MIMBA YA JINI -25

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-25-

LIKE PAGE HIII USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA SHARE STORY NIPOST NYINGINE

ILIPOISHIA:
Kwa vile mke wa Mustafa hakupakwa mafuta ya kumlaza, sauti ya kulalamika kimapenzi ilimshtua usingizini.
SASA ENDELEA...

Alipoangalia pembeni yake alimuona mumewe akifanya mapenzi na mwanamke mzuri wa Kiarabu, wote walikuwa katikati ya tendo. Alitulia kwa muda na kujiuliza alichokiona ni kweli au anaota.
Alikaa kitako na kupekecha macho yake kama kweli amelala au yupo macho, akili yake ilimweleza hakulala bali yupo macho na anachokiona ni kitu cha kweli wala si cha ndotoni.
Alijiuliza yule ni mwanamke gani asiye na woga aliyeingia ndani mwake bila hofu, alijiuliza tabia ile ya mumewe kuingia na mwanamke ndani na kufanya naye mapenzi kitanda wanacholala bila woga, imeanza lini?
Wakati akiwaza vile, Shehna alishtuka baada ya akili yake kutambua mke wa Mustafa ameamka na kuangalia kilichokuwa kikiendelea pembeni yake.
Alijibadili ghafla na kutoweka kitandani na kumuacha Mustafa akilalamika kwa kumwita jina lake.
“Shehna mpenzi unaenda wapi?”
Shehna hakujibu, alisogea pembeni ya mke wa Mustafa na kumpuliza usoni, usingizi mzito ulimchukua Husna na kurudi kitandani kulala.
Baada ya kulala, Shehna alimuuliza Mustafa aliyekuwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea.
“Mustafa umefanya nini?”
“Kuhusu nini mpenzi?”
“Kwa nini hukumpaka mafuta mkeo?”
“Nilimpaka.”
“Muongo! Tutamwambia nini mkeo ikiwa ameona kila kitu?”
“Kwani aliamka?”
“Ameamka na ameona kila kitu.”
“Mungu wangu!” Mustafa alishika mikono kichwani.
“Basi mi naondoka na hutaniona tena katika maisha yako,” Shehna alisema kwa hasira huku akielekea alipoweka nguo zake.
“Usifanye hivyo mpenzi, nakuhitaji kuliko kitu chochote, inawezekana uchovu ulisababisha nipitiwe. Naomba unisamehe sana.”
“Mustafa nakupenda sana, lakini masharti yangu ya kuendelea kuwa na wewe yatakuwa magumu sana kuliko mwanzo na nina imani utayashindwa.”
“Nakuahidi kuyatekeleza yote.”
“Kweli?”
“Kweli kabisa.”
“Unajua nakupenda?”
“Tena sana.”
“Kesho mkeo lazima atakuuliza kuhusiana na alichokiona usiku huu kwa vile aliendelea na usingizi atataka ukweli kutoka kwako. Wewe kataa kwa vile hana uhakika kwa kile alichokiona kama ni kweli au ndoto.”
“Sawa nitafanya hivyo.”
“Kwa vile amelala tuendelee na dozi ya mwisho lakini kuanzia kesho tunabadili mfumo.”
“Sawa mpenzi nipo radhi kwa lolote.”
Walikwenda kuoga na kurudi kumalizia dozi ya mwisho kisha Shehna aliondoka na kumuacha Mustafa usingizini.
***
Husna alikuwa wa kwanza kuamka mumewe alikuwa bado amelala, alimuangalia na kujikuta akivuta kumbukumbu ya usiku na kujiuliza alichokiona usiku kilikuwa kweli au ndoto kwa vile toka aolewe na Mustafa, hakuwahi kutokewa na tukio kama lile kwa sababu alimuamini sana mumewe kwa uaminifu wa ndoa yao kwa kipindi chote pamoja na matatizo yote, hakuwahi kumdharau wala kumsaliti.
Kwa akili ya kawaida aliamini kabisa aliamka usiku na kukuta mumewe akifanya mapenzi na mwanamke wa kiarabu. Lakini kilichomshtua mbona ameamka asubuhi kutoka usingizini?
Kila lililokuja mbele yake lilimchanganya, ili apate jibu la kitendawili chake aliamua kumuamsha mumewe. Baada ya kumtikisa kwa muda huku akimwita kwa jina lake, Mustafa alishtuka usingizini na kumgeukia mkewe.
“Vipi?” alimuuliza huku akilazimisha macho kufumbuka.
“Mume wangu hebu amka.”
“Kuna nini?”
“Si uamke,” Husna alisema kwa sauti kali kidogo.
Mustafa aliamka na kukaa kitako ili amsikilize mkewe.
“Mume wangu,” alianza kwa kumwita.
“Naam.”
“Kuna kitu kimetokea sijui ni kweli au ndoto.”
“Kitu! Kitu gani?” Mustafa alijifanya kushtuka.
“Kuna kitu nimekiona usiku, kimenichanganya sana.”
“Kitu gani?” Mustafa alimuuliza huku akifikisha macho yake na kupiga miayo ya uchovu wa kulala.
Husna alimweleza mumewe kila kitu alichokiona ambacho yeye aliamini haikuwa ndoto. Kwa vile alielezwa na Shehna kilichotokea na nini ajibu, alimwambia mkewe.
“Kwa akili ya kawaida kitu hicho kinaweza kufanyika?”
“Hata mi nashangaa, lakini nakumbuka niliamka na kukaa kabisa.”

Je, nini kitafuatia hapo? Fuatilia baadae basi

LIKE PAGE HIII MWENDELEZO WA HADITHI HII USIKUPITE jion napost nyingnee

0 comments:

Post a Comment