MIMBA YA JINI 27

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_jini-27-

NATUMAI MMEFURAHIA SIKUKU VEMA KABSA NIPE USHAURI WAKO KUHUSU STORY HIII ILA MATUSI STAKI #LIKE PAGE VIPANDE VINAVYOENDELEA VISIKUPITE ONYESHA UPENDO #SHARE STORY NIPOST NYINGNE

ILIPOISHIA:
“Basi nikuache ufanye kazi.”
“Nashukuru.”
Shehna aliaga na kuondoka na kumuacha Mustafa akijiandaa kuanza kazi ya siku ile.
SASA ENDELEA...

Msichana mmoja alionekana amelala chini ya mti mkubwa pembeni ya barabara kuu ya kutoka Dodoma kwenda Mpwapwa akiwa amejifunga kipande kichafu cha khanga kwa chini na juu matiti yalikuwa wazi.
Miguu ilikuwa pekupeku, ilijaa tope lililokauka na kujaa vumbi. Wasamaria wema waliopita njia ile waliamini yule ni mwendawazimu, lakini ilikuwa ajabu kwa eneo lile hakuna hata mmoja aliyekuwa akimfahamu.
Toka watu walipomuona amelala chini ya mti, ilipita zaidi ya saa sita bila kugeuka kitu kilichowatisha na kufikiria labda amefariki.
Walimsogelea na kumtikisa, alifumbua macho kuwatazama lakini alikuwa amechoka kwa njaa na uchovu. Walimchukua na kumpeleka kwenye makazi ya watu na kumpatia chakula baada ya kushiba, walimpatia maji ya kuoga na nguo. Alionekana ni mtu mwenye akili zake timamu wala si kichaa kama walivyomfikiria.
Baada ya kutulia, walimuuliza maswali kutaka kujua ametoka wapi na amefikaje pale.
“Unaitwa nani?”
“Sara.”
“Umetokea wapi?”
“Dar es salaam.”
“Umefikaje huku?”
“Kwani huku wapi?” aliuliza huku akipepesa macho kuishangaa sehemu ile ambayo ilikuwa ngeni kwake.
“Hapa ni Kongwa njia ielekeayo Mpwapwa.”
“Kongwa si Dodoma?” Sara alishtuka.
“Ndiyo.”
“Waongo!” Sara alibisha haku haamini kufika Dodoma kwa kutembea usiku mmoja tena kwa miguu.
“Dada kwani sehemu hii unaijua?”
“Mmh! Hapana.”
“Duh! Uliondoka kwako lini?”
“Jana usiku?”
“Mmh! Upo sawa kiakili?” mmoja alimshangaa majibu ya Sara.
“Na wala sijawahi kuugua ugonjwa wa akili.”
“Basi hapa ni Kongwa.”
“Mungu wangu, nimefikaje huku?” Sara alishtuka huku macho yakimtoka pima.
“Kwani ilikuwaje?”
Sara aliwaeleza jinsi alivyopotea baada ya kutoka kwake kuelekea kwenye banda la chipsi kununua chakula cha usiku na kujikuta akipotea njia na kushangaa kujiona yupo katikati ya pori na kutembea bila kufika mpaka alipofika chini ya mti ule alfajiri, akiwa amechoka sana na kuamua kupumzika kwa vile hakujua anapoelekea.
“Haiwezekani utoke Dar kwa miguu jana usiku ufike Dodoma alfajiri!” mtu mmoja alipingana na maelezo ya Sara.
“Basi hapa ni Kongwa mkoa wa Dodoma ndiyo maana tuna wasiwasi na maelezo yako huenda akili yako haipo sawa.”
“Akili yangu iko sawa, kwani leo ni siku gani?” aliuliza baada ya kumuona watu wakipita kuelekea kanisani.
“Jumapili.”
“Mungu wangu! Haiwezekani nitoke nyumbani Jumatatu mpaka leo Jumapili, haiwezekani nitembee kwa miguu wiki nzima, nimewakosea nini kunitesa hivi,” Sara alilalamika huku akitokwa machozi.
“Kina nani?”
“Hata najua, Mungu atanilipia.”
Sara alianza kulia na kuwafanya wasamaria wema kumbembeleza, baada ya kunyamaza. Aliwaomba msaada wa kumrudisha Dar kwa vile muda ulikuwa umekwenda, walimpa hifadhi ya kulala pale ili siku ya pili alfajiri wampandishe basi mpaka njia panda kisha apande basi kurudi Dar.
Usiku kucha hakulala kuwaza yaliyomtokea, kwake hakuamini, aliamini tukio lile ni la ndotoni halina ukweli wowote. Siku ya pili aliamshwa alfajiri na wenyeji wake na kupandishwa mabasi yanayokwenda njia panda ili apande yanayokwenda Dar es Salaam.
Baada ya kupanda haisi iliyompeleka njia panda ambapo alipanda basi la Shabib na kutulia kwenye siti, basi likiwa linakwenda aliangalia mapori ya njiani ambayo yalimfahamisha yupo safarini lakini bado hakuamini njia nzima alikuwa akijiuliza nini kilichomfanya afike mkoani Dodoma kwa miguu bila kuchoka wala kudhurika na wanyama wakali.
Pamoja na kuamini yumo ndani ya basi, bado hakuamini tukio lililomtokea ni la kweli. Kwake aliamini ile ni ndoto iliyomchanganya na akiamka asubuhi atajikuta yupo kitandani amelala. Basi lilingia Dar majira ya saa sita na nusu mchana, bado Sara hakuamini. Aliteremka kwenye basi baada ya abiria kuanza kuteremka.

Itaendelea

#LIKE PAGE USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HII NAOMBEN  SHARE ZIWE MING NIPOST KIPANDE KINGNE COZ VIEWZ 50000 ILA SHARE NI CHACHE SANA PAMOJA NA LIKE EBU NIPE MOYO WAKUPOST VIPANDE VINGNE LEO KWA KUSHARE NA KULIKE PAGE HIIII

0 comments:

Post a Comment