MIMBA YA JINI -20

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-20-

Mtunzi: #Mzizi_Mkavu

#LIKE_PAGE USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HII YAKUSISIMUA #SHARE NIPOST KIPANDE KINACHOENDELEA.

ILIPOISHIA JANA USIKU:
Mustafa baada ya kumtafuta Shehna kwa kuzunguka nyumba bila kumuona, alisogea mpaka

mbele ya nyumba labda yupo barabarani lakini hakumuona. Baada ya kutomuona alisimama kwa

muda kujiuliza atafanyaje ikiwa muda umekwenda na lazima akapande kitandani na ilikuwa lazima

ampe mkewe haki yake ya ndoa kwa vile hakuwa na sababu ya kumnyima.
SASA ENDELEA…

Aliamua kurudi ndani akiwa amejikatia tamaa ya kutimiza masharti ya Shehna, alipofika sebuleni alishangaa kukuta hakuna mtu. Alijua labda amekwenda msalani, alibeba Laptop yake na kuingia chumbani, alishangaa kumkuta mkewe chumbani amelala hajitambui.
Alishtuka usingizi wa dakika tano kumkuta mkewe amelala kama mtu aliyelala saa mbili zilizopita wakati anatoka alikuwa macho makavu. Hakuamini, aliona kama anamtania au alifanya vile ili kumtega. Alisogelea kitandani na kumwita mkewe kwa sauti lakini alionesha ana usingizi mwingi hata alivyomgeuza alionesha kweli amelala.
Hakuamini zoezi lake kufanikiwa akiwa amekata tamaa kwa vile naye alikuwa na usingizi. Alichukua chupa ya manukato aliyopewa na Shehna, alikwenda bafuni kuoga na kujipaka nanukato yale.
Kabla ya kupanda kitandani alihakikisha mlango amerudisha bila kufungwa, kisha alipanda kitandani na chupa yake ya manukato. Kwa vile mkewe alikuwa ameisha lala alimsogeza ukutani na yeye kulala katikati. Alifuata maelekezo ya kutolala na nguo ya ndani, alitoa nguo zote na kupanda kitandani akiwa mtupu. Alichukua mafuta kidogo na kumpaka kichwani mkewe ambaye alikuwa katikati ya usingizi mzito.
Naye alijilaza pembeni ya mkewe, haikuchukua muda usingizi ulimpitia. Katikati ya usiku aliamshwa kwa kubembelezwa, alipofumbua macho alimuona Shehna amesimama pembeni ya kitanda akiwa amejifunga mtandio mwepesi ulioonesha mwili wake mzuri uliokuwa hauna kitu ndani.
"Shehna," Mustafa alishtuka na kutaka kuongea kwa sauti.
"Shiiii!" Shehna alimkataza asitoe sauti.
Aliondoa mtandio aliojifunga na kuutupa pembeni kisha alipanda kitandani na kujilaza pembeni kwa Mustafa ambaye alikuwa akitetemeka huku jasho likimtoka, alijiuliza mkewe akiamka na kumkuta mwaname juu ya kitanda chake atamwambia nini. Hali ile Shehna aliiona.
"Mustafa," alimwita kwa sauti ya chini.
"Mmh!" Mustafa alishindwa kutoa sauti.
‘Wasiwasi wako nini?"
"Shehna nakupenda lakini unanitia kwenye matatizo."
"Naomba uniamini hakuna kitu chochote kitakachotokea, mkeo hawezi kuamka mpaka kesho asubuhi."
"Umejuaje?"
"Niamini."
"Sawa," Mustafa alikubali kumridhisha Shehna lakini alitetemeka mpaka utumbo.
Shehna alipomuona Mustafa hayupo naye kimawazo alianza kumpapasa na kulifanya joto lisambae mwili mzima na kujikuta akijisahau kama yupo kwenye kitanda chake na mwisho kuzama kwenye penzi zito ambalo hakuwahi kulipata katika maisha yake.
Shehna pamoja na kuwa mwanamke mrembo pia mapenzi aliyajua kwa kiwango cha hali ya juu. Kama kawaida, Shehna baada ya kupata dozi yake ya mara tatu, aliondoka na kumwacha Mustafa kwenye usingizi mzito.
***
Sara baada ya kuponea tundu la sindano kufukuzwa kazi alijikuta akimchukia Shehna na kumuona ni kiumbe mbaya katika maisha yake. Kabla ya kuja kwake alikuwa akielewana na bosi wake ambaye siku zote alikuwa mpole na mwenye hekima, hakuwahi kumfokea hata siku moja. Lakini toka alipokuja yule mwanamke imekuwa kinyume kabisa.
Alijikuta akikumbuka matukio ya kushangaza toka siku ya kwanza alipoitwa ofisini na Bosi wake kuulizia kama kuna mgeni ameingia ofisini. Tokea hapo amejikuta akikutana na matukio ya ajabu ya kupanda teksi na kujikuta nyumbani na lingine la kulala ofisini kitu ambacho siku za nyuma hakikuwahi kumtokea.
Na tukio la siku ile la kutaka kufukuzwa kazi bila kosa lilizidi kumfanya amchukie sana. Siku ile aliporudi nyumbani alijikuta mwenye hasira nyingi, kila aliyemuona alijua siku ile hayupo vizuri.
Shoga yake wa karibu Happy baada ya kufika nyumbani alimfuata chumbani kumsalimia. Alishangaa kumkuta amekaa kwenye kochi bila kuvua viatu na mkoba wake mkononi huku machozi yakimtoka.
"Shoga vipi mbona hivyo?"
Sara hakumjibu, alichukua kitambaa na kujifuta machozi, hali ile ilimfanya shoga yake adhanie labda amefiwa.

Je, nini kitatokea? Usikose kufuatilia
#LIKE UKURASA HUU UWE KARBU NAMI MWENDELEZO WA HADITHI HII USIKUPITEEE.

0 comments:

Post a Comment