HATUKUPENDA TUWE HIVI-26

Author

uyu mtu itakua kaenda wapi?” Anitha alizidi kuchanganyikiwa baada  ya kusubiri kwa mda, lakini ghafla alijiwa na wazo la huenda katapeliwa kwani alianza kujiuliza kuhusu ujumbe toka kwa Miriam,kwani alikumbuka Miriam hajui kuandika wala kusoma, “itakua nimefanyiwa kama yule dada wa siku ile pale kituo cha mabasi” Miriam alijisemea huku akirudisha kumbukumbu nyuma kwa kukumbuka jinsi siku ,moja dada mmoja aliibiwa kwa kutoa kila kitu kisha kuja kukumbuka badae hivyo nae kumbukumbu zilianza kurudi taratibu alianza kulia kwa uchungu kwani kumbukumbu zilishamjia na ashaamini kua kaibiwa, “kulilkoni binti mbona unalia?” aliuliza baba mwenye nyumba ya Miriam, “kuna watu wameniibia baba” Anitha alijibu huku ameinamisha kichwa chini, “wamekuibia nini na mbona umetoa godoro nje,kwani huyu ndugu yako anaendeleaje huko?” huyo baba aliuliza akiwa anashangaa godoro lililokua nje wakati siokawaida, “ndio hivo baba kuna kaka kaja kasema ametumwa na Miriam kua niwape vitu eti anahama sasa ameniambia nimsubiri aje kuchukua hili godoro lakini cha ajabu masaa mawili yameshaisha nabado hajaja na kwanza walipoondoka nimegundua hawajatumwa na Miriam,maana Miriam namjua anajua sana kuzingatia suala la umakini hivyo kuna kitu hapa”Anitha alijibu huku akirudisha godoro ndani tayari kupanga safari yakuelekea kituo cha polisi kuripoti pia kumtaarifu Miriam, “hutampa presha kweli ukienda kumtaarifu huko aliko maana ni kwenye matatizo mengine ?”huyo baba alimuuliza, “sasa baba nisipoenda sahivi sijui atanielewaje maana alinikabidhi kila kitu chake hapa sasa sijui kama atanielewa jamani” Anitha alijibu kisha kutimua mbio ili aweze kupitia kazini kwake na kumpa tajiri yake taarifa. *** “Mumpe ulinzi wa kutosha”ilikua sauti ya askari akithibitisha Miriam akitoka kuenda kuhudhuria msiba waJosephat “sawa mkuu” alijibu mwenzake. Miriam alipakizwa kwenye gari ya polisi chini ya ulinzi wa askari wawili, “tena una bahati wewe mtoto kwani washtaki wako wamekuombea tu ukazike nahii kesi yako inaweza kuisha maana umeua mtoto wa wazazi wenye utu sana,sijui
wewe mchawi gani maana unaonewa huruma kabisa na wazazi wa marehemu”yalikua maneno ya askari mmoja akiyaelekeza kwa Miriam wakati wakiwa njiani. Miriam alilia sana kuitwa muuaji ingali anajua kabisa hajaua na hana roho ya kuua    “mimi sijaua” Miriam alijibu kwa hasira ingawa moyoni alifarijika sana kusikia anaonewa huruma na wazazi wa Josephat kwani alifikiri labda itakua imejulikana kua yeye sio muuaji *** “Parapanda inalia parapanda,parapanda inalia parapanda,ndugu yetu amekwisha nyakula kumlaki bwana yesu mawinguni” zilisikika sauti za wakina mamawakiimba kwa uchungu katika msafara uliotokea Mount Meru hospital ambapo ndiko mwili wa Josephat ulihifadhiwa. Wanafuzi wa shule ya sekondari Arusha waliandamana na mwili wa marehemu kutoka chumba cha kuhifadhia maiti,wanafunzi wa kike walionekana kulia zaidi njiani huku wakiume wakitembea kwa ukakamavu huku wakiacha vifua wazi  kuashiria hasira ya kuondokewa na mwenzao. “Am crying because he is my husband”(nalia kwa sababu huyu ni mume wangu) Happy aliongea kwa uchungu huku akizidi kulia njai nzima kwani aliyekufa alikua rafiki wake wa kiume,alikua akikumbuka mipango yao ya kuoana badae na jinsi walivyozoea kuongea pamoja, “siamimi kama ndio tunaenda kukuhifadhi katika nyumba yako ya milele,wakati tulipanga kuja  kujenga nyumba yetu sote” hakika ilikua siku ya huzuni kubwa kwa Happy,alibebwa na wenzake hadi msibani. “Hadi huku msibani kumekuja maaskari?”Angel alijiuliza baada ya kuona gari lenye nendo ya PT (POLICE TANZANIA) likiwa limepaki nje.Msiba ulikua na watu wengi lakini sare za shule ziliwatambulisha vyema wanafuzi waliosoma na marehemu.Katika taratibu za mazishi baada ya mwili kufika nyumbani uliingizwa ndani kwa ajili ya kuagwa kwa mara ya kwnza ndipo ifanyike ibada fupi ya kikristo kasha mwili ukazikwe, “ndugu waombolezaji basi tayari mwili ushaingizwa ndani na tutaanza  kwa utaratibu wa kuingia ndani kuuga mwili kwa mara ya kwanza kabla ya ibada,hivyo basi tupange mstari mmoja kwa haraka kuokoa mda, tuanze na wanafunzi waliosoma nae enzi za uhai wake tukatoe heshima za mwisho” yalikua maneno ya MC John Shirima akitoa utaratibu wa kutoa heshima za mwisho. *** “Jamani kuna wezi wameiba vitu vya Miriam vyote” yalikua maneno ya Anitha mara baada ya kufika kazini kwake huku akionekana kuhema sana, “mbona hatukuelewi au umechanganyikiwa “aliuliza mmoja wa wafanyakazi “sio kuchanganyikiwa,boss yuko wapi nimpe hii taarifa aipeleke kituo cha polisi ili ampe na Miriam taarifa?”Anitha alizidi kuongea kama mtu aliyechanganyikiwa hadi wenzake wakawa wanamcheka “boss kaenda kwenye  huo msiba wanaodai Miriam ndiye kauwa,maana pia
am kaitwa kwenye msiba pia na siunajua Miriam na boss wanaenda sana hivyo boss kasema anaenda hakikisha usalama wa Miriam” alijibu msichana mmoja. Anitha alizidi kuchanganyikiwa kwani hakujua afanye nini kwa mda huo “nakuishi kwangu mjini mda mrefu hivi leo natapeliwa, tena mali za mtu”Anitha alijisemea moyoni huku akiona kilichotokea kama ndoto ambapo atazinduka mda wowote na kukuta vitu vya Miriam vikiwepo tena, “hata ningejua nikakariri namba za lile gari afadhali,sijui kama Miriam atanielewa mimi”ni maneno ya Anitha ambayo yalimaanisha ningejua inavyokuja baada ya tendo. *** Watu walizidi kulia kwa uchungu kwa kifo cha Josephat,nae Miriam alizidi kuomboleza akiwa ndani ya gari kwani watuwakiwa wanatoa heshima za mwisho kwa mara ya kwanza bado Miriam alikua ndani ya gari ya polisi yeye aliona kila kitu kupitia kioo cha gari ambacho hakikuruhusu mtu aliyeko nje kuona ndani. “Sasa simnitoe namimi nikatoe heshima za mwisho jamani?” Miriam aliomba kushushwa kwenye gari, “wewe subiri utashuka tu”alijibiwa na mmojawapo ya askari, “jamani naomba” Miriam alizidi kuomba msaada wa kuruhusiwa kuenda kutoa heshima za mwisho lakini alinyimwa ruhusa kutokana na sababu za kiusalama ,wao walisubiri hadi mda wakuuaga mwili kwa mara mwisho ndipo atapewa ruhusa. “aise umecheki alivyokauka?”Brown alimuuliza Chris walipotoka kungalia mwili maana walifuatana, “kawa kama kama mamba”Chris alijibu huku wakijisifu kwa kazi waliyompa Angel kua aliifanya kwa ustadi wa hali ya juu na akafanikiwa kwa asilimia mia. Baada ya dakika arobaini na tano zoezi la kutoa heshima za mwanzo lilikamilika na mwili ulitolewa nje tayari kuanza  ibada. *** “Mamasamahani ni kwenye huu msiba wa kijana aliyeuawa kwa sumu mnaenda?”Anitha aliuliza kinamama aliowakuta njiani wakiwa wamejifunga doti za kanga, “ndio mwanangu ni huko tunaenda kama na wewe unaenda basi tunaweza kuandamana” huyo mama alijibu na wakaanza kutembea kwa kasi. Sehemu ya (iii) Hakika siku ilikua mbaya kwa Miriam kwani alijiona mkosefu mbele za mungu na jamii yote hasa pale alipotolewa kwenye gari ili aangalia na kuaga mwili wa Josephat ambae kila mtu aliamini kua ndiye aliyetekeleza mauaji hayo. "Kwani nimekufanyaje mungu wangu mbona mwanao nataseka au wazazi wangu walinilaani kwa kutoroka kifo ambacho kingetokana na mimi kukeketwa ?" Miriam alisema kwa sauti akirudishwa ndani ya gari la polisi kwani tayari alikua kashaaga mwili wa marehemu na alishuhudia jeneza likibebwa na vijana ili kuenda kaburini tayari kufukiwa. Wakati huo Chris na Brown walikua wakipongezana kwa kilichokua kikiendelea, "Hata Angel hafai aise" Chris alimnong'oneza Brown, "aise hata mimi nimemwaminia kabisa amemuua kama mtu anayeua kuku" Brown alijibu.

0 comments:

Post a Comment