Majonzi yalizidi kutanda kila kona ya shule kwani ndani ya wiki moja walikufa wanafunzi watatu kwa ajali, bendera ilipepea nusu mlingoti kwa tukio hilo,kila mtu aliamini kitu kinachoendelea ni mambo ya kishirikina, lakini haikua hivyo kwani kila kitu kilichotokea kilikua na sababu ya kutokea. Kwa Angel ilikua furaha kubwa kutokea kwa kifo cha Chris na Brown kwani ndio walikua maadui zake waliomshurutisha kuua, "Mungu anisamehe sana sitakaa nifanye mauaji yoyote maishani mwangu" Angel aliapa kimoyo moyo. *** Shughuli za mazishi ya Chris na Brown zilifanyika na baada ya siku tatu walizikwa ,ilikua majonzi makubwa sana kwa familia zao kupoteza vijana wao, wazazi walisikika wakisema "jamani vijana wa kiume wanakufa wakiwa bado wadogo na hata watoto hawana,mimi mtoto wangu wakiume akizalisha akiwa na miaka kumi na nane ni halali jamani waache kizazi chao kikiendelea". *** Baada ya wiki mbili Miriam aliachiwa huru na kurudi uraiani kama kawaida, "Miriam ni wewe?" Anitha alimkimbilia Miriam aliyeshushwa kwenye gari la polisi, "ndio ni mimi"Miriam alijibu huku akimfuta Anitha machozi. Kila mtu pale alilia sana kiasi hadi Miriam akachukua jukumu la kuwabembeleza, "jamani msilie nishaachiwa huru" Miriam alisema kuwaihi wenzake wasilie, "yanini sasa walienda kukukondesha huko gerezani tu huna hata kosa jamani" mfanyakazi mmoja alisema kwani Miriam alikua kama vile kapungua sana, "acha tu ndugu yangu,usiombe uingie kwenye mkono wa serikali nakwambia utakonda tu tena ukute umeingia hujui hata kosa lako lazima uwe hivi" alijibu Miriam huku akionesha jinsi alivyokonda mikono na shingo. Siku hiyo katika hotel Miriam aliyofanya kazi basi kulifanyika tafrija ndogo,iliyoongozwa na mzee Massawe ambaye alikua mmiliki, "jamani basi wapendwa leo hii tafrija ni ya kusherekea kitendo cha mfanyakazi mwenzetu kuachiwa huru kwani alikua jela bila hatia,licha ya kusherekea basi kutakua na mchango wa
kumpa pole kwani alipokua gerezani,aliibiwa vitu vyake vya nyumbani kwa utapeli aliofanyiwa rafiki yake Anitha bila kujua" mzee Massawe aliongea mengi na baadaye shughuli ya kuanza kumchangia ilianza, wafanyakazi wenzake walimchangia kwa moyo mmoja, "ama kweli ukikaa vizuri na watu unavuna matunda mazuri" dada mmoja alisema kwa sauti ya chini baada ya kuona hadi wafanyakazi wengine wakiahidi kumpa Miriam mshahara wao wa mwezi mzima, hakika Miriam alipata furaha kuona anapendwa na wengi. "Unaona kama nilivyokuambia Miriam utakuja kua mtu mkubwa na tajiri sana" mzee Massawe alimnong'oneza Miriam kwani walikaa wote kwenye jukwaa. Tafrija iliisha na mchango ulihesabiwa pale pale, "jamani sisi kama wanafamilia,tunaopendana kwa shida na raha tumemaliza zoezi letu kwa uzuri,nimefurahi kwa mchango wenu mkubwa mlioonyesha kwa huyu ndugu yetu,ni vizuri mkawa mnafanya kazi mkiwa na upendo kama huu,msibaguane kama baba wa taifa hili Nyerere alivyotusihi tuishi kwa upendo na umoja,kweli kwa tafrija hii basi tumepata kiasi cha shillingi Milioni tatu pesa taslimu na ahadi ni milioni moja na nu,,,,,,". Hata kabla ya kumaliza kuongea shangwe na vigelegele vilisikika kwa kishindo. " Haya tumpe Miriam nafasi kidogo atoe shukrani zake pia" mzee Massawe aliongea na kumkabidhi Miriam kipasa sauti naye aseme neno, "jamani kwanza niwashukuru kwa upendo wenu kwani sisi ni kama wanafamilia na tunatakiwa kukaa kwa upendo huu hadi mwisho kwani umoja ni nguvu, kwa sababu jumla ya pesa zote ni milioni nne na nusu basi mimi nitachukua milioni mbili tu nikanunue vitu vyangu vilivyoibwa lakini hii milioni mbili na nusu sisi kama wanafamilia basi tutaanzisha mradi wetu ambao kila mfanyakazi akipatwa na tatizo basi unamsaidia, au tuwe tunakopesha watu pesa na kutulipa kwa riba ndio tutafika mbali zaidi kwani tukifanya kazi kama familia basi tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa au mnasemaje ndugu zangu?" "ndioooooo tufanye hivo" Kila mtu pale alifurahia wazo la Miriam kwani hakuna mtu aliyewahi kuwaza hivo pale kazini na kila mtu alishangaa jinsi Miriam alivyokataa kuchukua pesa zote, "hakika hapa huwezi amini kama huyu mtoto hajaenda shule wala hajui hata kusoma wala kuandika kitu" Anitha alijisema moyoni kwa kuona jinsi Miriam anavyowaza mbali. *** Kwakua basi Miriam hakua na mahali pa kulala kwa siku hiyo alienda kulala na Anitha, "Vipi Genes hajawahi hata kuniulizia hapa?" Lilikua swali la kwanza Miriam alilomuuliza Anitha walipoingia ndani, "ha wewe acha ujinga yani mimi najua hutamuwaza tena huyu mbwa aliyekufanya uteseke hivi kama sio huyu mbwa Genes unafikiri ungeenda polisi kwa mambo haya?" Anitha alimjibi kwa hasira, "usimuite mume wangu mbwa hata siku moja" Miriam alijibu kwa hasira za utani, "haya ila unapoelekea mapenzi yatakupeleka pabaya" Anitha alijibu, "kwa hiyo nisipende ? kama nimeumbwa na hisia ni haki yangu kupenda" Miriam alijibu kwa kujiamni, "subiri upendwe basi mdogo wangu" Anitha alizidi kumsisitiza Miriam ila Miriam katu hakusikia kitu, "sasa kama nimemuona mwanaume nikampeda kuna haja gani ya kusubiri kupendwa, cha kufanya ni kumwelezea hisia zangu,allah?" huo ndio ulikua wimbo wa Miriam kila kukicha.
HATUPENDA TUWE HIVI -29
14:02:00
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment