kochaMkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa
ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini
Mbabane. Akizungumza jijini Dar es salaam, Nooij amesema kikosi hicho kinachotarajia
kuingia kambini Novemba 10 kitafanya mazoezi mara moja ambapo ni jioni
na baada ya hapo Novemba 11 kitaondoka kuelekea nchini Afrika Kusini
ambapo kitaweka kambi ya siku mbili na Novemba 13 kitaeleka nchini
Swaziland kujiandaa na mechi hiyo.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam)
na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar),
Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka
(Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua
(Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari
Kapombe (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo
(Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said
Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP
Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas
Ulimwengu (TP
0 comments:
Post a Comment