Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-22-
#LIKE_PAGE MWENDELEZO WA HADITHI HII USIKUPITE #SHARE NIPOST NYINGINE
ILIPOISHIA JANA:
“Asalam aleiykhum.”
“Waaleiykhum Msaalam, mmeamkaje?”
“Salama.”
“Mbona hujatoka kwenda kazini?”
“Si huyu mshe…”
SASA ENDELEA…“
Weee! Mustafa unataka kusema nini, usithubutu tena kumwita mkeo mshenzi, tatizo nini?” sauti ya Shehna ilikuwa kali kidogo iliyomkata kauli.
“Si..si..,” aliingiwa na kigugumizi.
“Mustafa nakuamini kwa nini unataka kuharibu mambo, tatizo la mkeo umeishalijua ulitakiwa uzungumze naye kwa sauti ya upole kuliko kuzungumza kama mhuni.”
“Samahani nilipandwa na jazba.”
“Mpe simu mkeo.”
Mustafa alimpa simu mkewe aliyekuwa akitokwa na machozi huku akiamini ndoa yake imekalia kuti kavu baada ya siri zake kuwa nje kutokana na kiburi chake cha kutofuata masharti ya kupata mtoto wakati mumewe alikuwa amepoteza fedha nyingi. Alipokea simu katika sauti ya kilio, huku akiwa na donge moyoni baada ya kujua yule ndiye mbaya wake hata akiachika yule ndiye mchawi wake.
“Haloo.”
“Haloo, asalam aleiykhum.”
“Waleiykhum msaalam.”
“Vipi mbona unalia?”
“Ha..ha..pana.”
“Ni hivi yaliyopita yamepita, kama kweli unataka mtoto acha mambo ya kijinga, kuchanganya dawa za uzazi utakuwa mgumba. Wa kulia ningekuwa mimi kwa vile gharama ya dawa niliyowapa ni kubwa zaidi ya kununua gari la kifahari, lakini mwisho wa yote ukafanya kiburi chako ambacho kuna siku kutakuharibia maisha yako.
“Sasa nasema hivi kuanzia leo nitakupa dawa ya kuoga na kujipaka kwa mwezi mzima bila kukutana na mumeo. Baada ya mwezi ruksa kukutana na mumeo, sasa upo tayari nikuletee hiyo dawa?”
“Ndi..ndiyo.”
“Usiseme kutufurahisha, litoke moyoni lisije la kutokea ukasema sijakuambia, najua moyoni mwako unaniona adui. Lakini napigania ndoa yako la sivyo siku zako zilikuwa zikihesabika… Unazungumza vizuri na familia ya mumeo kama zamani?”
“Hapana.”
“Unajua kwa nini?”
“Sababu ya kuchelewa kupata mtoto.”
“Sasa kwa nini unafanya mchezo wa kitoto.”
“Hata sijui, labda nimerogwa.”
“Hujarogwa na mtu bali kiburi chako, kama utaendelea nacho nyumba utaiacha bado unaipenda. Wa kukutoa ndani ni ndugu wa mumeo, nakuibia siri kuna msichana ametafutwa kuja kukutoa ndani, hivyo sasa kazi kwako kufuata masharti ili ubakie katika nyumba yako au vinginevyo.”
“Sasa kwa mwezi huo hawatakuja kunitoa ndani?” Husna aliingiwa na uoga.
“Hawawezi, we nisikilize mimi kila kitu kitakwenda vizuri.”
“Ninakusikiliza dada yangu.”
“Ukifanya hivyo utanifurahisha, nakuahidi kukupa zawadi kubwa sana maishani kwako.”
“Nakuahidi dada yangu kukufurahisha, nitayafanya yote utakayoniambia.”
“Utakuwa umefanya jambo zuri, haya mpe simu mumeo.”
Husna alichukua siku na kumpa mumewe aliyekuwa bado amesimama koti na mkoba wake vikiwa mkononi. Mustafa aliipokea simu.
“Haloo.”
“Nina imani kila kitu tumemaliza, sasa sitaki ufikie alipotaka kufikia kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.”
“Nashukuru, kama amekuelewa mi sina tatizo.”
“Haya baba wahi kazini.”
“Nashukuru.”
Mustafa alikata simu na kumgeukia mkewe na kumweleza.
“Nina imani mmemalizana naye.”
“Ndiyo mume wangu, nisamehe kwa yote.”
“Yote yameisha tumefungua ukurasa upya.”
“Asante mume wangu.”
Walikumbatiana kisha Husna alimpokea mumewe alivyobeba na kumsindikiza mpaka kwenye gari.
Kabla ya kuingia walikumbatiana na kubusiana kisha Mustafa aliingia ndani ya gari na kuondoka kuwahi kazini. Alikwenda moja kwa moja mpaka ofisini, alishangaa kuikuta ofisi haijafunguliwa, kwa vile tangu siku Sara alipochelewa ofisini ufunguo mmoja alikuwa akiondoka nao mwenyewe.
Alifungua na kuingia ndani ambako alikuta ofisi imejaa vumbi na uchafu kutokana na kutofanyiwa usafi.
Itaendelea
W LIKE_PAGE MWENDELEZO WA HADITHI HUU USIKUPITE #SHARE NIPOST NYINGINE
0 comments:
Post a Comment