HATUKUPENDA TUWE HIVI -28

Author

"Kuna vijana wawili wamekufa alafu ni wanafunzi wa hii shule aliyosoma marehemu Josephat" ilikua taarifa ya ghafla sana kila mtu alionesha hali ya kutoamini, "wamekufaje?" aliuliza dada mmoja aliyejifunga doti, "wamegongwa na gari ila kwa uzembe wao maana walikua walevi wakasimama katikati ya barabara" kijana huyo alijibu kwa sauti ya chini.Hali hiyo ilipelekea kila mtu pale kuangua kilio kwani walihisi kama kuna pepo la kuua wanafunzi kwa kipindi hicho, "mh! kuna kitu,,haiwezekani hata wiki haijaisha wafe wanafunzi watatu kwenye shule moja" kijana mmoja aliongea kwa hasira. "hao vijana majina yametambulika kweli?" mama mmoja mwenye mtoto wake anayesoma Arusha Secondary,aliuliza kwani mama huyo alipatwa na na wasiwasi maana mtoto wake ni mnywaji wa pombe sana, "kwa nilivyosikia majina waliyokua wakiitana kabla ya kugongwa na gari ni Brown na Chris ila siwezi kuwajua nani Brown na nani Chris, "ahaa pole zao jamani kwa hiyo miili imepelekwa Mount Meru au wapi?" mama mwingine aliuliza, "ndio hapo imepelekwa" alijibu kijana huyo na maombolezo yakaendelea kama kawaida,hali ya huzuni ikiongezeka mara mbili zaidi  ya ilivyokua mwanzoni. *** Mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi Angel alishtuka usingizini, haraka aliingia bafuni na kujiandaa na shule,kichwani mwake alijaa mawazo kuhusu kifo cha Jesophat, "mungu nisamehe kwa kosa hili" Angel alianza kuumia na kulia kwa kitendo alichokifanya.
Genes naye alikua akisikitika kumpoteza rafiki yake kipenzi, "dah chali wangu aise kafa kiutani aise ama kweli dunia mapito leo unakua naye kesho hayupo jamani inauma sana" yalikua maneno ya Genes akikaribia lango la shule, "leo vipi mbona makundi sana huku shule" Genes alishangaa kwani aliona wanafunzi wakiwa katika makundi pia aliona kila kundi likiwa katika mfumo wa kupashana habari mpya, "vipi mpenzi umesikia tena habari mpya?" Angel alimfuata Genes na kumuuliza, "ipi tena zaidi ya kuzikwa kwa Josephat jana?" Genes alijibu huku akitaka kujua ni habari gani mpya, "nasikia jana usiku Brown na Chris wamepeta ajali na kufa" Angel alijibu, "sangapi wamepata hiyo ajali?" Genes aliuliza kwa mshangao, "usiku"Angel naye alijibu, " itakua walikua walevi kama kawaida yao,wakishalewa  huwa wabishi na mara nyingine hujifanya traffic (askari wa barabarani )"Genes alieleza kwa machungu huku akikilaani kitendo chao cha kulewa sana.

0 comments:

Post a Comment