Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-28-
#SHARE HADITHI HII NIPOST MWENDELEZO WAK #LIKE PAGE #COMMENT CHOCHOTE
ILIPOISHIA:
Pamoja na kuamini alikuwa ndani ya basi, bado hakuamini kama tukio lililomtokea lilikuwa la kweli. Kwake aliamini ile ni ndoto iliyomchanganya na akiamka asubuhi atajikuta yupo kitandani amelala. Basi liliwasili jijini Dar majira ya saa sita na nusu mchana, bado Sara hakuamini ndipo aliteremka.
SASA ENDELEA...
Baada ya kuteremka aliangalia pesa yake ya nauli aliyokuwa amefunga kwenye khanga chakavu.
Alifungua na kuikuta elfu moja iliyochafuka kwa udongo wa kijijini, chini alikuwa amevaa ndala rangi mbili moja nyekundu na nyingine bluu. Nywele zake zilikuwa timutimu.
Sara alionekana kweli mwana kijiji kutokana na jinsi alivyokuwa, muda wote hakujiona kwani kama angejijua alivyo asingeweza hata kutembea kutokana na jinsi anavyojipenda. Hata alipotaka kupanda daladala konda alimuona wa kuja na kumsemesha maneno ya kejeri.
Sara hakujali aliingia ndani ya daladala hadi Kinondoni Kanisani anapokaa. Baada ya daladala kusimama aliteremka na kuelekea kwake. Alipokaribia alishangaa kuona mlango wa chumba chake ukiwa wazi. Shoga yake Happy aliyekuwa amekaa nje alikuwa wa kwanza kumuona na kushtuka kufuatia rafiki yake huyo kuwa katika mavazi ya ajabu, gauni lililochanika mabegani khanga iliyopauka na kandambili rangi mbili.
"Sara!" Happy alimwita kwa sauti ya juu.
Sauti ile ilikuwa kama kitu kilichomzindua toka usingizini na kujikuta naye akijishangaa.
"Shoga ulikuwa wapi? Jamani mbona umevaa nguo za ajabu?"
Kauli ile ilimfanya ajichunguze na kujikuta akijishangaa mavazi aliyovaa na kujikuta akiangua kilio huku akisema.
"Mungu wangu! Kumbe kweli nilidhani ndoto."
"Kumbe kweli nini jamani?" Happy alitaka kujua.
Sara hakusema kitu alikimbilia ndani na kujitupa kitandani na kuanza kulia kilio cha sauti na kuwafanya majirani wakusanyike nje ya chumba chake. Happy ndiye aliyeingia ndani kutaka kujua shoga yake alikumbana na nini, kitu kilichofanya atoweke nyumbani kwa wiki nzima na kurudi akiwa kama mwana kijiji.
"Sara umepatwa na nini?" Happy alitaka kujua.
"Mmh! Hata simamini nitembee usiku kucha mchana kutwa kwa siku sita bila kupumzika mpaka Dodoma?"
"Dodoma?" Happy alishtuka.
"Ndiyo dada hata siamini hizi nguo nimepewa na wasamaria wema wa Kongwa walioniokota nikiwa nimelala barabarani."
"Wewee!" Sara alishtuka.
"Yaani kama nisingepanda Hiace toka Kongwa kisha basi la Shabiby ningebisha na tiketi yake ni hii," Sara alimuonesha Happy tiketi ya basi ambayo ilionesha ilikuwa ya siku ile.
Baada ya Sara kuisoma akili yake bado haikuamini shoga yake kwenda Dodoma kwa miguu aliona kama mchezo wa kuingiza.
"Sara, siku ile si ulisema unakwenda kununua nyama ya nguruwe na ndizi?"
"Ndiyo shoga yangu, nimetoka vizuri mpaka karibu kwa Macha Kitimoto. Ghafla nilijishangaa kujikuta katikati ya pori hata sijui ni pori gani."
"Wewee!" Happy alizidi kushtuka.
"Yaani niliogopa mpaka haja ndogo ikanitoka, kibaya zaidi nyuma yangu kulikuwa na milio ya ajabu ya kutisha na kunifanya nikimbie kwenda mbele japosikujua ni wapi nilipokuwa nakimbilia. Kila nilivyokuwa nikikimbia ndivyo sauti za kutisha zilivyokuwa zikinisogelea na kunifanya nizidi kukimbia.
"Nakumbuka upande wa khanga wa juu ulinidondoka lakini sikuujali zaidi ya kuyaokoa maisha yangu ambayo niliyaona yapo hatarini. Kandambili nilizokuwa nimevaa zilinidondoka na kujikuta nakimbia pekupeku huku nikikatiza kwenye vichaka na kukanyaga miba.
"Kutokana na kutokewa na vitu vile vya kutisha ambavyo sikudhania kukutana navyo hata siku moja, nilijua ile ni ndoto tu wala si kweli. Baada ya kukimbia kwa muda mrefu bila kupumzika, nilianza kusikia vichomi kwenye mbavu na kunifanya nishindwe kutembea.
"Zile sauti za kutisha zilizidi kunisogelea nikaona kama nitazubaa basi nitakufa. Nilijilazimisha kukimbia huku nimeshika mkono kwenye mbavu. Nilikwenda hivyo kwa kuchechemea mpaka nilipotokea kwenye mti mkubwa.
Je, nini kitatokea?#LIKE PAGE Fuatilia KIPANDE KINACHOENDELEA
0 comments:
Post a Comment