HATUKUPENDA TUWE HIVI-27

Author

Baada ya mda waliamua kuondoka na kuenda kujipongeza kwa kunywa pombe, "twende zetu tukapige mvinyo bwana, hicho chakula cha marehemu sisi hatuli" Chris aliongea huku wakiondoka eneo la msiba na kuacha waombolezaji wakipata chakula. Walienda kwenye duka moja wakaagiza pombe za karatasi (viroba) wakanywa kwa hasira, "hawa wanafunzi wanakunywa pombe hivi watafaulu kweli?" muuzaji alijiuliza kimya kimya kwani walikua wakinywa kupita kiasi. Baada ya masaa mawili walikua wamelewa sana, "twende zetu mwana" Chris alimtaka Brown waondoke kuelekea nyumbani, "dah mwana naona nishazimika kabisa hebu nishike mkono" Brown alijibu huku akinyoosha mkono wake aweze kusaidiwa, "watafika kweli hawa?" muuza duka alisema baada ya kuona jinsi Brown na Chris walivyoondoka kwa kukokotana huku wakipepesuka huku na huko, "wanajifariji mwanafunzi mwenzao kafariki" mama mmoja alisema baada ya kuona wamevaa sare za Arusha sekondari. *** Anitha alizidi kuchanganyikiwa kwani hakuamini  kama ametapeliwa kila kitu cha Miriam tena ambaye yupo chini ya ulinzi wa polisi, "sasa haya mawazo aliyonayo juu ya hii kesi anayopewa je nikimuongezea haya  ya  kupoteza kila kitu siatachanganyakiwa kabisa" Anitha alijisema baada ya kuona msiba ukiisha na Miriam kupakiwa kwenye gari. Anitha alimfuata mwajiri wake na kumueleza kila kitu kilivyotokea, "huyu mtoto ni mchapakazi sana lakini mbona wanamtesa hivi"Mzee Massawe aliongea huku akilengwa machozi, "acha tu boss mimi sijui nitamlipa nini maana yeye ndie amenisaidia hadi hapa nilipo" Anitha alimuelezea mzee Massawe kila kitu na jinsi Miriam anavyopambana na maisha. Hadi kufika kazini tayari mzee Massawe ashazidi kumuamini Miriam na kumuona ni mmoja kati ya wanawake wapambanaji sana wanaopenda mabadiliko, "usijali nitamsaidia kila kitu kitakua sawa" mzee Massawe alimuondoa Anitha wasiwasi na Anitha alishukuru mungu kimoyomoyo kwani aliamini boss wake atamuanzishia Miriam maisha mengine. Waliokua wanafanya kazi na Miriam akiwemo Anitha,walikua na majonzi makubwa hadi kukafanania kana kwamba ni mfanyakazi mwenzao kafariki, "boss nenda kituoni jamani kamtoe Miriam tunampenda akiwa kazini" wafanyakazi walilalamika kwa majonzi, "nenda hata utumie mishahara yetu kumtoa" alisema mmoja wa wafanyakazi ambae alilia machozi kabisa, "msiogope atatoka kesho kutwa maana imechunguzwa na imegundulika yeye sio aliyesababisha mauaji ya huyo kijana" mzee Massawe aliwaondoa wasiwasi juu ya Miriam kufungwa gerezani.Wote walifurahi kusikia hivyo walilia machozi ya furaha na mzee Massawe akazidi kujionea ni jinsi gani Miriam alipendwa na kila mtu. *** Usiku wa mazishi ya Josephat ulikua wa majonzi kwa wanafunzi na waalimu wote wa shule ya sekondari Arusha. Aliyekua rafiki yake wa kike alilia sana lakini alijipa moyo kua ipo siku atakutana nae mbinguni na wataendeleza mapenzi yao ili waweze kufikia malengo ya kuishi pamoja waliyopanga. Wanafamilia na majirani wa marehemu Josephat walikusanyika nyumbani usiku moto
uliwashwa nje watu wakakesha kuomboleza, "yule mtoto hajaua naona kuna kitu kilifanyika hapa" mwanafamilia mmoja alisema kwa kuelezea hisia zake juu ya Miriam alivyoonekana mwenye  majonzi makubwa, "mimi nimeamua kumsamehe namuachia mungu ndio muweza wa  yote na ndio anajua sababu ya haya"  baba marehemu alijibu. Majira ya saa mbili usiku watu waombolezaji wakiendelea na maomboleza,kijana mmoja alifika ghafla na kutoa habari iliyoshtua watu wote na kuwafanya waanze kilio upya. *** "Ina maana kweli mimi ndiye niliefanya watu wote pale watokwe machozi pia mimi ndiye niliempotezea mama Josephat mtoto wake aliyeteseka naye miezi tisa tumboni ? ama kweli nina makosa makubwa sana ila yote haya ni kwa sababu akina Chris wanalijua lile tukio langu kumuua yule mwanaume mwingine sasa watanitesa hadi lini?" Angel aliwaza hayo kwa machungu kwani alilazimishwa kuuwa ili atunziwe siri yake  ya mauaji, "hiki kifo cha Josephat kimenitoa machozi kwa kweli na sitaua tena, na hata mbele za mungu naapa kuacha mauaji" Angel alilia sana huku akijutia kitendo alichofanya cha kutia watu machungu mbaya zaidi alimfikiria Miriam anayeteseka mahakamani. "Sasa mungu atanisamehe vipi?" Angel alizidi kulalamika na baada ya mda usingizi ukamchukua.

0 comments:

Post a Comment