Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-23-
ENDELEA KUONYESHA UPENDO KUWA KARIBU NAMI KIPANDE HATA KIMOJA KISIKUPITE LIKE PAGE HII TWENDE SAWA
ILIPOISHIA JANA :
Alifungua na kuingia ndani ambako ilikuwa ofisi imejaa vumbi na uchafu kutokana na kutofanyiwa usafi.
SASA ENDELEA…
Alijiuliza Sara amepatwa na nini mpaka muda ule hajafika ofisini, aliingia ofisini na kuweka vitu vyake kisha alitoa simu na kumpigia, simu iliyopokelewa na mwanamke upande wa pili.
“Haloo.”
“Haloo, nazungumza na nani?”
“Maria.”
“Sara yupo wapi?”
“Alitoka jana kufuata chakula lakini ajabu mpaka kunakucha hatujamuona.”
“Sasa kaenda wapi?”
“Hata sisi tunashangaa kibaya hata simu hakuchukua.”
“Mmh! Sawa.”
Mustafa alikata simu na kujikuta akichoka na kukaa kwenye kochi lake huku akijawa na mawazo ya kujiuliza Sara atakuwa amekwenda wapi. Akiwa katikati ya mawazo alisikia mlango wa ofisi ukigongwa alijua Sara ndiyo anafika.
“Ingia,” alisema kwa sauti.
Mlango ulifunguliwa na kutanguliwa na harufu nzuri ya manukato aliyoyazoea ya Shehna, mara aliingia shehna katika vazi la gauni refu la kitambaa cha kitenge na kiremba chake alionekana mwanamke mzuri kuliko siku zilizopita.
Mustafa kuzungumza alishindwa alibaki kamtumbulia macho kama siku yake ya kwanza kumuona.
“Mustafa kushangaa gani huko kama ndiyo leo siku yako ya kwanza kuniona?” alimuuliza huku akimsogelea alipokuwa amekaa.
“Shehna lazima nimsifu Mungu kwa utundu aliofanya kukuumba, Shehna wewe ni mwanamke mzuri wa wazuri, uzuri wako kama nyoka anayejibadili mwili wake, kila siku uzuri wako unaongezeka, wa leo unashinda wa jana pia naamini wa kesho utauzidi wa leo.”
“Mmh! Kawaida sema bado hutatuliza macho kwangu unaniangalia kwa wasiwasi, kama ungekuwa hunitazami kwa wasiwasi wala usingenishangaa. Nilichokibadili asubuhi hii ni nguo tu, mimi ni yuleyule wa jana wa leo na kesho vilevile.”
“Wewe unaweza kusema hivyo, najuta kuchelewa kukujua mapema.”
“Ulinifahamu mapema lakini hukunitilia maanani, nilikuja kwako kila wakati lakini labda uliniona mwanamke malaya.”
“Ha..ha..pana, sijakufikiria hivyo!”
“Sasa tatizo lako nini?”
“Nina wasiwasi wenye fedha zaidi yangu wataninyang’anya.”
“Kwani nipo wapi siku zote wasikunyang’anye wakunyanganye leo?” Shehna alimuuliza huku akimuangalia jicho tata lililozidi kumchanganya Mustafa na kutamani heri angekuwa mkewe wa ndoa. Lakini bado aliona maisha ya Shehna asingeyaweza kwani kila alipokutana naye alikuwa na nguo na vito vya thamani ambavyo aliamini hawezi kuvinunua.
Shehna aligundua alichokuwa akikiwaza Mustafa baada ya kukaa kimya kwa muda. Alimshtua kwa kumwita jina lake.
“Mustafa.”
“Naam.”
“Kwa nini unajibebesha mawazo mazito ambayo sivyo unavyonifikiria?”
“Umejuaje?’
“Si kujuaje, bali nataka kukuthibitishia maisha yangu na wewe ni tofauti unavyonifikiria, kila kitu juu ya mustakabali wetu niachie mimi.”
“Sawa nimekuelewa.”
“Na..na mbona ofisi chafu?”
“Nashangaa mpaka muda huu msaidizi wangu sijamuona, ha..halafu nasikia toka jana usiku hajarudi.”
Kauli ile ilimfanya Shehna acheke kicheko cha umbea kilichomfanya Mustafa ashtuke na kuhoji.
“Vipi mbona unacheka kama unajua kinachoendelea.”
“Walaa, nimecheka tu.”
“Yaani hapa nimechanganyikiwa ngoja nimwite mlinzi ufanye usafi.”
“Walaa, kazi hiyo nitaifanya miye.”
“Hapana Shehna, acha ataifanya mlinzi.”
“Kwani mimi kufanya kuna nini?”
“Utajichafua bure wakati watu wa kuifanya kazi hii wapo.”
“Basi leo nitaifanya mimi, naomba unipishe mara moja.”
“Sawa, basi nipo nje kwa mlinzi.”
“Hakuna tatizo.”
Mustafa alitoka nje na kumuacha Shehna ofisini, kabla ya kufanya kitu aliangua kicheko cha mfululizo kufurahia alichomfanyia Sara mwanamke aliyemuona asidi aliyetaka kushindana naye. Kisha alijishika kwenye paji la uso na kutulia kwa muda, mara vijakazi na watwana toka ujinini walipiga magoti mbele yake na kumuuliza.
“Mwana wa Mfalme wa jini la bahari ya dhahabu una shida gani unayotaka tukufanyie?”
“Nataka baada ya muda mfupi ofisi yote uwe safi kuliko siku zote.”
“Hewala mwana wa mfalme.”
Vijakazi na watwana waliingia katika kazi ya usafi iliyochukua dakika tano kila kitu kilikuwa safi ndani. Kilibadilishwa kila kitu na kuwekwa pazia nzuri la halili na kuifanya ofisi ipendeze mara dufu. Baada ya kufanya usafi walipiga magoti mbele ya Shehna na kusema....
Itaendelea ENDELEA KUSHARE HADITHI HII YAKUSISIMUA NIPOST KIPANDE KUNACHOENDELEAAA
0 comments:
Post a Comment