Polisi ahukumiwa kunyongwa

Author
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa polisi wa upelelezi, Maduhu, F 5842, 
aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa
 Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Daniel Mwakyusa.
 
Aidha, mahakama hiyo imewaachia huru washitakiwa wengine wawili wa kesi hiyo, polisi wa upelelezi,
 Shaaban, F 7769, na polisi wa kike mpelelezi, Neema, F 6545, baada ya kuwakuta hawana hatia.
Hukumu hiyo ya kesi namba 16 ya mwaka 2013, ilitolewa jana mjini hapa na Jaji Rose Temba, 
baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.
Awali, ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali, Archiles Mulisa akisaidiwa
 na Catherine Paul kuwa washitakiwa walifanya mauaji ya kukusudia Februari 14 mwaka 2012 kinyume cha
 Kifungu Namba 196 cha Kanuni ya Adhabu sura 
ya 16 kama ilivyofanyiwa Marejeo mwaka 2002.
Mulisa alidai washitakiwa hao kwa pamoja walihusika na mauaji ya Daniel Mwakyusa
 baada ya kumpiga kwa kutumia silaha inayodhaniwa kuwa ni bunduki, nje ya ukumbi 
wa starehe wa Universal uliopo Uyole jijini Mbeya. 
Akitoa hukumu ya kesi hiyo, Jaji Temba alisema anawaachia 
huru mshitakiwa namba mbili, 
Shaaban ambaye alikuwa dereva wa gari ya polisi kwa kuwa
 ushahidi uliotolewa, unadhihirisha kuwa alibaki ndani ya gari akimsubiri 
mshitakiwa namba moja aliyeshuka na kuingia kwenye ukumbi wa Universal.
<Kwa upande wa mshitakiwa namba tatu, Neema, Jaji Temba alisema aliridhishwa na mshitakiwa
 huyo kutohusika na mauaji kwa kuwa siku ya tukio alikuwa akijisikia vibaya, hivyo alilazimika 
kubaki na dereva kwenye gari.
Jaji Temba alisema mshitakiwa namba moja, Maduhu, anahusika moja kwa moja na mauaji hayo, kutokana
 na ushahidi wa kimazingira, kwani yeye ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kuondoka na Daniel Mwakyusa eneo 
la tukio na kumpeleka kwenye gari.
Alisema sababu ya pili, ushahidi ulionesha kuwa silaha yake pekee ndiyo iliyotumika, tofauti na za 
askari wengine kwa kuwa risasi tatu zilionekana kupungua kati ya zile alizokabidhiwa sambamba na ushahidi 
wa maganda matatu ya risasi, yaliyookotwa eneo la tukio.
Jaji Temba alisema sababu ya tatu ni kuwa ushahidi uliotolewa, unaonesha kuwa mshitakiwa huyo alikuwa wa mwisho
 kurejesha silaha, hivyo kuhusishwa moja kwa moja na mauaji hayo.</p>Alisema kutokana na sababu hizo, mahakama
 inamtia hatiani kwa kuua kwa kukusudia,
 hivyo mshitakiwa Maduhu,
 amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.</p>
Awali, ilidaiwa kuwa siku ya tukio ilikuwa Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day), ambapo mtuhumiwa akiwa 
doria na askari wenzie, alimkuta Daniel Mwakyusa akiwa kwenye eneo la starehe na mwanamke anayesadikiwa 
kuwa alikuwa pia na mahusiano na askari huyo.
<!-- DISQUS comments block -->

0 comments:

Post a Comment