MIMBA YA JINI -26

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-26-

LIKE PAGE HIII USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA SHARE STORY NIPOST NYINGINE

ILIPOISHIA:
Kwa vile alielezwa na Shehna kilichotokea na nini ajibu alimwambia mkewe.
"Kwa akili ya kawaida kitu hicho kinaweza kufanyika?"
"Hata mi nashangaa, lakini nakumbuka niliamka na kukaa kabisa."
SASA ENDELEA...

"Baada ya kukaa nini kiliendelea?"
"Sikumbuki zaidi ya kushtuka alfajiri na kujikuta nimelala."
"Sasa wasiwasi wako nini?"
"Ndipo hapo ninapo changanyikiwa kilikuwa nini."
"Hebu achana na ndoto, hivi kweli nilete mwanamke ndani na kufanya naye mapenzi kitanda tunacholala, imeanza lini?" Mustafa alizidi kujifanya kumshangaa mkewe.
"Hata mi namshangaa."
"Hebu achana na ndoto za kijinga."
"Basi samahani mume wangu kama nimekukwaza."
"Walaa, una haki ya kuniuliza chochote."
Wakiwa katikati ya mazungumzo simu ya Mustafa iliita, alipoangalia ilionesha inatokwa kwa Shehna. Aliipokea na kuzungumza naye.
"Haloo."
"Haloo, asalam aleykum."
"Waleykum salam."
"Vipi mmeamkaje?"
"Mmh! Salama."
"Kweli?" Shehna aliuliza.
"Kweli."
"Mbona kama mkeo ana tatizo?"
"Sijui ameota nini."
"Ameota nini?" Shehna alijifanya kushtuka.
"Sijui ameniona eti mimi nina fa...fa.."
"Hebu mpe mwenyewe azungumze, acha kung'ata maneno," Shehna alimkata kauli Mustafa.
Mustafa alimpa simu mkewe aliyekuwa bado amesimama pembeni ya kitanda. Husna aliipokea na kuzungumza.
"Asalam aleykum."
"Waleykum salam, eti mpenzi kuna nini?" Shehna alimuuliza kwa sauti ya upole.
Husna alimweleza kama alivyomweleza mumewe kilichotokea usiku. Baada ya kumsikia alisema:
"Mpenzi hizo ni ndoto ambazo huvunja ndoa nyingi kwa vile mtu huota ukiwa macho na kuweza kuamini ni jambo la kweli. Hizo ni ndoto tu, lakini mumeo akirudi kazini atakupatia dawa ya kujipaka wakati wa kulala haitakutokea tena."
"Nitashukuru kwa kweli ilinishtua sana."
"Pole mpenzi."
"Asante dada yangu, jamani nina hamu ya kukuona tutaonana lini?"
" Utaniona tu usiwe na wasiwasi hata mimi nina hamu na wewe, unasema uliyemuota akifanya mapenzi na mumeo uliiona sura yake?"
"Ndiyo."
"Kwa mfano akutokee mbele utamjua?"
"Nitamjua nilimuona vizuri sana japo nilikuwa naota."
"Basi mpenzi nikimaliza mizunguko yangu nitakuja utanichoka mwenyewe."
"Walaa labda unichoke wewe."
"Basi mpenzi usiendekeze ndoto."
"Nimekuelewa."
Shehna alimalizia kuzungumza na Husna na kumalizia kuzungumza na Mustafa kisha alikata simu. Mazungumzo yake yalirudisha imani moyoni kwa Husna na kuamini aliyosema Shehna yalikuwa na ukweli mkubwa. Baada ya moyo wake kuamini ile ilikuwa ndoto, alimtayarishia mumewe maji ya kuoga na kifungua kinywa huku moyo wake ukiwa mweupe.
Mustafa baada ya kufungua kinywa alimuaga mkewe na kuelekea kazini, kama kawaida alikuta ofisi imesafishwa. Akiwa ofisini Shehna alimtokea kabla hajaanza kazi na kuzungumza naye sakata la usiku.
"Mustafa nilitaka kukulaumu lakini umenilahisishia kazi, yale mafuta niliyokupa kumpaka mkeo mpe ajipake mwenyewe. Hakikisha unamkumbusha kujipaka kabla hajalala, itatusaidia kumteka bila kujijua."
"Yaani nashukuru sana sijui bila wewe ingekuwaje?"
"Ungekataa tu, lakini lazima angeuliza kwa watu na kutaka kuchimba na kuujua ukweli."
"Unafikiri angeujua ingekuaje?"
"Mmh! Tungejua tifanyeje japo ingetusumbua kidogo."
"Nashukuru sana mpenzi umenisaidia."
"Basi nikuache ufanye kazi."
"Nashukuru."
Shehna aliaga na kuondoka na kumuacha Mustafa akijiandaa kuanza kazi ya siku ile.

Itaendelea tena inshallah.

LIKE PAGE HIII USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA SHARE STORY NIPOST NYINGINE

0 comments:

Post a Comment