MIMBA YA JINI 21

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-21-

#LIKE PAGE HII USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA SORRY KWA UKIMYA ULIOTOKEA SIKU ZILIZOPITA ILA KAMA KAWAIDA TUNAENDELEA NA STORY YETU ILI UWE KARIBU NA MIMI #LIKE PAGE #SHARE STORY NIPOST NYINGNEEEE

ILIPOISHIA :
"Shoga vipi mbona hivyo?"
Sara hakumjibu alichukua kitambaa na kujifuta machozi, hali ile ilimfanya shoga yake awaze labda amefiwa.
SASA ENDELEA…

"Shoga una msiba?"
Alitikisa kichwa kukataa.
"Sasa nini?"
"Naomba kwanza maji," Sara alisema kwa sauti ya kukwaruza.
Shoga yake alikwenda kwenye friji na kuchukua maji kwenye jagi na kumuwekea kwenye glasi. Baada ya kunywa maji kwa mkupuo yaliyopunguza hasira, alishusha pumzi ndefu na kusema.
"Shoga kuna tukio moja leo linimeniudhi sana."
"Tukio gani?"
Sara alimweleza kilichomtokea na kutaka kufukuzwa kazi pamoja na matukio yote yaliyomtokea. Shoga yake alishtuka sana.
"Sara unayosema ni kweli?"
"Kweli kabisa, matukio ya yule mwanamke nina wasiwasi nayo, huenda yule ni jini si mwanamke wa kawaida."
"Mmh! Huenda kweli, lakini si nasikia majini wana kwato kwa chini, uliziona?"
"Yule ni mwanadamu wa kawaida lakini muonekano wake si wa kawaida hata manukato yake sijawahi kuyasikia sehemu yoyote!"
"Mmh! Mungu wangu kama ni jini unafikiri itakuwaje?"
"Dawa yake naijua, nakuapia kama ni jini atakimbia mwenyewe kuna vitu nitakwenda navyo kazini."
"Vitu gani?"
"Mifupa ya nguruwe au nyama yake, kama ni jini hawezi kuja tena ofisini na nitamwambia bosi kama yule si mtu ni jini."
"Basi fanya hivyo."
"Tena shoga nimejikuta nina hamu ya kiti moto, nakwenda kumchukua ili nimlie nyumbani."
"Unachukua kiasi gani?"
"Nusu na ndizi nne nikipiga na bia zangu mbili nalala vizuri."
"Shoga nunua kilo moja maana hata mimi nina hamu nayo sana."
"Poa nitakuchulia na ndizi mbili."
"Hakuna tatizo."
"Yaani kidogo kuzungumza na wewe hasira zimepungua, nakuapia nitamkomesha."
"Kwa kufanya hivyo, utamuweza."
Sara alijitapa huku akivua viatu kisha alibadili nguo na kuelekea bafuni kuoga.
Alipanga akitoka kuoga aende kwenye baa ya Macha iliyokuwa ikiuza kitimoto ili akatimize adhima yake ili ajue kama Shehna ni jini au mtu.
Alioga harakaharaka, alipotoka kuoga alijifuta maji na kujifunga upande wa khanga moja chini na nyingine alijitanda kwa juu. Alichukua noti ya elfu kumi na kutoka kuelekea kwenye baa hiyo.
***
Mustafa aliposhtuka usingizini alijishangaa kujikuta kitandani na mkewe lakini Shehna hakuwepo. Alipoangalia saa ya ukutani ilimuonesha ni saa kumi na moja kasoro alfajiri. Wasiwasi wake ulikuwa labda ameamka na kwenda bafuni kuoga kabla ya kuondoka.
Aliamka haraka kitandani huku akimtazama mkewe asiamke muda ule kabla hajajua Shehna yupo wapi. Alikwenda hadi bafuni lakini hakumkuta mtu akatazama msalani pia hakukuwa na mtu. Alikwenda mlangoni na kukuta umerudishiwa, alijua ameshatoka.
Kwa vile muda ulikuwa bado alirudi kitandani, alipojilaza usingizi ulimchukua mpaka aliposhtuliwa na mkewe kukiwa kumekucha. Alipofumbua macho kulikuwa kumekucha alinyanyuka kuelekea bafuni kuoga, alipotoka kuoga alikuta mkewe ameshamuandalia kifungua kinywa.
Baada ya kufungua kinywa, alimshukuru mkewe kwa kumbusu shavuni na kutaka kuelekea nje lakini mkewe alikumbuka kitu na kumuuliza.
"Mume wangu umefikia wapi?"
"Kuhusu nini?"
"Kuhusu Shehna, bado hujawasiliana naye?"
"Alinipigia na kumueleza, alisema kiburi kimejaa na dharau ndicho chanzo cha kuharibikiwa mambo yako ameapa kama utaendelea na tabia zako chafu utakufa bila mtoto."
"Muongo amejuaje mimi nina tabia chafu?"
Alimweleza kila alichoelezwa na Shehna kilichosababisha ashindwe kushika ujauzito, Husna alichanganyikiwa siri zake zote kuwa nje na kujikuta akitaka kumjua Shehna ni nani, alijiuliza ni kiumbe gani anayejua mambo yake ya siri kiundani ambayo hakuna mtu mwingine aliyekuwa akiyajua. Akiwa bado yupo katika dimbwi la mawazo, Mustafa alimuuliza.
"Lipi la uongo katika niliyokuambia?"
"Mmh! Shehna kiboko, kayajuaje haya?"
"Si kujua kwa nini anajua mambo yako, la muhimu kujua kwa nini natumia fedha na nguvu wakati mwenzangu huna ushirikiano?" Mustafa alizitoa hasira zake kwa mkewe baada ya kuonesha hakuwa na ushirikiano katika kutafuta mtoto.
"La..lakini mume wangu unamuamini vipi Shehna, yule ni mgombanishi tu," Husna alijitetea.
Mara simu ya Mustafa iliita alipoangalia aliiona inatoka kwa Shehna, aliipokea.
"Asalam aleykum."
"Waleykum Salamu, mmeamkaje?"
"Salama."
"Mbona hujatoka kwenda kazini?"
"Si huyu mshe

Itaendelea

#LIKE PAGE UNGANA NAMI KWENYE STORY HII YAKUSISIMUA DONDOSHA #LIKE #SHARE #NA COMMENT CHOCHOTE KUHUS STORY HIII KIPI KIONGEZEKEEE KATKA EPISOD ZINAZOFATAAA

0 comments:

Post a Comment