayo ni Medelii, Mwangaza, Bwawani, Njedengwa Mashariki, Msangalale Mashariki na Msangalale Magharibi huku mtaa mmoja wa Njedengwa Magharibi uchaguzi wake ukiahirishwa.
Kata ya Iyumbu yenye mitaa saba, CCM imeshinda mitaa mitatu ambayo ni Mwinyi, Nyerere, Iyumbu na mtaa wa UDOM, ambao uchaguzi wake unarudiwa huku Kata ya Ipala yenye mitaa miwili ya Ukombozi na Mwinyi ikichukuliwa na CCM.
Mpaka sasa CCM imepata ushindi katika kata za Majengo, Madukani, Makole, Hazina, Kilimani, Viwandani, Kikuyu Kusini, Kikuyu Kaskazini, Mnadani, Kiwanja cha ndege, Ihumwa, Mtumba, Mbabala, Mbalawala, Mpunguzi, Ipala, Chahwa, Hombolo, Makutupora, Nala na Zuzu. Katika uchaguzi huo, CCM imeshinda katika vitongoji vyote 89 vilivyopo katika manispaa hiyo, vijiji 19 vyote vimechukuliwa na CCM na katika mitaa 170 iliyopo CCM imechukua mitaa 164.
Mitaa ambayo Chadema imefanikiwa kuipata ni mitano ambapo ni mtaa wa Chinyika kata ya Mkonze, Mtaa wa Relini kata ya Kizota, mtaa wa Swaswa na Mlimwa C kata ya Ipagala na Kikombo Makulu.
Wilayani Chemba, vijiji vilivyofanya uchaguzi ni 1013 na matokeo yaliyopatikana ni ya vijiji 100, ambapo kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji, CCM imeshinda vijiji 73 Chadema 9 na CUF 14.
Matokeo hayo yalitolewa na wakati Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, William Mafwere, wakati akizungumza na gazeti hili. Imeandikwa na Veronica Mheta (Arusha), Nakajumo James (Moshi), Angela Sebastian (Bukoba) na Sifa Lubasi (Dodoma).

0 comments:
Post a Comment