Hadithi ya Kusisimua #Mimba_ya_Jini-13-
Mtunzi: #Mzizi_Mkavu
SASA SKIA ILI USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HII YA KUSISIMUA #LIKE_PAGE HII UWE KARIBU NAMI KIPANDE KINACHOFUATA KISIKUPITE SHARE NIPOST NYINGINE NASUBIRIA #SHARE 250 NIENDELEEE NA HADITHI
ILIPOISHIA...JANA
"Mke wangu tumehangaika sehemu ngapi tumepewa masharti mangapi tuliyoyatekeleza, yaani hili ndilo umeliona gumu?"
"Mi nimechoka kila siku masharti magumu."
"Ha! Mke wangu umeweza kulala makaburini kutafuta mtoto, umeone kazi kutotumia dawa za kizungu ikiwa hali yako ilikuwa nzuri?"
SASA ENDELEA...
"Mume wangu mimi nina wasiwasi huyu mwanamke si mwanadamu!"
"Mke wangu shida yetu mtoto au kujua Shehna ni mtu au jini?"
"Mi simuelewielewi."
"Mke wangu Shehna si jini ni mwanadamu pia si mganga."
"Ni nani?"
"Nimekuambia mtu."
"Kama si jini wala mganga ni nani mbona unataka kutusaidia?"
"Yule dada alipatwa na tatizo kama letu kuna siku nilimsikia akizungumza na mtu jinsi alivyohangaika kutafuta mtoto na kufanikiwa kupata. Nilivutiwa na habari zake na kumuomba anisaidie. Aliahidi kunisaidia na ndicho alichotusaidia, sasa mke wangu kipi kilichokutuma kuniulia mwanangu?" Mustafa alimuuliza akiwa amemkazia macho mkewe.
"Mume wangu sikujua," Husna alikuwa mpole.
"Sasa tutafanya nini? Lazima Shehna tumemuudhi tutafanyaje, kumbuka mke wangu tumehangaika sehemu ngapi hatukuona dalili za mimba hata siku moja. Lakini dawa ya Shehna siku moja na mimba juu."
"Dah! Sijui itakuwaje ukimuona naomba uniombee msamaha, nipo radhi kufuata masharti yoyote atakayonipa."
"Mmh! Sijui!"
"Mume wangu tusitake kujihukumu, najua lazima atapiga simu, naomba umweleze aje nyumbani ili nimuombe msamaha au nimfuate popote."
"Sawa nikimuona au kunipigia simu nitafanya hivyo."
Mustafa alimuaga Husna na kwenda kazini kwa vile alichelewa kutokana na kumfuata mkewe hospitali.
***
Mustafa baada ya kufika ofisini, alijawa na mawazo kuhusiana na matukio yote yaliyokuwa yakimtokea. Bado alikuwa njia panda kutokana na Shehna mwanamke mrembo aliyeonesha mapenzi mazito kwake. Lakini mambo yake yalionekana kama yana muujiza yaliyokuwa kila siku yanamstaajabisha.
Alijiuliza alimjulia wapi mpaka kumpenda kiasi kile, kutokana na mavazi na vito vyote alivyovaa vilikuwa vya thamani kubwa sana. Ilionesha anatoka katika familia yenye uwezo mkubwa sana. Alipanga akikutana naye amuulize vizuri ajue alimuonea wapi na kipi kilichomfanya ampende na kupelekea kutaka kuzaa naye na si mwanaume mwingine.
Sara akiwa bado yupo katika dimbwi la mawazo, sekretari wake aliingia ofisini na kushangaa kumkuta bosi wake amezama kwenye mawazo. Toka aingie ilikuwa ilimeta saa moja bila kugusa kitu zaidi ya kuzama kwenye mawazo. Alimwita na kumfanya ashtuke.
"Vipi bosi mbona upo mbali kimawazo?"
"Wee acha tu, vipi unasemaje?" alijibu huku akifuta mikono usoni na kujinyoosha kama mtu mwenye usingizi au aliyechoka sana.
"Nimekupigia simu ya mezani nashangaa inaita bila kupokelewa, naingia ndani naona upo kwenye dimbwi la mawazo. Unajua bosi siku hizi sikuelewi kabisa inaonekana hapo sawa."
"Nipo sawa, ulikuwa unasemaje?" Mustafa alijibu huku akijiweka sawa kitini na kuiweka sawa Laptop iliyokuwa juu ya meza.
"Kuna mgeni wako."
"Duh! Akili yangu haijakaa sawa mwambie arudi baadaye," alijibu huku akifungua kazi kwenye desktop.
"Lakini mgeni unamjua?"
"Kwani nani?"
"Yule dada mrembo."
"Ooh! Kumbe Shehna mwambie apite."
"Unaona!" Sara alisema huku akitabasamu na kutoka nje.
Mustafa alishtuka na kushangaa kumfuata ofisini ikiwa walilala pamoja na kuachana muda mfupi. Akiwa ameinama alishtuliwa na harufu ya manukato na sauti tamu ya Shehna.
"Asalamu aleykum Mustafa."
"Waleykum salam Shehna."
Alinyanyua uso na kukutana na Shehna akiwa katika vazi la hijabu iliyomziba mwili mzima. Baada ya kuketi aliiondoa nikabu iliyomziba uso na kufanya aonekane vizuri kisha alitikisa nywele zake nyingi nyeusi na kufanya zichanue kama ua huku tabasamu mwanana akilichanua na kumfanya Mustafa kujiona kama yupo ndotoni.
Alitulia na kumtazama Mustafa aliyekuwa ametulia kama mtu aliyekuwa akitazama picha nzuri na kuitikia kama ameitwa.
"Abee mpenzi," Shehna aliitikia bila kuitwa kitu kilichomshtua Mustafa na kumuuliza:
"Shehna mbona unaitikia? Sijakuita."
"Mustafa uniite mara ngapi?"Shehna alimtazama Mustafa usomi huku macho yake makubwa kidogo ya kusinzia yaliyopakwa wanja na kufanya azidi kupendeza. Hakika Shehna alikuwa mrembo wa warembo.
"Haki ya nani Shehna sijakuita," Mustafa alijitetea kwa kuamini toka aachane naye hajapiga simu wala kuonana naye.
"Huna kitu unachotaka kuniuliza?" Shehna alimuuliza huku amemkazia macho ambayo yalizidisha uzuri wake.
Itaendelea ENDELEA KULIKE PAGE HII KIPANDE KINACHO ENDELEA KISIKUPITE SHARE KWA MARAFIKI NIPOST NYINGINE NASUBIRIA #SHARE 250 NIPOST MWENDELEZO
0 comments:
Post a Comment